Pendekezo: Posho na mshahara wa mbunge, usizidi milioni 5 Kwa mwezi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
16,907
25,677
Salaam, Shalom!!

Niliwahi kuandika thread isemayo, Wabunge wafanyabiashara matajiri wanasimamia Maslahi ya nani bungeni?

Haijaisha miezi SITA tangu kuandikwa thread hiyo, tayari Kuna tetesi kuwa Wabunge wamejiongezea posho na marupurupu Yao Kutoka ml 13 Hadi ml 15 Kwa mwezi.

Mbunge anayeona posho na marupurupu ya ml 13 kuwa haitoshi, huyo hawezi kamwe kutosheka. Na watu Hawa, lazima ni matajiri wakubwa walioacha biashara zao na kwenda bungeni wakidhani bungeni Pana maslah binafsi ya kiuchumi.

KAZI ya ubunge ni KAZI ya season, Si ajira ya kudumu, lazima uwe na KAZI Yako ,bungeni unaenda kutetea Maslahi ya wananchi, wabunge wanaodhani kuwa ubunge ni ajira ndio wanatuletea shida.

Pale Uingereza, mbunge anapanda treni ya umma kwenda bungeni, gari yake binafsi anatumia akiwa jimboni kwake na umma hawajibiki kumlipia mambo lukuki kama huku.

Mshahara na marupurupu usizidi ml 5 Kwa mwezi, na mbunge lazima awe na KAZI yake, bungeni pasifanywe ajira.

Wabunge wapande mabasi kama raia wengine waendapo Dodoma, Kodi zetu zisitumike kulipa mshahara wa dereva, mbunge akitaka gari, akopeshwe na alipe Yeye mwenyewe na ajigharamie gharama za mafuta.

Tunachagua wabunge Ili wasaidie wananchi tupate bima walau za watoto chini ya miaka mitano iliyofutwa Ili kujazia pesa za kulipa wabunge ml 18 Kwa mwezi na kulipa wake wa wastaafu.

Wabunge oneni Aibu na muwe na huruma Kwa wananchi.

FAIDA ZA KULIPA MISHAHARA YA WABUNGE CHINI YA ML 5 KWA MWEZI.

1. Itasaidia wabunge wazalendo kuingia bungeni.

2. Itapunguza wizi wa kura.

3. Itasaidia kujipunguzia Serikali Mzigo kuhudumia wabunge, Badala yake, pesa hizo zitasaidia kulipa posho walimu mashuleni Ili wafundishe Kwa Ari na morali zaidi.

Hivi wabunge jiulizeni, bodaboda, matching guys ,wakulima, wavuvi ambao Kwa mwezi hawapati hata laki 5 Kwa mwezi, wamepata wapi uwezo kuwalipeni wabunge 399 , milioni 18 Kwa mwezi=7 bilion?

Mkiendelea na uroho huo, tutasusia mikutano yenu na hatutowapigia kura!!

KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa, wabunge wamedhihirisha wazi kuwa hawaangalii maslah ya Wananchi maskini, wanajiangalia wao na familia zao.

Pia wabunge wazuiwe kujiongezea mshahara bila kupata ridhaa ya walipakodi.

Karibuni 🙏
 
KAZI ya ubunge ni KAZI ya season, Si ajira ya kudumu, lazima uwe na KAZI Yako ,bungeni unaenda kutetea Maslahi ya wananchi, wabunge wanaodhani kuwa ubunge ni ajira ndio wanatuletea shida.
Mimi napendekeza wasilipwe posho zaidi ya pesa kama perdiems na wafanye retirement kama wafanyavyo watu wengine. Pale bunge CCM wamepageuza kichaka cha uhalifu
 
Kama haitapatikana KABLA ya uchaguzi zingatia neno KABLA
Ikiwa haitapatikana KABLA,

Tuhakikishe uchaguzi haufanyiki.

Wizi wa kura Mtwara katika marudio ya udiwani umetuonyesha kuwa wizi wa kura uTAENDELEA.

Na wezi wa kura, ndio Hawa wanajiongezea mishahara wakati huku.mtaani, watu wanapoteza ajira na biashara kufilisika Kila kukicha sababu ya Hali ngumu ya maisha .

Tuamke Watanzania.
 
Mimi napendekeza wasilipwe posho zaidi ya pesa kama perdiems na wafanye retirement kama wafanyavyo watu wengine. Pale bunge CCM wamepageuza kichaka cha uhalifu
Yaani wamegeuza Eti Ile kama ajira.

Wasivyo na Aibu wanajilipa kiinua mgongo kana kwamba Ile ni ajira ya kudumu.

Ubunge ni seasonal job, hata mwalimu anaweza ifanya.

Miezi ya kwenda bungeni unakabidhi, unaenda, ukirudi, unaendelea na chaki.

Hawa ndio wanaifilisi Nchi!!
 
Umeongea fact sana mkuu. Kuna mambo mengi sana ya kuweka sawa nchi hii lakini mijitu yenye dhamana ndio kwanza imeanza na uMIMI, haitosheki kabisa.

Njia pekee ya kutunusuru na huu upumbavu ni MACHAFUKO pekee
Hilo halikwepeki,

Ikiwa kura zinaibwa wazi wazi bila kificho,

Inamaana IPO siku, drug dealer au muuza bangi anaweza kuwa kiongozi mkubwa wa Nchi Kwa kununua kura Kwa pesa chafu Ili akajilipe bungeni au wizarani.

Ikiwa tumeshindwa kufuata HAKI kuongoza nchi,

Ifike time wananchi tuchukue hatamu!!
 
Salaam, Shalom!!

Niliwahi kuandika thread isemayo, Wabunge wafanyabiashara matajiri wanasimamia Maslahi ya nani bungeni?

Haijaisha miezi SITA tangu kuandikwa thread hiyo, tayari Kuna tetesi kuwa Wabunge wamejiongezea posho na marupurupu Yao Kutoka ml 13 Hadi ml 15 Kwa mwezi.

Mbunge anayeona posho na marupurupu ya ml 13 kuwa haitoshi, huyo hawezi kamwe kutosheka. Na watu Hawa, lazima ni matajiri wakubwa walioacha biashara zao na kwenda bungeni wakidhani bungeni Pana maslah binafsi ya kiuchumi.

KAZI ya ubunge ni KAZI ya season, Si ajira ya kudumu, lazima uwe na KAZI Yako ,bungeni unaenda kutetea Maslahi ya wananchi, wabunge wanaodhani kuwa ubunge ni ajira ndio wanatuletea shida.

Pale Uingereza, mbunge anapanda treni ya umma kwenda bungeni, gari yake binafsi anatumia akiwa jimboni kwake na umma hawajibiki kumlipia mambo lukuki kama huku.

Mshahara na marupurupu usizidi ml 5 Kwa mwezi, na mbunge lazima awe na KAZI yake, bungeni pasifanywe ajira.

Wabunge wapande mabasi kama raia wengine waendapo Dodoma, Kodi zetu zisitumike kulipa mshahara wa dereva, mbunge akitaka gari, akopeshwe na alipe Yeye mwenyewe na ajigharamie gharama za mafuta.

Tunachagua wabunge Ili wasaidie wananchi tupate bima walau za watoto chini ya miaka mitano iliyofutwa Ili kujazia pesa za kulipa wabunge ml 18 Kwa mwezi na kulipa wake wa wastaafu.

Wabunge oneni Aibu na muwe na huruma Kwa wananchi.

FAIDA ZA KULIPA MISHAHARA YA WABUNGE CHINI YA ML 5 KWA MWEZI.

1. Itasaidia wabunge wazalendo kuingia bungeni.

2. Itapunguza wizi wa kura.

3. Itasaidia kujipunguzia Serikali Mzigo kuhudumia wabunge, Badala yake, pesa hizo zitasaidia kulipa posho walimu mashuleni Ili wafundishe Kwa Ari na morali zaidi.

Hivi wabunge jiulizeni, bodaboda, matching guys ,wakulima, wavuvi ambao Kwa mwezi hawapati hata laki 5 Kwa mwezi, wamepata wapi uwezo kuwalipeni wabunge 399 , milioni 18 Kwa mwezi?

Mkiendelea na uroho huo, tutasusia mikutano yenu na hatutowapigia kura!!

KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa, wabunge wamedhihirisha wazi kuwa hawaangalii maslah ya Wananchi maskini, wanajiangalia wao na familia zao.

Pia wabunge wazuiwe kujiongezea mshahara bila kupata ridhaa ya walipakodi.

Karibuni 🙏
Ndugu yangu Pascal Mayalla kuna kipindi aliwahi kugombani hiyo nafasi lakini haikuwa bahati yake, leo hii ungekuta na yeye ni mmoja wa wanufaika katika hili sijui upi ungekuwa msimamo wake katika hili unalolisemea.

Kosa kubwa tunalolifanya watanzani kwa kulazimishwa na mfumo, ni kuwapa madara maskini na haya ndio maskini yanayoyasanya wakiwepo madarakani...

Mbunge ukiona anaugombania Ubunge, kwanchi maskini ujue huyo ni jobless hana source ya fund ambayo iko stable inayompa financial freedom yake kufanya mambo yake binafsi. Anafanyaje sasa, inabidi aingie kwenye siasa kuwaibia wananchi kwa kivuli chakuwatetea
 
Hawa matajiri kwanini hawajitolei?

Mbunge tajiri, Abuud au kishimba, bungeni anachukua posho au mshahara wa KAZI Gani?

Wabunge matajiri wanatakiwa wajitolee, wakatae posho na mishahara, watumie pesa zao kulipa madreva wao, wajigharamie mafuta nk nk.

Ikiwa hakuna tajiri hata mmoja mbunge bungeni aliyekataa posho na mshahara,

Jua kuwa hakuna tajiri hapo, wote mafisi tu!!

Utajiri wao Si wa HAKI!!

Utajiri wao ungekuwa wa HAKI, wangeridhika.
 
Ndo maana nakubaliana na mleta mada. Pale kwenye point yake #1 anasema mishahara ikiwa 5m au less, itatupatia wabunge wazalendo.

Kwa kiasi kikubwa yuko sahihi, kwasababu kabla hata hawajajiongezea mishahara, tayari walikuwa wanalipwa pesa nyingi. Kwa tajiri mkubwa, hawezi kupoteza muda wake kwa ajili ya milioni 5 kwa mwezi.

Kwasababu huwa wanatumia pesa nyingi kuweza kuchaguliwa, na kwahiyo ni kama biashara hapo wanawekeza kwenye ubunge.

Kwa muda atakaokuwa bungeni akitoka ana zaidi bilioni. Na hapo labda ametumia milioni 100 kuupata ubunge.
 
Kwa sasa kitita cha fedha kwa mbunge :

Mshahara wa mbunge ni zaidi ya bilioni moja akitumika miaka 5 (miezi 12 x 5 ) ktk kikokotoo:

Mchanganuo wa mshahara wa miaka mitano wa mbunge ni Bilioni 1 na milioni themanini :

Shilingi 18,000,000 x miezi 12 = 216,000,000

Shilingi 216,000,000 × miaka 5 =1,080,000,000

  • Bado hapo pia anapokea allowance za vikao vya bajeti
  • Ziara za mafunzo Dubai, India n.k
  • Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge PAC, LAAC, Mambo ya Nje na ulinzi usalama n.k
  • Marupurupu ya mkopo wa gari n.k
  • Bima ya Afya kwa mbunge hospitali VIP Class n.k
  • Pensheni ya mkupuo akimaliza ubunge miaka
 
1711318476106.png
 
Hapa naona tatizo ni ccm inafanya kuwahonga wabunge wapige tu meza kupitisha ufisadi kwa maslahi ya mafisadi mfano kuuza nchi nk nk.

Bunge tunasema ni rubber stamp. Lakini ni zaidi ya rubber stamp. Wabunge ni washiriki wa uhalifu na ni wahujumu wa Taifa.

Hakuna mijadala ya maana zaidi ya porojo, lakini unashangaa miswada ya kuuza nchi na kuzidi kukandamiza demokrasia na maslahi ya Taifa ikipitishwa tu kimya kimya.
 
Salaam, Shalom!!

Niliwahi kuandika thread isemayo, Wabunge wafanyabiashara matajiri wanasimamia Maslahi ya nani bungeni?

Haijaisha miezi SITA tangu kuandikwa thread hiyo, tayari Kuna tetesi kuwa Wabunge wamejiongezea posho na marupurupu Yao Kutoka ml 13 Hadi ml 15 Kwa mwezi.

Mbunge anayeona posho na marupurupu ya ml 13 kuwa haitoshi, huyo hawezi kamwe kutosheka. Na watu Hawa, lazima ni matajiri wakubwa walioacha biashara zao na kwenda bungeni wakidhani bungeni Pana maslah binafsi ya kiuchumi.

KAZI ya ubunge ni KAZI ya season, Si ajira ya kudumu, lazima uwe na KAZI Yako ,bungeni unaenda kutetea Maslahi ya wananchi, wabunge wanaodhani kuwa ubunge ni ajira ndio wanatuletea shida.

Pale Uingereza, mbunge anapanda treni ya umma kwenda bungeni, gari yake binafsi anatumia akiwa jimboni kwake na umma hawajibiki kumlipia mambo lukuki kama huku.

Mshahara na marupurupu usizidi ml 5 Kwa mwezi, na mbunge lazima awe na KAZI yake, bungeni pasifanywe ajira.

Wabunge wapande mabasi kama raia wengine waendapo Dodoma, Kodi zetu zisitumike kulipa mshahara wa dereva, mbunge akitaka gari, akopeshwe na alipe Yeye mwenyewe na ajigharamie gharama za mafuta.

Tunachagua wabunge Ili wasaidie wananchi tupate bima walau za watoto chini ya miaka mitano iliyofutwa Ili kujazia pesa za kulipa wabunge ml 18 Kwa mwezi na kulipa wake wa wastaafu.

Wabunge oneni Aibu na muwe na huruma Kwa wananchi.

FAIDA ZA KULIPA MISHAHARA YA WABUNGE CHINI YA ML 5 KWA MWEZI.

1. Itasaidia wabunge wazalendo kuingia bungeni.

2. Itapunguza wizi wa kura.

3. Itasaidia kujipunguzia Serikali Mzigo kuhudumia wabunge, Badala yake, pesa hizo zitasaidia kulipa posho walimu mashuleni Ili wafundishe Kwa Ari na morali zaidi.

Hivi wabunge jiulizeni, bodaboda, matching guys ,wakulima, wavuvi ambao Kwa mwezi hawapati hata laki 5 Kwa mwezi, wamepata wapi uwezo kuwalipeni wabunge 399 , milioni 18 Kwa mwezi?

Mkiendelea na uroho huo, tutasusia mikutano yenu na hatutowapigia kura!!

KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa, wabunge wamedhihirisha wazi kuwa hawaangalii maslah ya Wananchi maskini, wanajiangalia wao na familia zao.

Pia wabunge wazuiwe kujiongezea mshahara bila kupata ridhaa ya walipakodi.

Karibuni

Viongozi wangzkuwa wanatumia public transport , huenda miundo mbinu ingeboreshwa na wengeweza elewa shida zenu.

Kwa Africa, uongozi ni ulaji na utajiri, ni kawaida kukuta Rais mstaafu au waziri mstaafu ana Trilion kwenye Ac yake

Kwa Developed countries , Uongozi ni Accountability Ni kawaida kukuta kiongozi mkuu akiwa na normal life.

Niliwahi kusema being in Africa is a curse

Haiwezekan nchi kama Tanzania ni masikini kweli kweli but viongoz wao ni Trilionea
 
Ndugu yangu Pascal Mayalla kuna kipindi aliwahi kugombani hiyo nafasi lakini haikuwa bahati yake, leo hii ungekuta na yeye ni mmoja wa wanufaika katika hili sijui upi ungekuwa msimamo wake katika hili unalolisemea.

Kosa kubwa tunalolifanya watanzani kwa kulazimishwa na mfumo, ni kuwapa madara maskini na haya ndio maskini yanayoyasanya wakiwepo madarakani...

Mbunge ukiona anaugombania Ubunge, kwanchi maskini ujue huyo ni jobless hana source ya fund ambayo iko stable inayompa financial freedom yake kufanya mambo yake binafsi. Anafanyaje sasa, inabidi aingie kwenye siasa kuwaibia wananchi kwa kivuli chakuwatetea
Sasa matajiri shida, masikini shida, solution ni nini?

Nadhani bado mleta mada ana hoja nzuri tu. Maana mwisho wa siku, mbunge anagombea kwa kupitia chama cha siasa ambacho kina sera zake nk.

Huu uozo unaanzia kwenye chama. Wanapotaka kupitisha miswada yao hovyo na kifisadi, haijalishi mbunge ni mtu wa aina gani. Hata akiwa bubu bado anafaa kabisa.

Mwisho wa siku wananchi ndiyo waamuzi wenye kutakiwa kuwawajibisha.
 
Walipwe kwa kazi wazifanyazo siyo kuchota pesa tu bila shughuli yoyote. Mil 5 kwa kazi gani? Walipwe tu wanapofanya kazi za kibunge, vinginevyo watafute ajira au shughuli binafsi kama wananchi wengine.
 
Kama ml 5 ni kubwa, ml 18 ni kubwa kiasi Gani?

Na wananchi tukihoji, wanatwambia kuwa wanafanya hayo Kwa ridhaa yetu.

Unajiuliza, lini Mimi mkulima ambaye ninaweza kulima shamba nikatumia gharama, mvua isinyeshe nikapata HASARA, lini nimeridhia mbunge alipwe ml 18 Kwa mwezi Kutoka Kodi nilipayo?
 
Back
Top Bottom