Tundu Lissu aunguruma Bungeni!

Ona maneno ya Jaji Mkuu.

Athari ya pili, Mheshimiwa Spika, ni kwamba kuwa mdeni sugu kunaiondolea Mahakama heshima na hadhi yake mbele ya jamii na hasa hasa mbele ya watendaji wa mihimili mingine ya dola kama Serikali na Bunge. Napenda kumnukuu Jaji Mkuu Ramadhani tena: “Kila nilipokwenda mikoani nilikwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa na kwa Mkuu wa Wilaya kutoa heshima zangu na kusaini kitabu cha wageni. Wakuu wa Mikoa wachache walitoka ofisini mwao kunilaki nje. Wengine walibakia ofisini mwao na kutuma mwakilishi kuja kunipokea ili nikamkute Mkuu wa Mkoa ofisini mwake ingawa Jaji Mkuu amefunga safari kutoka Dar es Salaam kumfuatia yeye. Kuna wakati nilikwenda Wilaya moja na nikaambiwa kuwa Mkuu wa Wilaya aliondoka jana yake kuanza likizo ya mwaka! Hivi kweli Mkuu wa Wilaya asingeweza kuahirisha likizo kwa siku moja tu kukutana na Jaji Mkuu. Ikikumbukwa kwamba Jaji Mkuu ndiye anayemuapisha Rais ili aweze kushika madaraka ya juu kabisa katika Taifa naye DC ni mwakilishi wa huyo Mhe. Rais wilayani humo.” Kama Jaji Mkuu haheshimiwi kiasi hiki na Wakuu wa Mikoa na Wilaya, maamuzi ya Mahakama yake yanawezaje kuheshimiwa na watendaji hawa wa Serikali?
 
mmmmh makubwa tena haya, naomba achomeke na lile la mheshimiwa jaji Mkuu Mstaafu Augustine kuondlewa walinzi nyumbani kwake siku moja baada ya kustaafu kama ailivyolisema yeye mwenyewe dodoma juzi...

Hilo sio kosa kwani ulinzi unawekwa kwa jaji mkuu. Hivyo aliechaguliwa baada ya yeye kustaafu ndio walinzi hao walipelekwa. yeye nafikiri hao walinzi na wafanyakazi wa ndani pamoja na msaidizi wake atapewa katika packege yake ya kila mwezi. Hivyo aajili wamasai wamlinde.
 
Waziri Kombani Kiswahili Kinampiga Chenga, niko hapa namsubiria Lisu kwa Bahati Mbaya Kombani naye anapata Channel masikioni mwangu huwa sinaga hamu ya Kumsikiliza huyu mama
 
Hilo sio kosa kwani ulinzi unawekwa kwa jaji mkuu. Hivyo aliechaguliwa baada ya yeye kustaafu ndio walinzi hao walipelekwa. yeye nafikiri hao walinzi na wafanyakazi wa ndani pamoja na msaidizi wake atapewa katika packege yake ya kila mwezi. Hivyo aajili wamasai wamlinde.

Mkuu Barubaru judge Mkuu anastahili ulinzi nyumbani kwake kwa maisha yake yote mpaka atakapokufa wala sio pale anapostaafu hilo liko kwenye package yake na wala sio aajiri walinzi awalipe kwa pesa yake
 
Vp huyo Mama ameshamalza?huku kwe2 wenye umeme wameuchuku muda huu. Tunawategemea mtu up date.
Jairo hoyeee! Aibu yako.
 
Waziri Kombani Kiswahili Kinampiga Chenga, niko hapa namsubiria Lisu kwa Bahati Mbaya Kombani naye anapata Channel masikioni mwangu huwa sinaga hamu ya Kumsikiliza huyu mama

hana confedence anaogopa maswal makal kutoka ktk wabunge c kwa posho wa Chadema, anabwabwanya maneno.
 
Jamaa kawachoma sijando taratiiiibu. Naamini hii sindano imemwingia jk na serikali yake vizuuuri. Asante sana kamanda Lissu.
 
Lissu Akaba wizara vibaya mno, kwa mliokosa kushuhudia filamu hiyo kisa umeme hii hapa nakala nzima ya hotuba yake...

 

Attachments

  • Tundu Lissu-waziri kivuli.doc
    132 KB · Views: 234
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom