Mkuu
Mchambuzi ni wazi tunakubaliana sana kwenye mengi.However kuhusu mapinduzi,ni wazi kwamba baada ya uchaguzi wa huko zanzibar wa mwaka 1961 mwezi wa january,ASP ilishinda uchaguzi kwa kupata viti 10, ZNP viti 9 na ZPPP viti vitatu.Kwasababu ASP haikufikisha nusu ya kura,ikabidi kutakiwa iwepo serikali ya mseto.Hatahivyo ZPP na ZNP viliungana,na makubaliano(chini ya mwingereza), yakafikiwa kuwa iwepo serikali ya muda(bila ya ASP kushirikishwa) hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika,ambapo ulipangwa kufanyika hapo june 1961(kiukweli Zanzibar ilikuwa haitawaliki).
Kumbuka Abdurahman babu yeye alikuwa ni mwanachama wa ZNP,na kwahiyo kutokana na muungano wao na ZPP,wao ndiyo waliokubaliwa na waingereza kuunda serikali ya mseto.Ambayo iliongozwa na Juma Shamte kama sikosei.Lakini tatizo lilikuja baada ya mwingereza kumshauri awatenge kina Babu kutokana na misimamo yao ya kikomunisti.
Hilo la kutengwa ndilpo lililosababisha Babu akaanzisha chama chake cha UMMA Party,ambapo sasa walishirikiana na ASP kwenye mapinduzi(MORE CREDITS WANAPEWA ASP),lakini chama hicho kikavunjwa rasmi mara baada ya mapinduzi na viongozi hao(kina Babu,Hanga et al),pamoja na wafuasi wao wakajiunga rasmi na ASP chini ya uongozi wa Karume.
Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa kiasi kikubwa ulikuwa hauepukiki,hilo kwa kweli historia itamjudge mwalimu Nyerere pamoja na Karume.Chama cha Karume,kilikuwa na wazanzibari weusi,na kilipigwa vita na hivyo vyama vingine na hata mwingereza alishirikiana na Sultan kuwapiga vita(thanks for the revolution),maana hata huo uhuru wa december 1963,haukuwa uhuru wa watu wa Zanzibar,bali ni madaraka ya nchi yalikabidhiwa kwa Sultan.However jambo la msingi hapa,ni kwamba TANU na ASP vilikuwa vikishirikiana kutokana na hilo la bias ya mkoloni na Sultani,ukweli ukiwa kwamba waarabu na wazungu ndiyo walikuwa wakipendelewa na waafrika kuwa daraja la chini.Hayo yalikuwa mojawapo ya sababu za ushirikiano mkubwa kati ya TANU na ASP.
Sina shaka kabisa kuwa nia ya mwalimu ya muungano ilikuwa njema kabisa,kwasababu mwalimu mwenyewe alishawahi kunakiliwa(Gazeti la Tanganyika Standard la desemba 1964), akisema kuwa ni bora uhuru utolewe kwa block nzima ya Afrika mashariki kama muungano mmoja wa kisiasa,na alikuwa radhi kuona hilo likifanyika hata kama ni kwa kuchelewesha uhuru wa Tanganyika.Maneno hayo aliyazungumza kwenye ile iliyokuwa jumuiya ya wapigania uhuru wa Afrika mashariki na kati(Pan African Freedom Movement fo East and Central Africa-PAFMECA).
Kwenye muungano huu kuna confusions nyingi sana,na hilo siwezi kumlaumu sana mwalimu kwasababu yeye alitaka kuu save muungano huu by any means.Muungano huu una "Hati ya muungano",(Iliyozaa jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar),ambayo ndiyo ilitiwa saini na mwalimu pamoja na Karume,hati hiyo ndiyo ilitumika kwenye uundaji wa katiba ya muungano hapo 1977(ambapo sasa iliitwa jamhuri ya muungano wa Tanzania), pamoja na katiba ya Zanzibar 1984.
Lakini pia kabla ya hapo,tukumbuke pia kwamba mwaka 1964,bunge la Tanganyika lilipitisha sheria ya muungano,na zikathibitishwa na baraza la wawakilishi,lakini bado ukweli unabaki kwamba hawakushirikishwa kwenye utungaji wa sheria hizo.Tatizo walilokuwa nalo Zanzibar,ni kwamba kulikuwa hakuna katiba,bali nchi ikiongozwa na presidential decrees,ikiwa na maana kwamba atakachosema Karume ndiyo sheria,na yeye ndiye mwamuzi wa mwisho on almost everything.
So again,hapo wa kulaumiwa si mwalimu,kwasababu inawezekana Karume ndiye aliyetoa hiyo amri kuthibitisha sheria hizo za muungano kwasababu Karume alikuwa desparate kufanya lolote ili asipate shida ya kuitawala Zanzibar ambayo kiukweli ilukuwa haitawaliki.Na alikuwa akiwaogopa sana mahasimu wake kina Babu,Hanga na wengineo.
Kwahiyo kazi kubwa ya sheria hizo za muungano,ilikuwa ni kuithibitisha ile hati ya muungano pamoja na kutabanaisha muundo wa muungano pamoja na mgawanyo wa madaraka.Na mwaka 1964,mabadilishano ya hati za muungano yalifanyika,Zanzibar ilipata wawakilishi wa baraza la mapinduzi kwenye serikali ya muungano, na walikuwa saba(Abdulrahman Babu,Idris Abdulwakil,Kassim Hanga,Sheick Nasir Moyo,Sheick Aboud Jumbe,na Sheick Hasnu Makame)
Kwasababu Zanzibar walikuwa hawana katiba,ndipo walipo i adopt katiba ya Tanganyika ambayo lifanyiwa marekebisho hapo mwaka 1965,na ndipo ilipokuja na yle maazimio 11.
Kwa kifupi mkuu,mimi nwashangaa sana wazanzibari wasiojielewa,ndiyo maana mwalimu aliwahi kusema nje ya Tanzania,hakuna Zanzibari,na ni ukweli mtupu,hao kina Jussa wanaopigia kelele wakristo,kesho muungano ukivunjika,watatafuta mchawi mwingine kwasababu kisiwa kile hakipo na hakitatawalika nje ya muungano,huo ni ukweli mtupu.
Wataanza kubaguana wapemba na waunguja,weusi na waarabu,kwasababu dhambi ya ubaguzi imo ndani ya damu zao.Na Sultani naye hatocheza mbali,na kwa kawaida,lazima yeye ndiye atakayeshinda,lakini haina maana kwamba amani itakuwepo,kwasababu pia kuna wale weusi ambao lazima watatengwa kwasababu hawatakuwa na haki sawa na waarabu etc.
It is a very volatile situation,na shida ndipo ilipo.Tatizo kubwa ni kwamba sidhani kama muungano wa serikali tatu utatatua tatizo lolote kama serikali hiyo(ya muungano) haitakuwa na mamlaka ya juu zaidi ya yale ya serikali za Zanzibar na Tanganyika kwenye issue za ulinzi na usalama na mambo mengine ambayo yanalalamikiwa kwasasa hivi kwamba yaliongezwa kutoka kwenye yale 11.Kwasababu kuna issue ambazo ili kuendelee kuwepo na amani,ni lazima zibakie chini ya serikali ya muungano,jambo ambalo sidhani kama wazanzibari wanaopinga muungano wanakubaliana nalo.
Issue hii ni issue inayohitaji mjadala haswa.Lakini pia ni muhimu tusipoteze muda mwingi na rasilimali ku fix the unfixable.Ni wazi mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa,na hivyo ni muhimu tuende na wakati tujadiliane upya kuhusu muungano wetu,tuufanyie marekebisho ama hata kuuvunja ikibidi.