Tundu Lissu, Lema watangaza mpango wa kurudi Nchini, Lissu ataja kinachomkwamisha

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu na Mjumbe wa kamati Kuu ya Chama hicho, Godbless Lema wametangaza kuwa watarejea nchini hivi karibuni ili kuendeleza jitihada za kudai Katiba mpya.

Wakizungumza katika kongamano la Baraza la Vijana la CHADEMA (Bavicha) Mkoani Arusha, Mei 21, 2022 wamesema siku ya kurejea itatangazwa na watapokewa kwa uwazi.

Akizungumza kupitia mtandao, Lissu amesema wamekuwa wakiahidi kurejea nchini mara kadhaa lakini kuna vitu vichache bado havijakaa vizuri.

"Lazima tutarejea nchini, tumekuwa tukiahidi kurudi lakini kuna vitu vidogo kuhusiana na masuala ya usalama wetu ila tutakuja tumechoka kukaa ugenini," amesema Lissu.

Amesema siku ya kurejea nchini itatangazwa na watakuwa na mkutano na wananchi na wakifika wataendelea na kazi ya kuimarisha chama kupitia mikutano ya hadhara na Katiba Mpya.

"Mimi na Lema tutarudi pia Wenje na wengine kwa sababu mnajua mazingira tuliyoondokea nchini," amesema

Hata hivyo Lissu amewataka vijana wa CHADEMA kutambua kuwa bado sheria nyingi zilizopitishwa na utawala wa Serikali ya awamu ya tano hazijafutwa.

"Sheria kandamizi bado zipo ila sasa Rais Samia anajitahidi kurejesha mahusiano lakini hatuwezi kujihakikishia usalama wa kufanya siasa bila kuendelea kuzungumza," amesema.

Amesema anaunga mkono jitihada ambazo anafanya Rais Samia Suluhu Hassan kuanza mazungumzo na viongozi wa CHADEMA ili kurejesha mahusiano mazuri katika Taifa.
 
Amesema anaunga mkono jitihada ambazo anafanya Rais Samia Suluhu Hassan kuanza mazungumzo na viongozi wa CHADEMA ili kurejesha mahusiano mazuri katika Taifa.
Safi sana kamanda Lisu. Lisu nakuaminia Sana. Karibu sana nyumbani kwako Tanzania. #TogetherWeCan.

Nakumbuka ulisisitiza mara nyingi sana wakati wa kampeni 2020 kwamba " mwambieni Magufuli asicheze na uchaguzi huu". Magufuli akapuuza na sasa yuko jehanamu.
 
"Lazima tutarejea nchini, tumekuwa tukiahidi kurudi lakini kuna vitu vidogo kuhusiana na masuala ya usalama wetu ila tutakuja tumechoka kukaa ugenini," amesema Lissu.
Tundu Lissu, karibu tuu nyumbani, huna haja ya kuwa na wasiwasi wowote kuhusu usalama wako kwasababu yule YEYE aliyekulinda tokea mwanzo, yupo!.

P
 
Tundu Lissu, karibu tuu nyumbani, huna haja ya kuwa na wasiwasi wowote kuhusu usalama wako kwasababu yule YEYE aliyekulinda tokea mwanzo, yupo!.

P
Paskali jamani.
 
Tundu Lissu, karibu tuu nyumbani, huna haja ya kuwa na wasiwasi wowote kuhusu usalama wako kwasababu yule YEYE aliyekulinda tokea mwanzo, yupo!.

P
Lisu hakikisha usalama wako, hawa akina Pascal usiwasikilize, hawa ni CCM, ni wauaji wakubwa! Ya Kabendera hatuwezi kuyasahau yanatokana na huyu mtu leo anaku assure kuwa uko salama. Achana naye please
 
Tundu Lissu, karibu tuu nyumbani, huna haja ya kuwa na wasiwasi wowote kuhusu usalama wako kwasababu yule YEYE aliyekulinda tokea mwanzo, yupo!.

P
Sijawahi kuonamzee mnafiki na mzandiki kama wewe njaa
 
Back
Top Bottom