Ungeongeza nyama kidogo kwenye paragraph ya mwanzo kabla ya haya Maandiko ingekuwa vizuri zaidi otherwise yanamuelekea huyu huyu aliyaambiwa hapa atubu hasa hiyo.....
Mhubiri 10:17...
Kwa tafsiri yangu changa ya Maandiko Matakatifu hii Aya inaenda kwa Watanzania moja kwa moja ambao hapa wanasimama kama “Taifa” ikiwaasa kwamba kiongozi wao awe mtu wa watu(kama huyu Lissu) mfano ukiangalia watu walivyojitokeza bila kujali jua au polisi,na hakuna msanii yeyote pale useme wameenda kuangalia wasanii....“na wale kwa wakati ufaao”,kwamba wakati wa upinzani ulikuwa bado na sasa ndiyo zamu yao,“Ili makusudi wapate nguvu”,kwamba wapate nguvu kuwashughulikia wale waliokuwa wakidhulumu nafsi za watu refer B.Saanane,A Gwanda etc...“Wala si kwa ajili ya ulevi”,hakuna ambaye ameona ulevi wa madaraka ktk Taifa hili kama awamu hii,hapo haijamaanishwa ulevi wa gongo sijui bia ila ni ulevi wa kiburi,kujiona wewe ndiye una haki ya kuishi or uwageuze wenzako vilema na kuwapeleka watu jela kwa kesi zisizo na mashiko etc.
Mhubiri 10:1
“Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima”
Hapa sitatia neno sana ila kama kiongozi ukajifanya mpumbavu japo kidogo tu,japo inauma ila hekima na heshima (hasa ya kauli) ukawa nayo hakuna atakayekulaumu,hili andiko Dk Kikwete aliliishi,alitukanwa sana ila hakuna siku ameambia watu kwamba kwa sababu ulichagua mpinzani basi “nenda kamweleze yeye shida zako akutatulie”.
Kwa uelewa wangu mdogo nadhani haya Maandiko yanarudi kwa watawala!