Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
- Thread starter
- #21
Ona maneno ya Jaji Mkuu.
Athari ya pili, Mheshimiwa Spika, ni kwamba kuwa mdeni sugu kunaiondolea Mahakama heshima na hadhi yake mbele ya jamii na hasa hasa mbele ya watendaji wa mihimili mingine ya dola kama Serikali na Bunge. Napenda kumnukuu Jaji Mkuu Ramadhani tena: Kila nilipokwenda mikoani nilikwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa na kwa Mkuu wa Wilaya kutoa heshima zangu na kusaini kitabu cha wageni. Wakuu wa Mikoa wachache walitoka ofisini mwao kunilaki nje. Wengine walibakia ofisini mwao na kutuma mwakilishi kuja kunipokea ili nikamkute Mkuu wa Mkoa ofisini mwake ingawa Jaji Mkuu amefunga safari kutoka Dar es Salaam kumfuatia yeye. Kuna wakati nilikwenda Wilaya moja na nikaambiwa kuwa Mkuu wa Wilaya aliondoka jana yake kuanza likizo ya mwaka! Hivi kweli Mkuu wa Wilaya asingeweza kuahirisha likizo kwa siku moja tu kukutana na Jaji Mkuu. Ikikumbukwa kwamba Jaji Mkuu ndiye anayemuapisha Rais ili aweze kushika madaraka ya juu kabisa katika Taifa naye DC ni mwakilishi wa huyo Mhe. Rais wilayani humo. Kama Jaji Mkuu haheshimiwi kiasi hiki na Wakuu wa Mikoa na Wilaya, maamuzi ya Mahakama yake yanawezaje kuheshimiwa na watendaji hawa wa Serikali?