Lissu: 2020 CHADEMA tulifanya makosa kuteua Mgombea Urais Zanzibar ndio sababu tulijisahihisha na Kumuunga mkono Maalim Seif wa ACT

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,028
142,085
Tundu Lissu amesema Chadema haina urafiki na CCM na hata kinachofanyika kwenye Maridhiano ni kurekebisha makosa yalifanyika awamu ya 4 ikiwemo JK kutukosesha Katiba mpya na makosa ya Awamu ya 5 ya Magufuli

Lisu amesema uungwana ni kukiri makosa na kujirekebisha ndio sababu 2020 Kamati kuu ya Chadema iliteua mgombea Urais wa Zanzibar lakini baadae Uongozi ulibatilisha na Kumuunga mkono Maalim Seif wa ACT Wazalendo

Lisu anasema Chadema kuusimamisha mgombea Urais Zanzibar ni kuibeba CCM kwa sababu Wao na ACT watagawana kura za Wapinzani ukizingatia tofauti ya kura za Ushindi Zanzibar huwa ni mdogo sana

Lisu amesisitiza Chadema haiko tayari kuibeba CCM Katika Mazingira yoyote yale

Source Star tv
 
Back
Top Bottom