Zanzibar 2020 Tundu Lissu: Hatuna maslahi na Urais Zanzibar, tutatangaza rasmi kumuunga mkono Maalim Seif

Chey na Mrema walianza mapema mno na hawakuweka wagombea urais
ACT wanamgombea wao aliefuata mchakato wote,upinzani wa Tanzania utaendelea kushindwa miaka yote kwa ubabaishaji kama huu
Kwan chadema walikua wapi wakati ACT wanaanza mchakato?hii ni dalili ya kunusa kushindwa,wanazinyatia kura za muungano za ACT,halafu wakishindwa watatupa lawama kwa Membe kwamba ni jasusi alikuja kuwavuruga,kumbe wanajivuruga wenyewe
 
“Sisi CHADEMA tumetangaza rasmi kumuunga Mkono Maalim Seif kama ilivyo kwa Cheyo na Mrema kumuunga mkono Magufuli na hili tutatangaza rasmi muda si mrefu"- Tundu Lissu.

"Kama ilivyosahihi kwa Mrema na cheyo kumuunga mkono Magufuli, ni sahihi kwa Maalim Seif na ACT kuniunga mkono na ni sahihi kwa Tundu Lissu na CHADEMA kumuunga mkono Maalim Seif na ACT." Mhe. @TunduALissu.

“Nikichaguliwa kuwa Rais nitaunda Serikali ya Chadema kwasababu ya Katiba inavyosema. Kama kutakuwa na uhitaji itabidi tubadilishe Katiba kwanza, na moja ya maazimio ya Chadema ikishinda Uchaguzi Mkuu ndani ya siku 100 tutaanzisha mchakato wa Katiba mpya.”Tundu Lissu

“Bob Amsterdam ni Mawakili wangu, wanashughulika na maswala yangu yote yakisheria ya ndani na nje ya Nchi. Kama Tume imeandikiwa barua basi Mawakili wangu wamekuwa wakitimiza wajibu wao, Kama nilivyosema uchaguzi mkuu hatutaki mchezo" Tundu Lissu

===
LISSU: HATUNA MASLAHI NA URAIS ZANZIBAR, NDIO MAANA TUNAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF

Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema CHADEMA kumuunga mkono Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo sio ushirikiano

Amesema wao hawatatangaza ‘coalition’ ya vyama vyao bali wataungana mkono kwenye maeneo ambayo hawana maslahi nayo. Amesema hawana maslahi na Zanzibar ndio maana wamemuunga mkono Maalim Seif Shariff Hamad

Amesema wamefanya hivyo kama ambavyo Lyatonga Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP walivyomuunga mkono mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli

Amesema hiyo haikatazwi na sheria. Amesema ni muungano wa vyama ndio unatakiwa kisheria kupeleka barua kwa msajili na wao hawana muungano
Kimenuka !
 
Misimamo inatangazwa mara ngapi? Mara ya kwanza wametangaza mgombea wao wa Uraisi wa Chadema Zanzibar sasa wanakuja na mwingine tena kuwa wanamtaka Seif sharrf Hammad huu utoto
Kwani wamesema wanakuja na mwingine. Lissu kasema yeye anamuunga mkono Maalimu .... Maalimu kasema anamuunga mkono Lissu. Mrema anamuunga mkono Magufuli na Cheyo anamuunga mkono Magufuli .... Vyama vitasema muda ukifika. What's wrong with that? Kinachofanyika hapa ni COLLABORATION na siyo COALITION ...!!
 
hili bango hawakawii kusema lilikuwa la mwaka 2015 kwenye kampeni.
Kuna “2020” kuuuubwa pale. However, hata wakisema ni la 2015 bado ukweli upo palepale. Ni haki ya kikatiba kumuunga mkono umtakaye.

If it is OK kwa TLP na Mrema, then it is OK kwa CHADEMA na Lissu. Hii inaitwa “logic”. Dr. Mahera should understand this clearly
 
Umeshawaona kwenye majukwaaa?
Hao walisema kabala na ndo maana huwaoni wakisimama kupiga kampeni.
Sasa kama mnawaunga mkono ni sawa lakini sio kupanda kwenye jukwaa.
 
Lisu na Amsterdam wataligwa mchana kweupe oktoba 28.

Na ajiandae kurudi kwa beberu wake
 
Hayo magadget waliyomuwekea ni hatari kwa usalama wa taifa akiwa popote iwe ikulu au kituo cha jeshi au ofisi ya usalama wa taifa yanapiga picha na kubeba taarifa za ofisi alipo na kuzipeleka nje kupitia computer ya Amsterdam jasusi LA kimataifa

MTU ana mi gadget ya kijasusi ya mabeberu mwili mzima hafai u amiri jeshi mkuu
Huna facts zozote.
 
aisee hakuna wa kumstopisha Lissu.
Katika watu wenye visasi visivyoisha ukiwakosea ni watu wa kigoma kwa Zito Kabwe na wapemba kwa Maalim Seif

Lisu unakumbuka ulichomfanyia Zito akiwa Chadema? Lisu unakumbuka mlichomfanyia Duni Haji, Mpemba alipokuwa Chadema? Kwa hiyo walishasamehe?

Anyway tunawatakieni muungano mwema wa mashaka wa ACT wazalendo na Chadema

Ila binafsi I smell a rotten rat somewhere
 
Katika watu wenye visasi visivyoisha ukiwakosea ni watu wa kigoma kwa Zito Kabwe na wapemba kwa Maalim Seif

Lisu unakumbuka ulichomfanyia Zito akiwa Chadema? Lisu unakumbuka mlichomfanyia Duni Haji, Mpemba alipokuwa Chadema? Kwa hiyo walishasamehe?

Anyway tunawatakieni muungano mwema wa mashaka wa ACT wazalendo na Chadema

Ila binafsi I smell a rotten rat somewhere
hahaha mataga umepanic mnooo.
nakusihi kunywa maji lita 2 na panodol 4 alafu tafuta sehemu yenye kivuli upigwe na upepo kidogo utakaa sawa.
 
Hana Maslahi na Zanzibar kisha anataka urais.

Lisu hajui timing na hajui ni kea vipi aviteke hata vyombo vya usalama ili vikuunge mkono.
Wewe unayejua timing mbona hukuchukua fomu ya CCM vyombo ya usalama vikuunge mkono.
 
Hayo magadget waliyomuwekea ni hatari kwa usalama wa taifa akiwa popote iwe ikulu au kituo cha jeshi au ofisi ya usalama wa taifa yanapiga picha na kubeba taarifa za ofisi alipo na kuzipeleka nje kupitia computer ya Amsterdam jasusi LA kimataifa

MTU ana mi gadget ya kijasusi ya mabeberu mwili mzima hafai u amiri jeshi mkuu
fear of the unknown!! ugonjwa huu ni mbaya na utawatesa sana Lumumba.
 
Hao wengine Mrema na Cheyo matamko yao yaidhinishwa na kamati kuu zao na mikutano mikuu yao

CHADEMA hilo halipo ni Lissu kujiropokea mwenyewe kwenda mbele
Hivi we umesoma utaratibu wa tume kuhusu vyama kuungana au unabwatuka tu?

Walichokifanya kina Cheyo na Mrema siyo kosa kama ilivyo kwa Chadema na ACT. Jifunze kutofautisha kati ya coalition (muungano) na cooperation (ushirikiano).
 
Wewe unayejua timing mbona hukuchukua fomu ya CCM vyombo ya usalama vikuunge mkono.
Mimi nmemuweka Husein Mwinyi!

Eti sina maslahi na Zanzibar! Kisha anataka vyombo vya usalama vimuunge mkono awe rais.
 
Back
Top Bottom