Tundu Lissu ashinda Urais wa Chama cha wanasheria nchini (TLS) kwa kupata 88% ya kura

Bavicha na Bawacha mna matatizo...mnadhani kashinda urais wa nchi?

Hicho chama ni sawa na chama cha wakulima wa Tumbaku Tanganyika....au chama cha madaktari Tanganyika. Huyo Makonda ataendelea kuwa RC mtake msitake na huu ndio ukweli kwakuwa kijana anafanya kazi vizuri na nyie mafisadi matumbo joto...

Hongera Lissu kwa kushinda sasa fanya kazi bila kuendeshwa political motives zako..
Mbn wa kwako wanaendeshwa na political motives huoni jamaa yako anazuia hata wa bunge wake kusalimiana na wenzao, usimfundishe kazi paka wewe. Figisu zooote mbn kashinda tunataraji kelele nyingi zitaanza kupigwa sasa kwa serikali yenu yenye mihemko na isiyo zingatia katiba na utawala bora. Mikataba mibovu na serikali isiyozingatia maamuzi ya bunge na kufuata bajeti.
Tunacho nitaji ni kelele tu zinatosha ili sisi wananchi tuelewe sheria na taratibu zinavyo vunjwa.
Chama cha mawakili (TLS) kumchagua wakili msomi na machachari mhe.Tundu Lissu tutarajie kufutwa na kuanzishwa chama kipya cha kutetea wanasheria Tanganyika !
 
IMG-20170318-WA0026.jpg
 
Bavicha na Bawacha mna matatizo...mnadhani kashinda urais wa nchi?

Hicho chama ni sawa na chama cha wakulima wa Tumbaku Tanganyika....au chama cha madaktari Tanganyika. Huyo Makonda ataendelea kuwa RC mtake msitake na huu ndio ukweli kwakuwa kijana anafanya kazi vizuri na nyie mafisadi matumbo joto...

Hongera Lissu kwa kushinda sasa fanya kazi bila kuendeshwa political motives zako..
.....
......kalemalimao
 
Wakili msomi Mhe.Tundu Lissu ameshinda Urais wa Chama cha wanasheria nchini (TLS) kwa kupata kura 1,411 kati ya kura 1,682 zilizopigwa, sawa na ushindi wa 84% ya kura zote. Katika mawasiliano na Lissu amedhibitisha ushindi huo na kusema kwa kifupi "Nimeshinda Urais TLS, ushindi huu uende kwa watanzania wote, na kwa wote mlioonewa ambao mpo mahabusu na magerezani"
Huuuuraaaaay!
 
Mzee tupatupa aka vuta n'kuvute hongera sana kwa kura yako kwa Lissu ukiwa kama mwakilishi toka Lumumba.
Jamani mwenye kawimbo ka dini kokote hata kama ni kaswida aweke hapa please.

Tume huru idaiwe mapema Tanzania kabla ya 2020.
 
Ni asubuhi iliyo njema kabisa ndani ya Jiji la Arusha Mjini hali ya utuvuli na amani imetawala ambapo siku ya leo mawakili wasomi wataandika historia mpya kwa kuchagua viongozi wapya wa Tanganyika Law Society (TLS )

Jana baada wagombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Tanganyika Law Society kujieleza na kuomba kura. Zoezi la kupiga litafanyika siku ya leo Jumamosi kuanzia majira ya Saa 06.00 hadi saa tatu baada ya hapo zoezi la kupiga kura kukamilika matokeo ya uchaguzi yatatangazwa rasmi.
Wagombea nafasi ya Uraisi wa TLS.
1-VICTORIA MANDARI
2-FRANCIS STOLLA
3-LAU KEGO MASHA ambaye amejitoa jana kumsapoti Tundu Lissu.
4 -GODWIN MWAPONGO
5-TUNDU LISSU
Tuwe pamoja kuwaletea yote yanayojiri kutoka ukumbini Arusha International Conference Centre (AICC)

==========

UPDATES. .

Mawakili wameshaanza kuwasili ukumbini.
Baada ya mawakili wote kuwasili ukumbini kura zitapigwa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa tatu asubuhi.

Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi wa AICC ukaguzi mkubwa sana unafanyika huwezi kuingia kama huna kitambulisho bado mawakili wanaingia kwa ajili ya zoezi la kupiga kura.
Zoezi la kupiga kura bado linaendea mawakili wanaendelea kupiga kura za kumchagua Raisi wa Tanganyika Law Society. (TLS) .
linatarajiwa kumalizika Saa 4:00 asubuhi leo.
Baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika mchakato wa kuanza kuhesabu kura unaanza.
Zoezi la kupiga kura limeshaanza kumalizika.
Kupiga kura kumemalizika sasa hivi ni zoezi na kuhesabu kura linaendelea mpaka saa nane mchana mshindi atatangazwa.
Mawakala wakiwa wamebeba kura kuzipeleka sehemu maalumu ya kuhesabu.
Uchaguzi wa TLS kwasasa umefikia hatua ya tatu ya kuhesabia kura!

Tayari mawakala wameingia ndani ya vyumba vya kuhesabia kura!

Vyumba hivi ni vinne cha kwanza ni cha uraisi, makamu wa Raisi, mhasibu na wajumbe wa baraza.

Mawakala wetu...Uraisi .Wakili msomi Kaunda na makamu wa raisi ni John Malya.

Tunategemea mpaka saa nane matokeo yatakuwa tayari!
Mawakili wamerudi ndani ya ukumbi wa Simba Hall AICC tayari kusubiria matokeo
Bado muda mfupi matokeo yatatolewa yote
Nafasi ya Makamu wa Raisi wa TLS Godwin MWAPONGO ameshinda .
Nafasi ya urais Tundu Lissu ameshinda kwa asilimia 88

PICHA Zoezi la upigaji kura TLS limeanza tangu Saa 1:00 asubuhi na linatarajiwa kumalizika Saa 4:00 asubuhi ya leo.
View attachment 482653
View attachment 482654
Mawakili wakiendelea kupiga kura za kumchagua Raisi wa Tanganyika Law Society.
View attachment 482619
View attachment 482622
View attachment 482626
Mgombea Uraisi wa Tanganyika Law Society (TLS )Mhe Tundu Antiphas Lissu akipiga kura akiwa na mke wake Wakili Alicia Lissu
View attachment 482637
View attachment 482639 View attachment 482626 .

View attachment 482750
View attachment 482751 View attachment 482752
List of Council Members.

1. Jeremiah Motebesya
2. Gida Lambaji
3. Hussein Mtembwa
4. Aisha Sinda
5. Steven Axweso
6. David Shilatu
7. Daniel Bushele.

President: Tundu Lissu.
VP; Godwin Ngwilimi.
HT; Magai
Ewe Mwenyezi Mungu Lini tutaona uchaguzi mkuu ukifanyika kwa ya Amani na uwazi kama uchaguzi huu.
 
Naskia Jecha Salum Jecha alifika usiku jijini Arusha na ndege ya kukodi!

Mi nilikuwa siifahamu kabisa TLS kabla ya Tundu Lissu, leo hii usiku wa manane naifuatilia TLS. Lissu akishinda uraisi wa TLS ajiandae kwa vita kubwa 2020, watanzania tumuweke pale juu agombee uraisi dhidi ya asiyejaribiwa. Itakuwa ni kati ya asiyeshindwa na asiyejaribiwa. Patamu hapo
Huenda alishindwa kupenya hadi kwenye chumba cha kuhesabia kura.
 
Chuki, Husda, Visasi, Vijiba vya roho, huyo mtu anaumia dunia nzima sasa hivi....
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom