Tundu Lissu aunguruma....Waziri mkuu awajibike

Hili linatakiwa lifanywe na Zitto atakapohitimisha hoja yake. Aweke motion ya kutokuwa na imani na serikali kisha wabunge wa CDM wasibweteke wasimame kuunga mkono tuone kama magamba wataunga mkono? na wananchi waone nani kweli anawatetea.

Naamini Zitto is one of good members wa hapa jamvini, otherwise, kwa wale wenye contacts zake kama e-mail mobile number etc wamjulishe haraka kuhusu hii idea inawezekana jamaa akawa very busy na isiione hii comment hadi siku ambayo atakuwa anafunga mjadala! Please please wadau this is very importnat kujua nani ni mnafiki na nani mkweli!
 
jamani tupeni nukuu za tundu lisu alizosema,bado hatuja wapata vizuri wengine tuko mbali nna bunge
 
Kama kweli wabunge wana uchungu na wanawakilisha wananchi basi wanapaswa kumuunga mkono Tundu Lisu. The guy has a valid point na kweli anaitetea nchi yake kama mbunge na mwanasheria wa kweli!
 
avatar17056_3.gif
 
alicho nena MP Lissu ni cha msingi ila kwa kuwa watz ni wabishi na hatujui nini tufanye na kwa wakati upi.
 
Alichosema Mh.Lissu ni kuwa kila mwaka
Kamati za Bunge za hesabu za serikali zimejaa
Ubadhirifu na wizi mkubwa lakini serikali
Ya CCM iko kimya na haichukui hatua stahili ama
Haichukui hatua kabisa. Hivyo amewaomba wenyeviti
Wa kamati hizo 3 wa move motion ya kupiga
Kura ya kutokuwa na imani na serikali. Pia
Kawaambia wabunge wa CCM kwa kuwa wao wako
Wengi waunge mkono jambo hilo ili serikali
Iwajibishwe kwa manufaa ya nchi.

Isingekuwa kuwa njama za CCM kumweka Tundu Lisu kwenye kesi ambazo hazina msingi, angekuwepo tangu tarehe 10 Aprili basi hadi leo kingekuwa KIMEELEWEKA.

Kudos Tundu Lisu!


Ulishindwa ubeberu na ufisadi nao utashindwa. Tutaenda na Mungu na kumaliza na Mungu.
 
mambo yanazua mambo. Kama kweli wabunge wa CCM ambao ni wengi zaidi bungeni wanaona uchungu jinsi fedha za uma zinavyotafunwa, na jinsi ambavyo serikali haijamuwajibisha hata mtendaji mmoja, basi wapitishe motion ya kutokuwa na imani na mtendaji mkuu ambaye ni waziri mkuu.

source; bunge

Kwa kweli amefanya kweli! Tunataka wabunge wasiouma maneno bali wanayatema mazimamazima maana serikali yetu ni kiziwi. Kwa hiyo, mtu anyeumauma maneno haiwezi kusikia.
 
Wengi walioko serekalini wanatumikia matumbo yao na wale walioko juu yao, hawaitumikii nchi. Wako radhi waue ili washibe wao na familia zao. Wabunge hawa hawana uwezo wowote wa kuinyooshea kidole serekali kwa sababu wakiinyooshea hawamtumikii bosi wao raisi na mwenyekiti wa chama chao. Kwa hiyo ni heri maisha yaende kama yalivyo, wananchi waumie lakini wao na familia zao waendelee kumridhisha bosi wao.
 
Kauri thabiti ya umma ni 'Watanzania wote hatuna imani na serikari', haya wabunge malizieni tuanze upya.
 
Wanachokifanya wabunge wa CCM kurudisha imani kwa wananchi kwa kuwadanganya/kuwazuga kuwa wanakemea mambo hayo lakini waelewe kipofu akishajua anakula na mwingine anakuwa makini sana. Hizo ni mbinu tu wameibuka nazo ili waokoe CCM hata hao wanaohama kutoka CCM hakika kuna malengo yao yakitimia wanarudi lakini ifike mahali wakubali mwisho wa jambo ukifika hata ufanye nini huwezi zuia ni kifo cha kawaida kila kitu au mtu anakipata baada ya muda wa ktumikia jamii ukikamilika. nasema ASILAUMIWE YEYOTE CCM KUFA NI KIFO CHA KAWAIDA TU! PIA WANANCHI WAELEWE RIZIKI KUGAWANA SI KILA SIKU UTAPATA WEWE TU TUJIFUNZE! NI WAKATI CHAMA MAKINI KIONGOZE!
 
WanaJF hao wabunge wa magamba si kuwa wana uchungu kweli ila wana test zari maana wanajua Tv hata kule Misenyi zipo hivyo wanajikomba kwa wapiga kura ili waonekane wamesema neno ndani ya mjengo. Lakini nawaambia hiyo haitoshi kama wamesema na tumewasikia na wanaona kuwa serikali yao sio sikivu basi kuna njia sahihi mbili tu, wachague moja kujiuzuru ubunge au waiwajibishe serikali yao kwa maslahi ya umma.
 
Nakubaliana na taarifa za kamati zote kwa kuibua madudu ya ubadhilifu katika serikali na taasisi zake.Ambayo yamekua yakiibuliwa mwaka nenda mwaka rudi bila kuwawajibisha wahusika,kwa vile imekua kawaida wakati wote pesa nyingi zinatumika kuibua madudu haya lakini hakuna hatua zote zinazochukuliwa.Malalamiko ya wabunge ni siasa wao wanachopashwa kufanya nikuibana serikali kuhusiana na madudu haya.Hivyo kushinikiza serikali kujiuzulu kwa mapungufu yake kushindwa kuchukua hatua kwa madudu haya mwaka nenda miaka rudi.Hii itatoa mfano kwa wahusika kuchulia mambo kwa makini na sio porojo.Vininevyo hatutafika popote MUNGU IBARIKI TANZANIA.

I appriciate...
Kwa hoja kama zako zisizo egemea chama na kuwa na nia ya kujenga na Kuikosoa Serikali yoyote isiyokidhi matakwa ya wananchi..
Hata mwezi hautofika kuitoa serikali iliyoko madarakani..
Keep it up..
 
Ndiyo maana nasisitiza kwenye kauli zangu kuwa Tanzania ya kweli itajengwa na wenye uchungu na nchi hii.
 
Nashauri mmoja wa wabunge wa CHADEMA aanzishe hoja ya kutokuwa na imani na serikali ili tupembue mchele na chuya kutoka wabunge wa CCM kama hasira wanazoonyesha ni za kweli au wanatupiga changa la macho?

changa la macho hilooo.
 
Daah! patamu hapo! jamaa saizi wanatoka moshi tu kwenye masikio!! ha ha ha!
 
haya magamba yameshaona kuwa ccm haina chao 2015 kwa hiyo yanatumia theory ya "chukua chako mapema"
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom