Nimeguswa kwa namna ya pekee na hoja aliyoiwasilisha Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Mhe. Tundu Lissu alipokuwa anachangia hoja Bungeni. Ni kweli, kila kukicha tumekuwa tukisikia ripoti za wizi wa kutisha unaofanywa na serikali yetu dokozi "Creptocrosy Government". Serikali yetu imejipambanua kama serikali dokozi kwa utaratibu wake wa kukumbatia majizi, mafisadi na mahujumu uchumi ya nchi. Ni wizi kila wizara. Je, kwa mfumo huu wa serikali Dokozi tutafika?????Serikali yetu inasifa gani basi ya kutufanya tuendelee nayo????Maendeleo hakuna, Hela haina, wizi kila kukicha, Rasilimali zinaibwa je kazi ya serikali ni nini basi???kwa nini tuendelee nayo ilhali haitunufaishi???jaman kwa serikali hii dokozi 2015 ni mbali sana.
Suala wabunge kulalama badala ya kuisimamia na kuiwajibisha serikali je tutafika????Mimi nadhani ifike mahali wananchi tufanye maamuzi magumu ya kuikomboa nchi yetu. Hii ni nchi yetu sio ya CCM. Kwa kuwa kazi kuu ya Mbunge ni kuwakilisha hoja za wapiga kura wake Bungeni, mimi nadhani tuwaite wabunge wetu majimboni tuwatume wakapige VOTE OF NO CONFIDENCE kwa serikali hii dokozi huko Bungeni. Mbunge atakayekiuka agizo hili la wapiga kura wake basi atafute wapiga kura wa kuwawakilisha huko Bungeni. Hatuwezi tukafika kwa utaratibu huu wa kipumbavu.
Aidha, Katika katiba mpya inabidi wananchi tujipe nguvu ya kuiwajibisha serikali hasa kwenye suala zima la vote of confidence mana naona wabunge katika hili wanatusaliti.