Tundu Lissu aunguruma....Waziri mkuu awajibike

Kweli nimeamini watanzania wanafiki. Wanalalamika serikali dokozi halafu wao wenyewe wanaomba rushwa!!!! Je tutafika. Anzeni wenyewe wapinzani kuwa waadilifu mtapata nguvu ya kuiangusha serikali dokozi. Vyenginevyo mnampigia mbuzi gitaa bure!!!!

Una ushahidi wa hayo mameno yako au unabwabwaja bwabwaja tu hapa. Kila siku ushahidi unapelekwa bungeni na kamati za bunge pamoja na AG kwamba watumishi wa serikali na viongozi wao wanaiba pesa za umma. Wewe ushahidi wako nini? Kajipange upya
 
Nashauri mmoja wa wabunge wa CHADEMA aanzishe hoja ya kutokuwa na imani na serikali ili tupembue mchele na chuya kutoka wabunge wa CCM kama hasira wanazoonyesha ni za kweli au wanatupiga changa la macho?

Ungekuwa karibu ningekupa tano !
 
Una ushahidi wa hayo mameno yako au unabwabwaja bwabwaja tu hapa. Kila siku ushahidi unapelekwa bungeni na kamati za bunge pamoja na AG kwamba watumishi wa serikali na viongozi wao wanaiba pesa za umma. Wewe ushahidi wako nini? Kajipange upya


Wewe vipi? hukusikia jana William MAlecela a.ka the mutuz alivokuwa akisema ! inawezekana wapinazni either wametoa rushwa au wamepokea hilo ni wazi ! na yeye akasema haamini ! wewe upo wapi?
 
katiba mpya itamke wazi siruhusa mwana ccm kugombea cheo chochote ktk jamhuri yetu!miaka 51 hawajafanya lolote

Hiyo ngumu. Tutakosa kuwaona magamba yanayoongoza kulala bungeni! na wengine tulioambiwa wanafanana na nyan....tehe! tehe!
 
Nimeguswa kwa namna ya pekee na hoja aliyoiwasilisha Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Mhe. Tundu Lissu alipokuwa anachangia hoja Bungeni. Ni kweli, kila kukicha tumekuwa tukisikia ripoti za wizi wa kutisha unaofanywa na serikali yetu dokozi "Creptocrosy Government". Serikali yetu imejipambanua kama serikali dokozi kwa utaratibu wake wa kukumbatia majizi, mafisadi na mahujumu uchumi ya nchi. Ni wizi kila wizara. Je, kwa mfumo huu wa serikali Dokozi tutafika?????Serikali yetu inasifa gani basi ya kutufanya tuendelee nayo????Maendeleo hakuna, Hela haina, wizi kila kukicha, Rasilimali zinaibwa je kazi ya serikali ni nini basi???kwa nini tuendelee nayo ilhali haitunufaishi???jaman kwa serikali hii dokozi 2015 ni mbali sana.

Suala wabunge kulalama badala ya kuisimamia na kuiwajibisha serikali je tutafika????Mimi nadhani ifike mahali wananchi tufanye maamuzi magumu ya kuikomboa nchi yetu. Hii ni nchi yetu sio ya CCM. Kwa kuwa kazi kuu ya Mbunge ni kuwakilisha hoja za wapiga kura wake Bungeni, mimi nadhani tuwaite wabunge wetu majimboni tuwatume wakapige VOTE OF NO CONFIDENCE kwa serikali hii dokozi huko Bungeni. Mbunge atakayekiuka agizo hili la wapiga kura wake basi atafute wapiga kura wa kuwawakilisha huko Bungeni. Hatuwezi tukafika kwa utaratibu huu wa kipumbavu.

Aidha, Katika katiba mpya inabidi wananchi tujipe nguvu ya kuiwajibisha serikali hasa kwenye suala zima la vote of confidence mana naona wabunge katika hili wanatusaliti.

Nakuunga mkono mkuu. Wananchi tunawachagua wabunge kutuwakilisha, hivi katiba yetu inasema nini jinsi ya wananchi kuwawajibisha hawa wabunge kabla ya muhula mwingine wa uchaguzi? Hiki kipengele kitakuwa muhimu sana katika kutoa msukumo kwa bunge kuiwajibisha serikali na hata kuleta maendeleo kwa kasi ya hali ya juu. Maana sioni mantiki ya wao kuogopa viongozi wa chama chao kuliko wananchi.
 
Wewe vipi? hukusikia jana William MAlecela a.ka the mutuz alivokuwa akisema ! inawezekana wapinazni either wametoa rushwa au wamepokea hilo ni wazi ! na yeye akasema haamini ! wewe upo wapi?

Taja mbunge mmoja wa upinzani aliyepokea rushwa kutoka kwa wagombea. As for William Malecela allegation hajamtaja hata mbunge mmoja == muongo, mbea na mzushi. As for you huoni mbali zaidi ya urefu wa pua yako.

Hustahili kupotosha mjadala jifunze uchangiaji makini toka kwa wachangiaji wengine wenye busara.
 
Creptocrosy Goverment > hili neno linavyoudhi! laiti ningekua waziri mkuu ningebwaga manyanga
 
Nimefungua hii thread kutaka kujua Tundu Lissu amesema nini? Cha ajabu nakuta story nyingine kabisa, kulikoni?

Alichosema Mh.Lissu ni kuwa kila mwaka
Kamati za Bunge za hesabu za serikali zimejaa
Ubadhirifu na wizi mkubwa lakini serikali
Ya CCM iko kimya na haichukui hatua stahili ama
Haichukui hatua kabisa. Hivyo amewaomba wenyeviti
Wa kamati hizo 3 wa move motion ya kupiga
Kura ya kutokuwa na imani na serikali. Pia
Kawaambia wabunge wa CCM kwa kuwa wao wako
Wengi waunge mkono jambo hilo ili serikali
Iwajibishwe kwa manufaa ya nchi.
 
Kweli nimeamini watanzania wanafiki. Wanalalamika serikali dokozi halafu wao wenyewe wanaomba rushwa!!!! Je tutafika. Anzeni wenyewe wapinzani kuwa waadilifu mtapata nguvu ya kuiangusha serikali dokozi. Vyenginevyo mnampigia mbuzi gitaa bure!!!!

Kitu cha kwanza kujiuliza ni hayo maneno ni ya kweli au uongo!! Kama ni kweli then action lazima zichukuliwe mara mmoja na si kuanza kusema oh upinzani waanze kujirekebisha kwanza. So far hakuna tuuhuma za rushwa zilizohusishwa na upinzani kuanzia uchaguzi mkuu mpaka leo........... Hayo maneno ya William hayana mshiko. Kila siku tunajua nani anatoa rushwa kwenye uchaguzi. Si ulisikia jinsi opinion polls za CCM Arumeru zilivyoleta kasheshe kwa ajili ya rushwa mpaka uchaguzi ikabidi urudiwe. Si ulisikia ni jinsi gani Mwigulu alivyo kuwa akigawa pesa kule Arumeru....... Sasa hao wapinzani mbona hatujasikia story yeyote. So far waliozungumzia rushwa kwenye uchaguzi wa EALA ni CCM wao kwa wao. Sasa sijui wapinzani unataka waanze kujisafisha vipi?? Au mwezetu unafaidika na hayo mashangingi ya Tillion 5!!
 
Lukolo,

katika maneno yote aliyoyasema Tundu Lissu bungeni leo wakati akitoa mchango wake, nimejaribu ku--summerize na kuandika hayo machache ambayo ndio aliyoyakusudia kubeba ujumbe mzito.. Ni bahati mbaya kwako kama hukuona kilichojiri bungeni leo.
 
Nashauri mmoja wa wabunge wa CHADEMA aanzishe hoja ya kutokuwa na imani na serikali ili tupembue mchele na chuya kutoka wabunge wa CCM kama hasira wanazoonyesha ni za kweli au wanatupiga changa la macho?

Kama wameitisha kikao cha dharura hao magamba tusubiri watakuja na motion ipi!
In fact serikali imekaliwa vibaya hakuna pa kutokea
 
Hivi CCM wanashindwa nini kuzuia wabunge wake kuhudhuria vikao vya Bunge? Au kuzuia Bunge lisifanye vikao kabisa? si ndio huwa wanatamba kwamba wanaongoza serikali hawa? wapi Nape Kwanza?
 
kipugala

Namuunga mkono Mh.Lisu na Wabunge wote wenye mawazo na uchungu na nchi hii uvumilivu dhidi ya serikali isiyo na huruma na mapenzi ya dhati kwa watu wake umefikia mwisho;wanadharau bunge,wanadharau wapiga kura wao pia wanamdharau Mwenyezi MUNGU tuwatose labda watajifunza.
 
Back
Top Bottom