Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Kuna ratiba ndefu sana ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania 2015-2021... Kwa ujumla wake ataagwa mara sita maeneo tofauti ya nchi ikiwemo Zanzibar iliyokuja kuchomekwa baadae kwa sababu za kisiasa
Msiba ni gharama kwa kila hatua na ni gharama zaidi kwa kila siku inayoongezeka kila siku ipitiyo bila kuzika...lakini zaidi kiimani ama kiroho si vema kuuhangaisha mwili uliokwisha tengana na roho labda tu iwe kwa maagizo ya mhusika
Safari ya kifo ni ndefu isiyo na kinyume ndio maana wafu hutolewa eneo alilofia, mochwari, nyumbani kisha kaburini... Ni safari ya njia moja... Ni kinyume cha mazoea kuutoa mwili mochwari na kuuanika siku nzima kisha kuurudisha mochwari tena na kuutoa tena na tena...

Watetezi wa hili wana hoja zao kama hizi
Dar kuaga ni mara mbili kutokana na wingi wa wakazi wake
Dodoma ni mji mkuu wa nchi alioupigania katika maisha yake hivyo si vizuri kuwaruka watu wa Dodoma
Mwanza ndio mkoa wa mji alikokulia
Geita na baadae Chato ndio nyumbani
Vipi kuhusu Zanzibar? Ni sehemu ya muungano , japo leo tayari kulikuwa na wawakilishi waliokuja kwa gharama za serikali
Kwa sasa ni matumizi , bajeti wanaijua wachache lakini huko mbeleni huu msiba unaweza kuja kuwa kashfa ya ufisadi
Kwa kila siku ya huu msiba kuna pesa inateketea
Per diem za viwango tofauti
Mafuta ya magari yanayohusika kwenye msiba
Malazi, chakula na vinywaji kwa waalikwa, wahudhuriaji, waombolezaji na wageni mbalimbali
Gharama za majukwaa mbalimbali, viti meza nk
Washereheshaji na watumbuizaji
Gharama za kuhifadhi mwili
Dharura nknk

Tunaweza kufanya mambo bila kujua mtazamo wake lakini isifike mahali tukakufuru kwa kuona kwamba hivi ndivyo inavyopaswa kuwa na zaidi kumbe kuna wapiga dili nyuma yake.

Hali ngumu ya maisha inawafanya baadhi kutumia misiba kama sehemu ya kujazia mashimo yao ya madeni, matumizi na mahitaji mbalimbali

Naweza kupigwa mawe kwenye hii post na wanufaikaji lakini huu... Wale wataosema msiba unabebwa na rambirambi za wapendwa wake. Na bajeti ya kitengo kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi..lakini kuagwa mara sita sehemu tofauti za nchi kunaweza kuweka rekodi mpya.

Mi nadhani hawawezi kumsumbua namna hii. Hamna kitu ndani ya sanduku. Ile picha kubwa inamwakilisha
 
ingekuwa wafu wanaweza kuongea marehemu kwa kaliba yake angeweza kusema inatosha nipumzisheni afu bajeti inayobaki ya kunizungusha mimi ielekezeni kwenye ununuzi wa chanjo ya corona
Nani amekwambia tunahitaji chanjo ?
Fateni chanjo nyie wakala wa shetani.

Sisi tumegoma waambieni na mabwana zenu kuwa hiyo chanjo pelekea nguruwe.
 
Yaani kwa tanzania gene za marehemu kuisha itachukua mda mrefu sana naona mwendo ni uleule,asa nikiangalia ratiba inaniacha hoi
 
Kusema kweli hii kitu ni pointless kabisa. Uongozi uliobaki wamedhihirisha kuwa nao bado ni malimbukeni tu.

Haiwezekani kufanya mikusanyiko mikubwa namna hiyo bila kujali uhalisia wa janga covid-19.

Watu tungeangalia shughuli kupitia kwenye TV na kusikiliza kwenye radio ingetosha. Hakukuwa na haja ya haya yote. Kwanza ni gharama kubwa tu zinatumika na zinaongeza mzigo kwenye kodi za wanaoitwa wanyonge.

Mimi kwangu haileti tofauti kuwa ameagwa na watu wengi au hajaagwa kabisa. Mtu akishakufa amekufa tu hata akiagwa na dunia nzima haimsaidii chochote.

Wangempumzisha tu tuendelee na maisha.

NB: In the end, all the people you know including you will die.
Hawa watu wana ajenda ya kishetani kuua as many as possible, labda ni kafara wametumwa kuzimu
 
Bro punguza ujuaji, unapenda sana umaarufu.unajiona unajua kila kitu..

Unajiona wewe ndio una fikra pevu humu..

Uwe na kiasi...

Sent using Jamii Forums mobile app
huyu ndio alivyo tumwache tu.

lakink tukubali,hawa mawakala wa ibilisi ndio walikuwa wakiomba mzee wetu afariki.

baada ya kuona amefariki na kuumiza hisia za kundi kubwa la watu,roho zao zinawasuta.wanachotamani kitokee azikwe asahaulike wapumue.
 
Anayoyaandika angeyaongea mtaani sidhani kama angekuwa anapumua muda huu, hizi simu zinasaidia sana sometimes..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom