Tundu Lissu ashinda Urais wa Chama cha wanasheria nchini (TLS) kwa kupata 88% ya kura

Wanafaki sana hawa jamaa. Wakati mwenyekiti wao anahangaika kuzuia Lisu asigombee walikuwa wanashangilia kila anapokamatwa na kuwekwa lupango, bila kujua kuwa matendo hayo yalikuwa yanampa promo. Watu tukawa tunajiuliza, kuna nini TLS hadi serikali inahaha na Lisu?
Leo ameshinda, wanaanza kugeuza maneno.
Unafiki mbaya sana.
Unafki upo kwenye katiba ya chama cha kijani.
 
Arusha nako jina la *Bashite* limenguruma leo kwenye mkutano wa TLS, ilikuwa pale Rais wa TLS alipomtambulisha Jaji (Mst.) *Thomas BASHITE Mihayo*.Ukumbi mzima wa AICC ulilipuka kwa kelele. Ikabidi mhe. JOHN SEKA aseme "this is the real BASHITE".
 
Kwa hiyo Mawakili wetu walishindwa kuyapinga hayo Mahakamani mpaka uchaguzi wa TLS ufanyike??..
Unaweza ukawa hata TLS umeijua Leo ... Maraisi wa TLS wa hivi karibuni wamekuwa hawana hata courage ya kufile case court kupinga uvunjifu wa sheria kama jamani...... Simaanishi lawyers hawawezi ila long time wamekosa kiongozi wa kuwaongoza....


Unawafahamu LHRC na Angeline kidjo ??? Pale kuna wabobezi wa sheria ... Kama unakumbuka enzi za kikwete walimburuza MAHAKAMANI Waziri mkuu mizengo pinda kwa ile kauli yake WAPIGWE TU...


Unajua kwanini sasa hivi wapo kimya japo kuna law breaching nyingi???



Hilo swali mpeleke mwakyembe wewe huwezi kujua
 
Leo nimegundua kuwa CCM inachaguliwa kwa wingi na mambumbumbu
1489837126859.jpg
 
..hii ni jumuiya ya wanasheria.

..kwa hiyo siyo rahisi kwa mtu wa kawaida kujua umuhimu, impact, pamoja mchango wa TLS, ktk taifa
letu.

..kwa maoni yangu anayeogopwa na Magufuli na Mwakyembe ni TUNDU LISSU na siyo TLS.

..Magufuli ameonyesha mwenendo wa kuingilia mhimili wa mahakama na kutozingatia sheria.

..sasa haitegemewi kwamba Tundu Lissu akiwa Raisi wa Law Society atakaa kimya kama watangulizi wake ikiwa Magufuli ataendeleza mtindo wake wa kuingilia mahakama, kutozingatia sheria, na kuwatisha wanasheria.
Lissu kama Lissu amewahi kukaa kimya?..Unatarajia kipi kipya mkuu...

Namuona Lissu kama zaidi ya TLS..Na TLS ina watu aina ya akina Wasonga and the likes..Hatasimama Lissu kama Lissu..

Ni wapi Magufuli ameingilia Mhimili wa Mahakama na Mahakama ikafanya kazi zake kwa utashi wa Rais?, ingekuwa Mahakama inafanya mambo kwa utashi wa Rais/Serikali sidhani kama hata huo uchaguzi wa TLS ungefanyika leo..Hao akina Wasonga & Co walifanya waliyofanya kwa kutumia haki yao ya kikatiba...Na Mahakama ikatenda haki..

Hivi unategemea TLS chini ya Lissu itaweza kumzuia Rais au serikali kufanya shughuli zake?...

Na vipi kuhusu Mswada wa sheria ya kuunda chombo mbadala wa TLS??..Hauoni kama bado serikali ina control over TLS?
 
Tuachane na hizo chokochoko....

TLS imeundwa lini?...Na imefanya nini tangu iundwe?...

Ni ipi hasa impact ya TLS...Naomba kujua..

TLS (kwa kufuata maudhui ya kuanzishwa kwake) inaweza kumzuia Rais asifanye kazi zake?, au serikali isifanye inachoona ni sahihi?...

Halafu, kuna sehemu nilisoma serikali imeshaandaa muswada wa kuifuta TLS na kuanzisha chombo kingine kitakachowasimamia wanasheria....imekaaje hii...

Naomba tu kujua Chifu....
Mkuu leo siyo siku ya maswali na majibu, leo ni chereko tu haki imeshinda udhalimu.

And note that, this is just a biggining.....
 
Back
Top Bottom