Tundu Lissu ni tanzi kwa utawala

uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,235
874
Kwa sisi wazee wa imani . ukisoma Yoshua 23: 12- 13. wana wa israel waliambiwa na joshua . wasirudi nyuma ,wasonge mbele kuwaondoa wale wana wa kanaani wote . wakiwaacha itakuwa mtego na kitanzi kwao .

Hoja yangu ni kuwa kwa kuwa wao waliamua kummaliza lissu na ikashindikana . sasa hii imekuwa Tanzi kwao . Huu ulikuwa ni uovu , kumuondoa mwenzako kwa utashi wako na wala si Mungu alivyotaka . Nina imani Kuna jambo kubwa lissu anaenda kufanya .Baada ya kufufuka huku . Iwe ni kukamata uraisi, kuukosa , iwe ni kupiga kampeni . all in all kuna jambo kwa utukufu wa Bwana .

Siku zote Mungu huwa anawatumia watu katika makusudi yake . Wale waliopinda pinda , wale ambao kwa macho ya kibinadamu unaona si perfect . Hata kiongozi wetu mkuu , alikuwa ni mtu aliyeanza majukumu ya siasa kutoka chini sana . kwanza niliwahi kusikia ushuhuda wake , kwa mara ya kwanza alikuwa anapiga kampeni kwa baiskeli . huku akihisi kama anabahatisha ,lakini leo katoboza . Ana good determination .

Nikisoma kitabu cha waamuzi katika biblia . kinaniambia mtu akitoka katika agano na Mungu , madhara ni lazima . kila siku waamaleki na wamoabi watakufukuza tu . swala ni kutubu kwa yale tuliyokosea , hasa damu zilizo mwagika . Kuna familia zina lia kwa wapendwa wao kupotea na kufa . baada ya hapo tusonge mbele .

Tundu Lissu ni mtego na tanzi kwa utawala huu . TUBUNI !
 
kwa sisi wazee wa imani . ukisoma Yoshua 23: 12- 13. wana wa israel waliambiwa na joshua . wasirudi nyuma ,wasonge mbele kuwaondoa wale wana wa kanaani wote . wakiwaacha itakuwa mtego na kitanzi kwa. ... TUBUNI !

Kwa kuwa wewe ni mzee wa imani na mimi nikurejeshe kwenye maandiko matakatifu. Soma Mhuburi Sura ya 10, ila nakutolea mstari mmoja tu ambao unamgusa anayepaswa kutubu.

Mhubiri 10:1 Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.

Jibu lake Mhubiri 10:17 Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.
 
Si haba lisu nae kaingia kwenye historia ya kuwa msindikizaji wa ushindi wa magufuli hakuna kipya
FB_IMG_1596790033084.jpg
 
Acha upumbavu usihusishe kupigwa kwa Lissu na serikali unaushahidi gani kama ndiyo inahusika ilhli kashindwa kwenda kushtaki ili ufanyike upelelezi anakaa kulaumu majukwaani waliomzuru anawajua yeye na ni siri yake usihusishe mungu na ujinga wa lissu
 
Back
Top Bottom