Tundu Lissu aunguruma....Waziri mkuu awajibike

queen matara

Member
Apr 29, 2011
40
61
mambo yanazua mambo. Kama kweli wabunge wa CCM ambao ni wengi zaidi bungeni wanaona uchungu jinsi fedha za uma zinavyotafunwa, na jinsi ambavyo serikali haijamuwajibisha hata mtendaji mmoja, basi wapitishe motion ya kutokuwa na imani na mtendaji mkuu ambaye ni waziri mkuu.

source; bunge

Nimeguswa kwa namna ya pekee na hoja aliyoiwasilisha Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Mhe. Tundu Lissu alipokuwa anachangia hoja Bungeni. Ni kweli, kila kukicha tumekuwa tukisikia ripoti za wizi wa kutisha unaofanywa na serikali yetu dokozi "Creptocrosy Government". Serikali yetu imejipambanua kama serikali dokozi kwa utaratibu wake wa kukumbatia majizi, mafisadi na mahujumu uchumi ya nchi. Ni wizi kila wizara. Je, kwa mfumo huu wa serikali Dokozi tutafika?????Serikali yetu inasifa gani basi ya kutufanya tuendelee nayo????Maendeleo hakuna, Hela haina, wizi kila kukicha, Rasilimali zinaibwa je kazi ya serikali ni nini basi???kwa nini tuendelee nayo ilhali haitunufaishi???jaman kwa serikali hii dokozi 2015 ni mbali sana.

Suala wabunge kulalama badala ya kuisimamia na kuiwajibisha serikali je tutafika????Mimi nadhani ifike mahali wananchi tufanye maamuzi magumu ya kuikomboa nchi yetu. Hii ni nchi yetu sio ya CCM. Kwa kuwa kazi kuu ya Mbunge ni kuwakilisha hoja za wapiga kura wake Bungeni, mimi nadhani tuwaite wabunge wetu majimboni tuwatume wakapige VOTE OF NO CONFIDENCE kwa serikali hii dokozi huko Bungeni. Mbunge atakayekiuka agizo hili la wapiga kura wake basi atafute wapiga kura wa kuwawakilisha huko Bungeni. Hatuwezi tukafika kwa utaratibu huu wa kipumbavu.

Aidha, Katika katiba mpya inabidi wananchi tujipe nguvu ya kuiwajibisha serikali hasa kwenye suala zima la vote of confidence mana naona wabunge katika hili wanatusaliti.
 
Nimeguswa kwa namna ya pekee na hoja aliyoiwasilisha Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Mhe. Tundu Lissu alipokuwa anachangia hoja Bungeni. Ni kweli, kila kukicha tumekuwa tukisikia ripoti za wizi wa kutisha unaofanywa na serikali yetu dokozi "Creptocrosy Government". Serikali yetu imejipambanua kama serikali dokozi kwa utaratibu wake wa kukumbatia majizi, mafisadi na mahujumu uchumi ya nchi. Ni wizi kila wizara. Je, kwa mfumo huu wa serikali Dokozi tutafika?????Serikali yetu inasifa gani basi ya kutufanya tuendelee nayo????Maendeleo hakuna, Hela haina, wizi kila kukicha, Rasilimali zinaibwa je kazi ya serikali ni nini basi???kwa nini tuendelee nayo ilhali haitunufaishi???jaman kwa serikali hii dokozi 2015 ni mbali sana.

Suala la wabunge kulalama badala ya kuisimamia na kuiwajibisha serikali je tutafika????Mimi nadhani ifike mahali wananchi tufanye maamuzi magumu ya kuikomboa nchi yetu. Hii ni nchi yetu sio ya CCM. Kwa kuwa kazi kuu ya Mbunge ni kuwakilisha hoja za wapiga kura wake Bungeni, mimi nadhani tuwaite wabunge wetu majimboni tuwatume wakapige VOTE OF NO CONFIDENCE kwa serikali hii dokozi huko Bungeni. Mbunge atakayekiuka agizo hili la wapiga kura wake basi atafute wapiga kura wa kuwawakilisha huko Bungeni. Hatuwezi tukafika kwa utaratibu huu wa kipumbavu.

Aidha, Katika katiba mpya inabidi wananchi tujipe nguvu ya kuiwajibisha serikali hasa kwenye suala zima la vote of no confidence mana naona wabunge katika hili wanatusaliti.
 
Huyu jamaa nimeamini kweli ni jembe ndiyo maana wanafanya wawelalo ili watengue ubunge wake.kila mwaka ripoti ni ile ile hakuna anayechukuliwa hatua,kama kweli wabunge wa ccm walio wengi basi wapige kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
 
kwani ni lazima uwe mbunge wa ccm? kwanza kwa sasa kimeishapoteza mvuto unahamia Airtell a.k.a CDM then 2015 unarudi bungeni tena kwa kishindo unawapiga mawe ya kutosha na kuwazomea kabisa
 
Nakubaliana na taarifa za kamati zote kwa kuibua madudu ya ubadhilifu katika serikali na taasisi zake.Ambayo yamekua yakiibuliwa mwaka nenda mwaka rudi bila kuwawajibisha wahusika,kwa vile imekua kawaida wakati wote pesa nyingi zinatumika kuibua madudu haya lakini hakuna hatua zote zinazochukuliwa.

Malalamiko ya wabunge ni siasa wao wanachopashwa kufanya nikuibana serikali kuhusiana na madudu haya.Hivyo kushinikiza serikali kujiuzulu kwa mapungufu yake kushindwa kuchukua hatua kwa madudu haya mwaka nenda miaka rudi.Hii itatoa mfano kwa wahusika kuchulia mambo kwa makini na sio porojo.

Vininevyo hatutafika popote MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Tundu Lissu nilikuwa nammis sana pale mjengoni. Sasa unganisha Tundu Lissu, Zitto na Mnyika... nahisi kama AG atakimbia bungeni
 
Kama kweli magamba wana machungu na nchi hii basi waiwajibishe serikali yao ili kuleta heshima kwa bunge letu.
 
Kweli nimeamini watanzania wanafiki. Wanalalamika serikali dokozi halafu wao wenyewe wanaomba rushwa!!!! Je tutafika. Anzeni wenyewe wapinzani kuwa waadilifu mtapata nguvu ya kuiangusha serikali dokozi. Vyenginevyo mnampigia mbuzi gitaa bure!!!!
 
Ni kweli kabisa, huu si wakati wa kuendelea kulalamika, ni wakati wa kuchukua hatua ili iwe fundisho kwa watakaokuja. Big up Tundu. Hii inakuwaje! Wananchi, walalamike, hata nyie Wabunge ambao mlio na silaha ya kuadhibu mlalamike!
Hapana, jamaa lazima wawajibishwe.
 
Nyerere Vicent, Lianzishe. Maana ushahidi wa ufisadi wa serikali unafahamika.

Please please please

CDM for Ever
Quality
 
mambo yanazua mambo. Kama kweli wabunge wa CCM ambao ni wengi zaidi bungeni wanaona uchungu jinsi fedha za uma zinavyotafunwa, na jinsi ambavyo serikali haijamuwajibisha hata mtendaji mmoja, basi wapitishe motion ya kutokuwa na imani na mtendaji mkuu ambaye ni waziri mkuu.

source; bunge
Nimefungua hii thread kutaka kujua Tundu Lissu amesema nini? Cha ajabu nakuta story nyingine kabisa, kulikoni?
 
Hoja ya kutokuwa na imani na serikali itolewe mara moja ili JK akatishe ziara yake kuja kuokoa jahazi!
 
Wabunge wetu nguvu ya soda, hasa hawa wa magamba kwa wakati huu ambapo chama chao kinaendelea kupoteza mvuto kwa wananchi, wanachofanya sasa ni sawa na mbwa mwoga, kubweka kwa ukali na sauti ya juu sana, lakini mwisho wa siku anaufyata na kujichimbia kibandani kwake as if hajaona mwizi ama hatari.

Ngoja waendelee kushindwa kutumia mamlaka yao ya kikatiba na kuwaachia viongozi wake wanaifilisi nchi lakini watambue kwamba uchaguzi ujao watasimama kizimbani kujibu tuhuma zao.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom