Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Wewe wala english hujui wala uwezo wa kumwelewa stephen suckur wa hard
tallk huna. Ungelewa ulivyo nyumbu ungelia.
Watu kama kina Tony Blair walitaka kukimbia mule ndani kwenye HARDTALK...sio pa kawaida sana mule..Unaweza ukaishia kuaibika bure ndani mule ukijua unaenda kutafuta popularity....

Maswali yao mara nyingi yanakuwa na majibu...kwa hiyo unapigwa swali ambalo ni Open ended ukishindwa anakushindilia kisha anakuambia wewe ni mwanasiaa au ...??

Yanahitaji Logic sana kuyadefend..

Huyo Stephen Sackur sio mtu wa mchezo mchezo ,hakwenda Havard kuuza sura...kapikwa akaiva...

Kwanza wengi wakipangwa nae HARDTALK wanadiverge wantamani bora wahojiwe na Zeinab Badawi au
Sarah Montague pamoja na
Shaun Ley lakini Nahisi uulizaji wa maswali wa Stephen Sackur unataka kufanana na ule wa Tim Sebastian ambao ni most interested na difficult kuhandle kwa baadhi ya wanasiasa....

But all in all Tundulisu Kajitahidi sana...Ana deserve kuwa hivyo alivyo...



Sent using Nokia 8 Plus
 
Pumba tupu hata ukumsikiliza vizuri unafkiri lissu ni Kama wale makasuku wa ndiyo kajibu kwa kusema kwa mujibu wa sheria ya Tanzania.siku nyingine hizi habari anza kwanza kusimuliana na watoto wako ndo ulete humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasifu politicians wako vizuri kwenye kudhibiti hisia ili kudumisha mawasiliano ya ubongo,masikio na mdomo pale wanapohojiwa na kujibu.
Ningekuwa Mimi ndio Lissu,huyu mzungu tungeishia swali la tatu tu,hayo ya ushoga tusingefika..na Kama angeanza nayo ningemwambia acha ungese,mss!
Hili swali ni gumu kwa mtz yeyote yule akisimama ktk capacity ya Lissu.Hata Mahiga ukimpeleka pale itakuwa shida kulijibu.Moyoni msimamo unaujua ila ukiuzungumza unaweza kuisababishia nchi yako matatizo makubwa.Lissu akaamua kutorokea uchochoro wa Privacy rights kwenye Katiba..na msimamo wa serikali uliotolewa na Mahiga juu ya ushoga!Tena mzungu alivyo kauzu anamwambia "Dunia yote inakutazama hapa bwana mkubwa,unatuambiaje?"😀😀
 
Dah! Kwenye ushoga wazungu wameshambaatiza nini huko ulaya?
Nalog off
 
Nimependa huyo Sacker anavyouliza maswali, I wish waandishi wetu wajifunze kwake, though lile swali la ushoga ni mtego na linaweza kuwa shimo kwa Tundu Lisu incase akawa candidate wa opposition.

Tamaduni zetu si tu haziruhusu tendo la ushoga lakini hata kulitamka tu ni kufuru. Lakini Lisu anasema hizo ni private issues wacha watu wale bata.
 
Kada wa CCM Bollen Ngetti anatoa rai yake.

DAWA YA TUNDU LISSU HII HAPA

Na Bollen Ngetti

YULE Afisa Usalama wa TISS alimwambia Zitto, "dawa yako ni kukuua". Hii maana yake ni kwamba mbinu zote zimefeli na njia sasa inayoonekana muafaka ni kumuua Zitto.

Inawezekana waliopanga na kuratibu mabunduki kwa Lissu nao waliona hakuna namna isipokuwa ni kumuua Lissu jaribio lililoshindwa licha kutumia risasi nyingi. Sitoshangaa kama kundi hilo la watu waovu linapanga Plan C maana kuua kulifeli, kuporwa Ubunge nao umeshindwa. Je, Tundu Lissu ameshindikana? Lakini pia tujiulize kosa hasa la Lissu ni lipi? Kukosoa Serikali? Kuna tofauti gani Kati ya Lissu na Jamal Kashoggy wa Saudia?

Nimefuatilia mahojiano ya Lissu kipindi cha "Hard Talk" cha BBC. Lissu amejitahidi sana kujibu maswali magumu ya BBC. Alichonivutia Lissu ni kwamba alikwepa kuongea uongo. Alisimamia ukweli wa alichofanyiwa na hali halisi ya siasa za Tanzania.

Dawa ya kutibu ugonjwa ws "Lissu" si kuweweseka, si kutapatapa, si kutukanana mitandaoni. Tunakosea sana wana CCM wenzangu. Lissu ajibiwe kwa hoja si vihoja. Mbona ni utamaduni wetu kujibu hoja? Wako wapi kina Nape, Mwigulu nakadhalika kumjibu Lissu?

Lakini pia tuelewe kuwa kutokana na kunusurika kifo, imemwongezea Lissu umaarufu mkubwa wa kisiasa maana sasa anabebwa na "global sympathy" (huruma ya dunia). Hii ni hatari sana. Kama kura ingepigwa Leo ya Urais Kati ya Lissu na Magufuli kuna uwezekano Lissu angepata kura nyingi za huruma kutoka kwa kina mama ni vijana chini ya miaka 35. Kura za huruma huwa ni hatari sana maana watu hawatoangalia mema yote uliyowatendea Bali wataangalia huruma.

Uwezekano wa Lissu kugombea Urais 2020 ni mkubwa na kadri tunavyoweweseka ndivyo tunavyozidi kumpaisha. Ninachoshauri CCM tuwe makini kumpata a very strong candidate kuweza kumvaa Lissu ili tuvuke salama. Tujiulize kwa tutakayemsimamisha je, atatuvusha salama au itabidi kutumia "bao la mkono?" Na je, "bao la mkono" litakuwa na nafasi tena katika mwanga huu ambapo dunia nzima macho yako Tanzania? Baraza la Wazee mtusaidie. Vyombo vya dola muwe "fair" kutenda haki na demokrasia. Ni vizuri JPM ashauriwe kugombea tena maana hajatangaza kufanya hivyo. Na endapo atakataa basi mgombea anayeweza kumuangusha Lissu 2020. Hiyo pekee ndio dawa ya Lissu na si kuweweseka na wito wa kumtaka arudi nyumbani. So what?

Sote tunajua mwezi wa tatu EU na USA watakata uhusiano wa kifedha na nchi yetu kwa mujibu wa taarifa zao. Sasa vijana wa Lumumba tusianze kujipanga kumhusisha Lissu na hili, hapana. Ni sisi wenyewe tumeshindwa kujenga mahusiano mazuri na mataifa haya katika kuheshimu utawala bora na haki za binadamu. Tujiandae kisaikolojia kabla ya kufikiria "kuchapa noti hewa" kuokoa jahazi. Tujibu hoja za Lissu maana zinajibika. Msemaji wa Serikali ajitokeze kumjibu Lissu na si propaganda! Paul Makonda si size ya Lissu maana si mwanasiasa huyu. Hoja za Lissu ni za kisiasa!
#AchaWoga2020
 
Since Mkapa, 2001, sijasikia Mtanzania mwengine akihojiwa kwenye Hardtalk.

Kwa ujumla Lissu yuko vizuri sana. Hakumpa nafasi jamaa ... ndiyo maana akawa free kuongea na kujibu maswali kwa jinsi alivyotaka yeye. The message was cleared sent!! Unlike Lissu, Mkapa aliwekwa kwenye kona mpaka akaadmit mwenyewe kuwa amekasirika ...!!

Tukubali tukatae, LISSU NAILED IT ....................!!
 
Nimependa huyo Sacker anavyouliza maswali, I wish waandishi wetu wajifunze kwake, though lile swali la ushoga ni mtego na linaweza kuwa shimo kwa Tundu Lisu incase akawa candidate wa opposition.

Tamaduni zetu si tu haziruhusu tendo la ushoga lakini hata kulitamka tu ni kufuru. Lakini Lisu anasema hizo ni private issues wacha watu wale bata.
Mwaka wake wa mwisho huu kusikika bwana LISSU 2020
Kuna yule form 6 lever
Kuna mamvi
Kuna Sumaye
Kuna Zitto Zitto kupitia muungano wa vyama
Kuna LISSU
Wote hawa wanataka 2020 kujaribu kete yao...hakika mtakuwa mashahidi hapa **** kutakuwa na kiongoz atayekumbuka kuwa LISSU alipigwa risasi hakika yajayo yanatisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom