100% Tanzania hakuna kesi kama hizo. Inakuwa kesi kama waliodhulika moja kwa moja kama Lissu ni wengi kwa mamia otherwise nchi zenye migogora muda mrefu viongoz wake wangekuwa walishafungwa siku nyingi i.e Ivory cost, DRC, Sudan, Ethiopia kwa sasa n.kSafi sana Mh. Tundu Lissu umefafanua vyema kuwa taarifa zipo katika dawati la Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ktk Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mjini The Hague Uholanzi yaani ICC- The Hague na zinafanyiwa kazi .
Hiyo ni hatua muhimu ya mwanzo ya ICC The Hague kuchunguza matendo na nyendo za waliopo madarakani (serikalini) kwa mujibu wa Makubaliano ya Mkataba wa Rome wa mwaka 1999 Rome Statute of the International Criminal Court . Mkataba wa Rome unashugulikia manne Mauaji ya kimbari, Makosa dhidi ya binadamu, Makosa ya Kivita, Nchi kuvamia nchi nyingine.
Makosa dhidi ya binadamu yakifanyika mara nyingi dhidi ya wananchi na mara nyingi nayo ni mauaji,kutaka kuangamiza, kuwatia utumwani, kuwahamisha watu , kuwanyima watu huru wao mfano kuwekwa kizuizini kwa namna inayoonesha unawalega kundi fulani, mashambulizi ya ngono, uonevu dhidi ya kikundi kwa sababu ya kisiasa au kidini au rangi au ukabila au ukanda.
Malalamiko dhidi ya Tanzania ni yale ambayo serikali iliyopo madarakani inaonekana kwa makusudi na mbinyo mkubwa inalenga kuumiza kikundi cha watu kwa mindhali ya kisiasa mfano kuwakamata, kuwafunga, kutochunguza kesi, kunyima haki ya dhamana, kukomoa ,kuharibu mali au mashambulizi ya kuumiza mfano viongozi, wagombea, wafuasi wa chama fulani kimekuwa kikishambuliwa n.k
Kwa miaka 5 na mfumo mzima wa serikali ya Tanzania chini ya hatamu za CCM Mpya ikiwemo mihimili yake na taasisi zake za Serikali kuu kutoka Dodoma, Dar es Salaam hadi Zanzibar na serikali za mikoa / wilaya /DEDs kuelekeza nguvu zake zote kukandamiza kikundi fulani na kukiumiza kwa makusudi.