Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Wapendwa. Kufikiri ni kazi muhimu ya binaadamu. Tatizo au tofauti iliyopo ni kujiuliza kichwa kinafikiri kuelekea wapi, jee kwa manufaa ya mtu na kundi lake au nchi na watu wake na maendeleo ya miaka mingi ijayo.
Kwa masna hiyo nadhani watu wajikite kufikiri kwa faida ya zanzibar ya kesho mana leo ndio tunaishi hata kama tuna matatizo ya ukubwa gani. Lakini future ya Zanzibar ndio muhimu. Kwa hivyo tujiulize wenzetu wanafikiriria kuelekea wapi
 


Sio LAND PRESSURE Pekee... Zanzibar Maeneo Mengi yako UNDER the SEA LEVEL... UZURI ni kuwa BAHARI ya HINDI Hatuna Madhoruba ya HURRICANE kama Bahari zingine lakini kutokana na Matatizo ya HALI ya DUNIA THELUJI kupungua Hauwezi kushangaa ukaona HURRICANE au MVUA kubwa ikainyeshea ZANZIBAR na kusomba ARDHI ya ZANZIBAR... Nadhani umesikia jinsi MAURITIUS nini kilichowapata JUZI JUZI....

Kwahiyo Waache Wajitenge... Uzuri kuna OMAN na YEMEN sidhani kama watakwenda SAUD ARABIA...

ndugu wazenji wangeachwa waende ili roho zao zipate furaha ili na sisi tunaoonekana kunufaika sana na muungano huu tujute,cha mhimu sana tukitengana ni kuweka ulinzi wa kutosha kulinda bandari na fukwe zetu.
 
ndugu wazenji wangeachwa waende ili roho zao zipate furaha ili na sisi tunaoonekana kunufaika sana na muungano huu tujute,cha mhimu sana tukitengana ni kuweka ulinzi wa kutosha kulinda bandari na fukwe zetu.

Ni kweli Kabisa... sasa na AZAM tutamrudisha Zanzibar?
 
"Hili" Lipi... je, unajua maana ya muungano. Okay, je wakati mnaunga huo muungano mliwashilikisha???naona mnatafuta mtoto atafanana na nani wakati mimba ilishatungwa na baba wa mtoto mnamjua...
MliwashiLIkisha!
 
Ni kweli Kabisa... sasa na AZAM tutamrudisha Zanzibar?
anaweza kwenda zanzibar au akabaki kuwa muwekezaji kama walivo wawekezaji wengine wa nje au akachukua uraia,hilo litakuwa juu yake ikitokea hivo ndugu.
 
anaweza kwenda zanzibar au akabaki kuwa muwekezaji kama walivo wawekezaji wengine wa nje au akachukua uraia,hilo litakuwa juu yake ikitokea hivo ndugu.

Akiwa MWEKEZAJI LAND OWNERSHIP itabidi awekewe LIMITATIONS... alivyo na VI-AZAM kila kona Dar; Kwasababu sheria ya Tanganyika Hairuhusu MGENI kumiliki ARDHI itabidi apewa MUDA wa kumiliki; lakini ni bora sababu Zanzibar hawaruhusu watu wa Tanganyika kumiliki ARDHI HUKO...
 
tatizo Zanzibar tukiuvunja muungano tu inakua kambi ya allshababi/ uamusho, kitu ambacho ni hatari kwa jamhuri ya Tanganyika. sababu bahari haitakua salama tena.!!!
 
Watanganyika mnatupenda sana eeh!basi hata tuzame sote kwetu n kwetu,hatuutakiiiiiii........!

ha ha haaa! Nimeipenda hii, nzuri ni kuwa muwe na nchi yenu. Haya mengine matokeo. Mbona wachina wanaishi na kujenga Tanganyika? Piganieni nchi yenu. Sera ya CHADEMA ni serikali tatu. ZENJ iwe dola kamili na Tanganyika iwepo
 
Tatizo kuu wa Wazanzibari (ambao wengi ni Waislamu) ni ubaguzi wa Kidini! Wanaulinganisha Muungano na Ukristo simply kwa sababu ulianzishwa na Nyerere (Mkristo). Fuatilia nchi mbalimbali duniani palipo na Waislamu wengi ndani ya nchi utakuta sera yao kuu ni ugaidi dhidi ya dini nyingine, wakishindwa ni kujitenga!

Kama vile walivyo fanya (wakristu) sudani kusini?
 
Hivi kwanini Tanzania bara tu ndio tunakazania lazima Muungano udumuu ?

Tanzania bara = Mfumo kristo
Zanzibar = Muungano udumu
 
Watalionea wapi hili wamekaa kucheza bao na kuimba taarabu hawana cha ziada
 
Idadi kubwa ya wanachi wa Tanzania ni vijana waliozaliwa miaka ya 70 na kuendelea, kumekuwa na maswali na sintofahamu kuhusu muungano wa Tanzania na Zanzibar wengine wakiuona una manufaa na wengine wakiuona hauna manufaa lakini hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyeweza kujitokeza mbele na kuwaeleza wananchi nini hasa faida za muungano na kwanini kumekuwa na muungano, na kama ni muungano kwanini zinaonekana kama nchi mbili badala ya kuwa nchi moja.

Viongozi hawa wa nchi ya Tanzania wamekuwa kama wanaogopa kuwaeleza wananchi nini hasa kilisababisha muungano na ni kwanini tunaendelea kuwa kwenye muungano, siku za karibuni tumeona purukushani Zanzibar watu wakitaka Zanzibar isiwe sehemu ya muungano kukatoke na vurugu mwishowe ikaonekana kama ni kikundi cha wahuni au magaidi waliotak kuchafua hali ya hewa, kwa viongozi wenye busara, hekima na weledi wangetakiwa kutumia nafasi hiyo kuwaelewesha walewakereketwa nini maana ya muungano. Badala yake walitumia nguvu sehemu ya busara wakifikiri wamezima vuguvugu hilo

Ukimuuliza mwananchi wa kawaida wa Ngara, au hata Kilimanjaro nipe sababu kuu tatu za muungano hawezi kukupa hata moja kwa sababu hakuna anachoelewa, amezaliwa ameukuta na haruhusuiwi kuuhoji maswali japokuwa ni mwanachi wa Tanzania ambayo na Zanzibar imo ndani yake. Kwenye sherehe za muungano tutaona maonesho tofauti tofauti ama ya kivita au gwaride lakini hata siku moja hatuwezi kuona kiongozi akitumia fursa hiyo kujibu maswali au sintofahamu iliyopo miongoni mwa jamii inayoiongoza
Ni jambo la ajabu sana kusema tumeungana huku kukiwa na maswali ambayo viongozi ama hawataki kuyajibu au hawana majibu yake kwa wananchi wake

Rai yangu kwa viongozi wa Tanzania tarehe 26April waitumie siku hiyo kuelezea sababu na faida za muungano na sio kuusifia na maonesho ambayo hata sikukuu ya uhuru tutayaona.
 
Tanganyika bana. Muungano kilema, una upande mmoja tu?
Flag_of_Tanganyika.png

images

tanzania.gif
 
Mkuu Hakuna muungano wa Tanzania na Zanzibar. Labda ingekuwa sahihi zaidi ungesema muungano wa Bara na Zanzibar. Bara na Zanzibar inazaa Tanzania. Viongozi na waasisi wa Taifa hili wamewakosea sana wananchi wa nchi wanayoiita "Bara" kwa kulizika jina la Tanganyika bila utashi wa waliowengi. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ungekuwa na faida kubwa kuliko sasa kama mfumo uliopo ungebadilishwa kuwa muungano wa serikali tatu. Ungekuwa na faida kubwa mno kama muungano ungekuwa wa serikali moja. Muundo wa sasa sio wa hiari bali wa kulazimisha na athari zake zinaonekana wazi. Hakuna utulivu. Manung'uniko ya chinichini kila kukicha.
 
Tunaomba magamba tarehe 26/04/2013 watueleze nchi yetu TANGANYIKA lini ilibadirishwa kuwa Tanzania bara na kwaridhaa ya nani muungano ninaoujua ni kati ya Tanganyika na zanzibar lakini magamba wanatoka povu kutuita watanzania bara kwanini au jina tanganyika kwao tusi!!
Mkuu Hakuna muungano wa Tanzania na Zanzibar. Labda ingekuwa sahihi zaidi ungesema muungano wa Bara na Zanzibar. Bara na Zanzibar inazaa Tanzania. Viongozi na waasisi wa Taifa hili wamewakosea sana wananchi wa nchi wanayoiita "Bara" kwa kulizika jina la Tanganyika bila utashi wa waliowengi. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ungekuwa na faida kubwa kuliko sasa kama mfumo uliopo ungebadilishwa kuwa muungano wa serikali tatu. Ungekuwa na faida kubwa mno kama muungano ungekuwa wa serikali moja. Muundo wa sasa sio wa hiari bali wa kulazimisha na athari zake zinaonekana wazi. Hakuna utulivu. Manung'uniko ya chinichini kila kukicha.
 
Hivi kwani huu ni muungano au shirikisho? Maana sioni maana ya Muungano kama tumeungana kwa mambo 22 tu mengine yoooote hatujaungana.
 
MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ULIO MADHUBUTI.

Inapokalibia siku ya kuanzimisha siku ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar napenda kupongeza waasisi wa muungano huo mzee karume na Kipenzi baba wa taifa mwalimu Nyerere ambao umedumu kwa miaka 49.

miaka 49 ya muungano ni miaka mingi licha ya kupita katika kuchafuka kwa hali ya hewa mara kwa mara na hali hizo kutatuliwa na viongozi wa pande mbili.
imefikia wakati kwa pande mbili za muungano kufikiria nini chanzo cha kuchafua hali ya hewa na kukitatua ili kuongeza mshikamano na umoja katika muungano huu.

Muungano huu baada ya kukumbana na dhoruba nyingi umefia wakati tumalize vyanzo vya manunguniko haya kwa kufanya muungano uwe wa serikali moja.

kuwepo kwa serikali moja utapunguza malalamiko ya pande mbili ambayo ndiyo mwanzo wa mmomonyoka wa undugu, umoja na ushirikiano na amani katika nchi yetu. kwa kufikia muungano wa serikali moja itakuwa imesaidia kuondoa baadhi ya manunguniko kama haya:-
1. Tanganyika kukosa rais wao na hali Zanzibar ina rais wao
2. Tanganyika kukosa makamu wawili wa rais na zanzibar ina makamu wawili wa rais
3. Tanganyika kukosa bunge lake la uwakilishi na Zanzibar ina bunge lake la uwakilishi
4. Tanganyika kukosa mawaziri wake na Zanzibar ina mawaziri wake
5. Tanganyika kukosa waziri kiongozi na Zanzibar ina waziri kiongozi
6. Tanaganyika inabeba mzigo wa kuiendesha serikali ya mapinduzi zanzibar
7. Tanganyika inakosa mamlaka yake kama ilivyo zanzibar
8. Tanganyika raia wake hawana uhuru wa kuishi, kujenga nyumba zanzibar kama wazanzibar wajengavyo Tanganyika
9. Tanganyika raia wake hawana uhuru kufanya biashara zanzibar kama wazanzibar
10. Tanganyika inanyonywa rasilimali zao kwa vile zanzibar hakuna rasilimali
11. Tanganyika wabunge huchaguliwa na wapigakura 200,000 na zanzibar 2,000
12. Tanganyika kuna uhuru wa dini tofauti zanzibar wanaubaguzi kama si muislamu
13. Tanganyika inadaiwa na zanzibar kuikalia nchi hiyo bila idhini ya wazanzabar
14. Tanganyika raia wake hawaruhusiwi kusoma zanzibar kama ilivyo wazanzibar
15. Tanganyika raia wake wananyanyaswa wakiwa zanzibar si kama ilivyo wazanzibar
Pamoja na manunguniko mengi mengine ambayo hata wewe msomaji unayajuwa ndiyo chanzo cha kuchafuka kwa hali ya hewa zanzibar kiasi kwamba inafikia viongozi wakubwa serikali walishawahi kulazimishwa kujiuzuru kwa kudai mabadiliko katika muungano huu. Kwa kufikia MUUNGANO wa SERIKALI MOJA itakuwa ndiyo suruhu ya kero za muungano huu na pia kwa kuwaenzi waasisi wake kuwa na muungano IMARA wa serikali moja na wala siyo serikali mbili au tatu.
Kwa pamoja tutajenga TANZANIA iliyo madhubuti.
 

Attachments

  • nyerere-karume-b03.jpg
    nyerere-karume-b03.jpg
    29.7 KB · Views: 74
  • nyerere-karume-b01.jpg
    nyerere-karume-b01.jpg
    9.2 KB · Views: 210
Back
Top Bottom