Tundu Lissu aunguruma....Waziri mkuu awajibike

Vijana tunaotoka ktk majimbo ambayo CCM ilishinda tujipange kuwang'oa kwa kuandaa majembe mengine kama Mh. Lisu.
 
Huyu jamaa nimeamini kweli ni jembe ndiyo maana wanafanya wawelalo ili watengue ubunge wake.kila mwaka ripoti ni ile ile hakuna anayechukuliwa hatua,kama kweli wabunge wa ccm walio wengi basi wapige kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.

hakuna mwenye ubavu wa kumchukulia mwenzake hatua vp we hujui issue ten% ww majukwaan watalalama sana
 
Kuna elimu ndogo tu baadhi ya wachangiaji humu JF inabidi tuwe tunapeana. Mtu anaweza kubbisha kwa kujiona pengine ni msomi wa shahada hivyo kaelimika kumbe alihudhuria tu shule lakini angali na shida ya uelewa. Ili mbunge ashiriki vikao kutimiza wajibu wake ana haki ya kulipwa posho ya kujikimu. Hii ndiyo hupokelewa na bwana Zito. Ile ya kukaa yaani siting allowance Zito aliikataa na huwa hapokei. Mtu kama Wiliam Malecela anapotuhumu wabunge wa upinzani kumuoba rushwa na akatakiwa kuthibitisha akazugazuga tu unamuelewaje mtu kama huyu. kwahiyo mtu anatumia hoja hiyo kama ndiyo post ya humu ndani unamshangaa. This is hopeless! Nenda kwa hoja za mashiko bwana not bla bla or gossip!
 
Hawana mamlaka hiyo, ila wanayo ya waziri mkuu....

Katiba yetu inaipatia Bunge mamlaka ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais wa Jamhuri....., Kilichopo ni kwamba mamlaka ipo ila wabunge wa CCM hawana Guts za kufanya hivyo!. Consequence zake ni kuwa na wao wanapoteza ubunge. Rais akitolewa unaitishwa uchaguzi mkuu upya na nafasi zote za kuchaguliwa zinakuwa wazi pamoja na za wabunge.


46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais-

a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama-

a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika sikuthelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais

b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi

(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-

a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;

b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na

c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.

(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa dhidi yake.

(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.

(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.

(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika
kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.

(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na bunge
 
Nashauri mmoja wa wabunge wa CHADEMA aanzishe hoja ya kutokuwa na imani na serikali ili tupembue mchele na chuya kutoka wabunge wa CCM kama hasira wanazoonyesha ni za kweli au wanatupiga changa la macho?
hakuna mbunge wa ccm atakayepiga hiyo kura kaka,kumbuka hata spika hiyo hoja hataisoma maana wote ni wana ccm,kila wanachofanya pale wanakuwa wameshapanga kwenye chama,yaani ni kitu kisichokuwepo alafu hii tabia ya ccm kumfanya rais awe mwenyekiti wa chama ndio wameharibu kabisa ,maana hata akitoka vitafanyika vikao vya chama kuangalia anayefaa utamjibu nini m/kiti wako?yaani haiwezekani na ni ngumu kama jiwe
  • kwa nini upige kura ya kutokuwa na imani na pinda wakati tatizo linajulikana liko kwa rais,kama ni kura iwe kutokuwa na imani na rais,ukimtoa pm watateua tena mwingine mbovu,alafu pinda uongozi wake ni kama botion tu hana mamlaka yeyote jk anaamua yeye binafsi masafari yake ya nje,fikiria swala la posho za wabunge pinda anasema hivi,ikulu inasema tofauti hapo kuna nini?
 
Tundu Lissu nilikuwa nammis sana pale mjengoni. Sasa unganisha Tundu Lissu, Zitto na Mnyika... nahisi kama AG atakimbia bungeni

AG alisema upande wa serikali hawasikilizi wanapiga soga tu Bungeni..fuatilia ansadi...
 
Back
Top Bottom