Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 121,032
- 227,185
Hii ndio taarifa mpya inayozagaa mitandaoni kwa sasa.
wote mnakaribishwa
===
Mgombea wa Urais, kupitia Chama cha Upinzania CHADEMA Tundu Lissu, alivyohojiwa na Citizen Online Radio Station, kutoka Nairobi Kenyan Tundu Lissu aongea mengi kuhusu mustakabali wa Tanzania, ambae anagombania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020
Katika mahojiano hayo Waandishi wa habari Vicent Ateya na Meody Sinzore wa kipindi cha Jambo Kenya wamemuuliza masuala mbalimbali ya Kinchi na uchaguzi kwa ujumla.
Wakiuliza kuhusu suala la usalama kwa wagombea wa Upinzani Tundu Lissu amesema "Kama ambavyo nimesema mara nyingi hali ya nchi ya Tanzania sio suala lenye afya hata kidogo. Ukizungumzia sisi wa Chadema, viongozi wetu, wanachama wetu wameuawa katika mazingira ambayo hakuna uchunguzi wa Polisi hakuna chochote kilichofanyika."
"Kuna watu wetu wametekwa nyara miaka zaidi ya miwili mwandishi wa habari Azory Gwanda alichukuliwa nyumbani kwake na hajilikani alipo". Ben Saanane hajulikani alipo tangu Novemba 2016. Watu wameumizwa sana. Mimi nimeponea chupuchupu nimepigwa risasi 16. Mwenyekiti wangu amevunjwa mguu kama mwezi mmoja na ushehe uliopita, hali imekuwa mbaya kwelikweli.
Kwahiyo tunapozungumza kuwa Tanzania ina hali mbaya tuna maana hiyo. Hali ya haki z binadamu imeporomoka sana. Sio sisi tu tunaolalamika bali hata mashirika ya haki za binadamu ya nchini na kimataifa yanasema hivyo hivyo.
Sasa tunakwenda katika uchaguzi Mkuu ambao utakuwa ni wa kihistoria. Rais Magufuli na Chama chake wamesemahadharani bungeni kwamba wakishinda watabadilisha katiba kuondoa ukomo wa madaraka. Maana yake ni kwamba tutakuwa na Rais wa Maisha. Sasa sisi ambao Mwalim Nyerere alisema hatuwezi kuwa na Rais wa Maisha kama ilivyokuwa kwa kiongozi wa Malawi Kamuzu Banda, atuwezi tukakubali kurudi kwenye utawala wa aina hiyo.
Rais Magufuli mwenyewe alitangaza tarehe Febuali 6,2016 kwamba anataka kuangamiza vyama vya upinzani ifikiapo mwaka 2020. Sisi hatutokubali kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Uchaguzi huu utaamua mambo mengi sana katika nchi yetu na tunaamini kwamba watanzania hawatamkubalia Magufuli na ajenda yake na Chama chake ya kuturudisha katika miaka ya giza ya utawala wa chama kimoja.
Aidha, wakimhoji jitihada za Tanzania katika kukabili Covid 19 Lissu ameeleza kuwa Majirani zetu wote wana Corona, Tanzania ukitangaza kuwa kuna Corona ni kosa la jinai. Katika hili Lissu amesema "Sasa serikali inayoamini kwamba hakuna Corona na inawatangazia watu hakuna Corona haijatoa taarifa yoyote ya maambukizi, ya waliofariki, ya waliopona tangu tarehe 29 mwezi wa nne mwaka huu, wanaamini kwamba tukinyamaza basi Corona itapotea. Tusiposema chochote kuhusu Corona maana yake Corona hamna. Huo ndio msimamo wa serikali yetu.
Mwisho, Tundu Lissu amewashukuru Redio hiyo ya Kenya kwa kumhoji na kuweka bayana kuwa tangu amefika nchini mpaka leo hakuna kituo chochote cha habari kilichomwita na kumhoji kwa sababu viombo hivyo vinaogopa kuzuiliwa.