Mkuu nguruvi3,
Sera ya CCM ni Serikali Mbili; Italigeuzaje hili kwenda serikali tatu au kuvunja muungano? Kote si itakuwa ni ujumbe kwa umma kwamba chama kilikosea, hasa katika mazingira ya leo ya ushindani ambapo ONE MISTAKE = ONE GOAL?
Nadhani utakubaliana nami kwamba CCM inaangamia kutokana na mambo mawili:
Moja - Kufa kwa Azimio la Arusha na madhara yaliyokuja na Azimio la ZNZ;
Pili - Kuzaliwa kwa Tanganyika iwapo itatokea;
- Je, iwapo CCM watatumia hekima za Nyerere kuhusu muungano, zitasaidiaje CCM at this juncture? Au inaweza jengwa hoja ya kutupia lawama kwa CUF kwamba wamevuruga muungano hivyo tujitenge? Kwa maana nyingine, iwapo itatokea opportunity ya CCM ku - hijack hoja ya Serikali ya Tanganyika kama ilivyo hijack hoja ya Katiba Mpya, suala hili litajitokeza kwa sura ya namna gani?
- Kwanini vyama kama Chadema havijaikamata hoja hii kisawa sawa na kukimbia nayo mpaka kieleweke? Nini mtazamo wako juu ya hili; je hili linakuja au kama ni hoja ya Tanganyika kupitia Chama Cha Siasa, wenye uthubutu ni CCM pekee?
Naomba pia uijadili hoja zifuatazo - hoja hizi sio msimamo wangu, bali hypothetical statements:
- "Iwapo suala la Tanganyika litashindwa kuzuilika, moja ya mambo yatakayoweza tokea ni kuhairishwa kwa uchaguzi mkuu wa 2015, hasa iwapo CCM itabaini kwamba ushindi 2015 ni mgumu";
- Suala la Tanganyika litakuja kupitia amendment kwenye Katiba itakayozaliwa, kwa njia ya hati ya dharura; Na hati hii italetwa na CCM, kwani Chadema au chama kingine cha siasa, pamoja na umuhimu wa Tanganyika, suala hili kwa vyama vingine is more of a political liability than an asset, hasa kutokana na msimamo wa baba wa taifa; Tofauti na vyama hivi, kwa CCM, suala la Tanganyika is both, an asset and a liability;
MKATABA WA MUUNGANOKwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zinafahamu uhusiano wa muda mrefu watu wake na mshikamano na kukuza uhusiano huo na kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa watu wa Afrika, zimekutana na kutafakari Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.
Baina ya
JAMHURI YA TANGANYIKA
Na
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR
Na kwa kuwa Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, zinapendelea ya kwamba Jamhuri hizi mbili ziungane kuwa Jamhuri moja huru moja kwa amasharti ya makubaliano yafuatayo:
Kwa hiyo IMEKUBALIWA baina ya Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar kama ifuatavyo:-
(i) Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa Jamhuri huru moja.
ii) Katika kipindi cha kuanza kwa Muungano mpaka Baraza la Kutunga katiba lililotajwa katika ibara ya (vii) litakapokutana na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano (Kuanzia hapa kitaitwa kipindi cha mpito), Jamhuri ya Muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (iii) mpaka ya (vi).
(iii) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:
a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar;
c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano;
d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.
(iv) Mambo yafuatayo yatakuwa chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano:-
a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
b) Mambo ya nchi za nje
c) Ulinzi
d) Polisi
e) Mamlaka yanayohusika na hali ya hatari
f) Uraia
g) Uhamiaji
h) Mikopo na biashara ya nchi za nje
i) Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
j) Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha
k) Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu
v) Bunge na Serikali vilivyotajwa vitakuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kuongezea mamlaka juu ya mambo yote yahusuyo Tanganyika.
Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri:-
a) Masharti yoyote yatakayowekwa na chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria.
b) Masharti yatakayowekwa kwa amri ya Rais wa Zanzibar juu ya sheria yoyote inayohusu jambo lolote lililotajwa kwenye ibara ya (iv), na kufuta sheria yoyote inayolingana Zanzibar.
c) Mabadiliko yoyote kama yataonekana yanafaa au kuhitajika ili kufanikisha Muungano na mkataba huu.
(vi) (a) Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano atakuwa ni Mwalimu J. K. Nyerere na ataongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kufuata masharti ya mkataba hu na kwa kusaidiwa na maofisa wengine atakaowateuwa toka Tanganyika na Zanzibar na watumishi wa Serikali zao.
b) Makamo wa kwanza wa Rais kutoka Zanzibar aliyeteuliwa kwa kufuata marekebisho kama yalivyoelezwa na ibara ya 3, atakuwa Sheikh Abeid Karume.
(vii) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.
(viii) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.
KWA KUSHUHUDIA HAPA Julius K. Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na abeid Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia saini nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar siku ya tarehe Ishirini na mbili ya mwezi Aprili, 1964.
___________________________
Umepitishwa katika Bunge siku ya tarehe Ishirini na Tano ya Aprili, 1964.
P. MSEKWA
..Karani wa Bunge
Nathibitisha kwamba Muswada wa Sheria hii ulipitishwa na Bunge kwa mujibu wa ibara ya 35 ya katiba.A.S. MKWAWA
.......... ..Spika
25, Aprili 1964.
______________________________________________________________________________________________________
Source: Jumbe, A (1995), The Partner - Ship: Muungano Wa Tanganyika na Zanzibar: Miaka 30 Ya Dhoruba.
Kuhusu hotuba Kamili ya Lissu nitaiwasilisha mara tu nitakapoipata kwani, again, kama nilivyoeleza kwenye my original Post i.e. Post Number 1, hotuba ya Lissu kwa bahati mbaya sana, haipo kwenye Hansard ya Bunge; Vinginevyo hata bila ya hotuba hiyo, hoja yangu inaunga tu mkono hoja ya Lissu juu ya kiini macho cha muungano wetu, vinginevyo nilichowasilisha kinajitegemea;
Nimeipitia kwa umakini mkubwa hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu nikashindwa kuelewa ni kwanini CUF haikuiunga mkono CDM.Wanasiasa ni watu wanafki sana hasa ukimsikiliza Maalimu na Jussa ndiyo unashindwa kuelewa wanataka nini haswaa.
Tatizo kuu wa Wazanzibari (ambao wengi ni Waislamu) ni ubaguzi wa Kidini! Wanaulinganisha Muungano na Ukristo simply kwa sababu ulianzishwa na Nyerere (Mkristo). Fuatilia nchi mbalimbali duniani palipo na Waislamu wengi ndani ya nchi utakuta sera yao kuu ni ugaidi dhidi ya dini nyingine, wakishindwa ni kujitenga!
Tarehe 26 Aprili 1964, yani siku ya muungano, Rais Julius Nyerere alitunga Amri ya rais iliyoitwa "Amri ya Masharti ya Mpito" ya mwaka 1964, iliyochapishwa na gazeti la serikali la siku hiyo.
Amri hiyo iliwabadilisha watu waliokuwa watumishi wa serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na kuwafanya kuwa watumishi wa serikali ya jamhuri ya Muungano. Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano. Na Nembo ya taifa la jamhuri ya Tanganyika iligeuzwa kuwa nembo ya taifa ya Jamhuri ya muungano.
Tarehe hiyo hiyo, Rais Nyerere alitunga Amri nyingine iliyoitwa Amri ya katiba ya muda ya mwaka 1964. Amri hii ilitangaza Katiba ya Tanganyika kuwa ndiyo Katiba ya muda ya jamhuri ya muungano. Kifungu cha (4) cha amri hiyo ndicho kilichoipatia serikali ya muungano majukumu kuhusu mambo yote ya muungano katika jamhuri yote ya muungano na vile vile kwa mambo yasiyokuwa ya muungano kwa upande wa Tanganyika.
Tarehe 15 Juni 1964, Mwalimu Nyerere alitunga Amri nyingine iliyoitwa "Amri ya Masharti ya Mpito (na.2) ya mwaka 1964. Hii ndiyo amri iliyoelekeza kwamba mahali popote ambapo sheria zilizopo zimetaja "Tanganyika" baso jina hilo lifutwe na badala yake jina la Jamhuri ya Muungano liwekwe.
Vile vile Amri hiyo ilielekeza, mahali popote ambapo serikali ya "Tanganyika" imetajwa au kwenye jambo au kit chochote ambacho kwa namna yoyote kinamilikiwa au kinahusishwa na serikali hiyo, basi itachukuliwa kuwa ni serikali ya jamhuri ya muungano ndiyo inatajwa.
Uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za jumla za Amri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndio ilikuwa Tanganyika lilitolewa uhai wake moja kwa moja kwa amri. Hiyo ndio sababu hata jina la eneo la kijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi libadilishwe na kuwa Tanzania Bara.
Pius Msekwa katika kitabu chake kipya kilichotoka mwaka huu kiitwacho:50 Years of Independence: A Concise Political History of Tanzania anasema yafuatayo:
Katika hili la kubadilisha Tanganyika kuwa Tanzania Bara, Aboud Jumbe kupitia kitabu chake cha: The Partnership: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Miaka 30 ya Dhoruba, Mzee Jumbe anaeleza kwamba sheria iliyoleta jina Tanzania Bara badala ya Tanganyika ilikuwa ni sheria namba 24 ya mwaka 1964. Kwa maana hii, amri za Rais kuanza kulifuta jina la Tanganyika, zilikuwa ni jitihada za kuelekea kuhalalisha ufutwaji wa Tanganyika baadae kwa mujibu wa sheria namba 24, 1965.
Baadae tutaanza kuwasilisha nyaraka zote anazojadili Msekwa (nakala) ili tuweze kuona kwa maandisha ni jinsi gani mkataba wa muungano ulichakachuliwa, pamoja na hatima ya Tanganyika.
Cc Nguruvi3, FJM, EMT, Mzee Mwanakijiji, Mtanganyika, zomba Ritz, MwanaDiwani, ZeMarcopolo, MTAZAMO, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, JokaKuu, Mag3, Barubaru
Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Hili ni la msingi sanaMchambuzi,mjadala utakuwa mzuri,ingewezekana tuwekee na hiyo nakala ya hotuba ya Lissu pamoja na mkataba wa muungano wa 1964.(muhimu sana hiyo nakala ya mkataba wa muungano),ili tuone vyema ulivyochakachuliwa na katiba ya muungano ya 1977.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Sheria Namba 18 ya 1965
NAKUBALI J.K NYERERE Rais MACHI 24, 1965 Sheria ya Kuongeza Muda Wa Kuitisha Baraza La Kutunga Katiba Jina Fupi na Tafsiri Sheria Na. 22 1964 GN. Na 243 1964 IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1. Sheria hii inaweza ikaitwa Sheria ya Baraza la Kutunga Katiba ya 1965 na itasomwa kama sheria moja na Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kuongeza muda wa kuteua Tume ya Kuitisha Baraza la Kutunga Katiba 2. Bila ya kuathiri masharti ya Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar au yale ya Mkataba wa Muungano baina ya jamhuri ya zamani ya Tanganyika na Jamhuri ya zamani ya watu wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano hatalazimika kuteua Tume ya kutoa mapendekezo ya katiba kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano, au kuitisha kikao cha Baraza la Kutunga Katiba kwa ajili ya kuyatafakari mapendekezo hayo na kupitisha Katiba, katika kipindi cha mwaka mmoja toka kuanza kwa Muungano isipokuwa Rais kwa kukubaliana na makamu wa Rais ambae ndiye Mkuu wa Serikali ya Zanzibar atateua Tume hiyo na kuitisha kikao cha Baraza la Kutunga Katiba wakati atakaoona unafaa. 3. Bila ya kuathiri masharti ya Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar marejeo ya Sheria hizo kuhusu Baraza la kutunga Katiba lililoitishwa kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha sheria hii lakini kuyafanya yawe yametolewa na Mkataba wa Muungano na kipindi cha mpito kiichoelezwa humi kitaongezwa muda itakavyokuwa. Nathibitisha kuwa Muswada kuwa Sheria hii ulipitishwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya ibaraya 35 ya Katiba. Dar-es-salaam A.S MKWAWA MACHI 24, 1965 Spika Umepitishwa na Bunge siku ya Kumi na Nane Ya Mwezi wa Machi, 1965. P. MSEKWA Karani wa Bunge
Ifuatayo ni moja ya nyaraka za muungano zilizoleta kizaa zaa bungeni kwa mujibu wa vyomba vya habari. Hii ni kuhusiana na baadhi ya wajumbe wa kamati za bunge maalum la katiba kudai kwamba saini za Mwalimu Nyerere na Pius Msekwa zimegushiwa/hazifanani na zile za kwenye nyaraka halisi. Nakala nayoweka hapa chini ni kwa mujibu wa kitabu cha mzee Jumbe (The Partnership) na Kitabu cha Issa Shivji (Panafricanism or Pragmatism). Nakala ya Shivji ni ya kiingereza na ile ya jumbe ni ya kiswahili:
Tutaendelea kuwasilisha nyaraka nyingine mbalimbali, lakini pia kujadili athari za sheria hizi kwa Tanganyika, Zanzibar na Muungano kwa ujumla. Ikumbukwe kwamba sheria na dikrii zote hizi zilikuwa ni kinyume na mkataba wa muungano (1964).
Na kwale wale wanaohitaji kuona Mkataba wa Muungano kama unavyowasilishwa na Shivji (2006) na Jumbe (1995), nyaraka hiyo ipo kwenye bandiko [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=6]#6 [/URL] la mjadala huu. Hotuba ya Lissu ambayo haipo kwenye Hansard, kwa bahati nzuri EMT ametuwekea kwenye bandiko [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=8]#8 [/URL] , lakini pia video yake ipo kwenye bandiko [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=50]#50 [/URL] .
Nawasilisha.
cc Nguruvi3, MTAZAMO, Mzee Mwanakijiji, Pasco, Mtanganyika, zomba, MwanaDiwani, Nape Nnauye, JokaKuu, FJM, ZeMarcopolo, EMT
Ndugu yangu utabadilika lini? Eleza basi kitu cha maana japo siku moja. Hapa watu wanajadili mambo muhimu wewe unaleta hadithi za mitaani. Hiyo kauli tumeisikia miaka 30 kipi cha ajabu.Zanzibar yenye mamlaka kamili inawezekana,muungano ni kama koti...likukubana unaweza kulivua!!!