Zanzibar 2020 Tundu Lissu: Hatuna maslahi na Urais Zanzibar, tutatangaza rasmi kumuunga mkono Maalim Seif

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271

“Sisi CHADEMA tumetangaza rasmi kumuunga Mkono Maalim Seif kama ilivyo kwa Cheyo na Mrema kumuunga mkono Magufuli na hili tutatangaza rasmi muda si mrefu"- Tundu Lissu.

"Kama ilivyosahihi kwa Mrema na cheyo kumuunga mkono Magufuli, ni sahihi kwa Maalim Seif na ACT kuniunga mkono na ni sahihi kwa Tundu Lissu na CHADEMA kumuunga mkono Maalim Seif na ACT." Mhe. @TunduALissu.

“Nikichaguliwa kuwa Rais nitaunda Serikali ya Chadema kwasababu ya Katiba inavyosema. Kama kutakuwa na uhitaji itabidi tubadilishe Katiba kwanza, na moja ya maazimio ya Chadema ikishinda Uchaguzi Mkuu ndani ya siku 100 tutaanzisha mchakato wa Katiba mpya.”Tundu Lissu

“Bob Amsterdam ni Mawakili wangu, wanashughulika na maswala yangu yote yakisheria ya ndani na nje ya Nchi. Kama Tume imeandikiwa barua basi Mawakili wangu wamekuwa wakitimiza wajibu wao, Kama nilivyosema uchaguzi mkuu hatutaki mchezo" Tundu Lissu

===
LISSU: HATUNA MASLAHI NA URAIS ZANZIBAR, NDIO MAANA TUNAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema CHADEMA kumuunga mkono Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo sio ushirikiano

Amesema wao hawatatangaza ‘coalition’ ya vyama vyao bali wataungana mkono kwenye maeneo ambayo hawana maslahi nayo. Amesema hawana maslahi na Zanzibar ndio maana wamemuunga mkono Maalim Seif Shariff Hamad

Amesema wamefanya hivyo kama ambavyo Lyatonga Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP walivyomuunga mkono mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli

Amesema hiyo haikatazwi na sheria. Amesema ni muungano wa vyama ndio unatakiwa kisheria kupeleka barua kwa msajili na wao hawana muungano

===
LISSU: KILA MTU ANA HAKI YA KULINDWA FARAGHA YAKE
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ame sema katiba ya Tanzania inatamka wazi kuwa kila mtu ana haki ya kulindwa faragha yake

Amesema hayo alipokuwa akijibu swali lilimuhusisha yeye kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Arusha

Amesema maisha ya chumbani na mkeo au yoyote yule ni marufuku kwa serikali kuchungulia. Amesisitiza kuwa kuanza kuchunguzana kunaweza kupelekea hata baadae kusema ‘mbona wewe hufanyi sawasawa’

Kwa hiyo amesema yeye anaunga mkono sheria hiyo, amesema kama serikali inapinga mapenzi ya jinsia moja basi wafute sheria hiyo

===
LISSU: DUNIA HAIHITAJI TANZANIA, TANZANIA INAIHITAJI DUNIA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu amesema dunia haituhitaji ila sisi ndio tunaihitaji dunia na tunapaswa kuweka mahusiano mazuri na dunia yaani mataifa mengine

Amesema hayo akijibu swali la muandishi aliyemuuliza kuhusu tuhuma za kutumika kwake kwa mabeberu. Swali ambalo alijibu kuwa kwa hali ya sasa hata miradi ambayo inajengwa imepata pesa kutoka kwa mataifa ya nje

Amesema bila mataifa ya nje hatuwezi kwenda sehemu. Sasa kama kutumiwa na mabeberu basi hao wanaokopa ili kufanya miradi kama barabara na SGR ndio mabeberu. Ndio maana yeye atafanya serikali yake kuwa marafiki wa mataifa yote

Amesema bidhaa nyingi zinapatikana dunia nzima sio Tanzania pekee, kama ni dhahabu ziko nchi nyingi zinazalisha, chai na bidhaa nyingine halkadhalika. Kwa hiyo ni muhimu kuweka mahusiano sawa ili kupata faida za kiuchumi
 
“Sisi CHADEMA tumetangaza rasmi kumuunga Mkono Maalim Seif kama ilivyo kwa Cheyo na Mrema kumuunga mkono Magufuli na hili tutatangaza rasmi muda si mrefu"- Tundu Lissu.

"Kama ilivyosahihi kwa Mrema na cheyo kumuunga mkono Magufuli, ni sahihi kwa Maalim Seif na ACT kuniunga mkono na ni sahihi kwa Tundu Lissu na Chadema kumuunga mkono Maalim Seif na ACT." Mhe. @TunduALissu.
Ndio hii unasikia waungwana wakisema "Jino kwa jino", au " Ukimwaga mboga namwaga ugali", au "Akupigaye ngumi ya jicho wewe mpige ya sikio. Akikuuliza umeionaje wewe mjibu umeisikiaje?"
 
“Sisi CHADEMA tumetangaza rasmi kumuunga Mkono Maalim Seif kama ilivyo kwa Cheyo na Mrema kumuunga mkono Magufuli na hili tutatangaza rasmi muda si mrefu"- Tundu Lissu.

"Kama ilivyosahihi kwa Mrema na cheyo kumuunga mkono Magufuli, ni sahihi kwa Maalim Seif na ACT kuniunga mkono na ni sahihi kwa Tundu Lissu na Chadema kumuunga mkono Maalim Seif na ACT." Mhe. @TunduALissu.
Sawaa
 
Mtaungana mpaka Mtaungama mwaka huu. CCM mbele kwa mbele.
 
1601456444573.png

Cc: Dr. Mahera
 
“Sisi CHADEMA tumetangaza rasmi kumuunga Mkono Maalim Seif kama ilivyo kwa Cheyo na Mrema kumuunga mkono Magufuli na hili tutatangaza rasmi muda si mrefu"- Tundu Lissu.

"Kama ilivyosahihi kwa Mrema na cheyo kumuunga mkono Magufuli, ni sahihi kwa Maalim Seif na ACT kuniunga mkono na ni sahihi kwa Tundu Lissu na Chadema kumuunga mkono Maalim Seif na ACT." Mhe. @TunduALissu.
Hao wengine Mrema na Cheyo matamko yao yaidhinishwa na kamati kuu zao na mikutano mikuu yao

CHADEMA hilo halipo ni Lissu kujiropokea mwenyewe kwenda mbele
 
Back
Top Bottom