samurai
JF-Expert Member
- Oct 16, 2010
- 11,495
- 24,174
Nchi ilishafanya makosa mengi. Na marekebisho mengine lazima yatapnekana ya kipuuzi kwa wapuuzi. Na yatakuwa na maumivu au gharama. Hata Mh Rais amesema hilo wazi. Kuwa lazima watu wengine (wachache) waumie.
Sasa katika kutafakari hili, ni kujiuliza, mwekezaji tunamhitaji kwa ajili ya nini? Pato la taifa. Pato la taifa kwa ajili ya nini? Kuwaletea watu huduma za kimaendeleo. Huduma hizi ni wazi maji safi na salama na huduma za afya ni vipaumbele. Maji ni uhai. Sasa, kama kitaalam (kama alivyojibu mhandisi wa maji alipoulizwa) akasema kila kitu kiko sawa isipokuwa tu mahali pa kuweka tank la maji kuna mwekezaji!!! Hivi kuna mtu anaelewa adha ya maji kwa baadhi ya maeneo ya nchi hii?? Kuna watu wananyang'anyana maji na mifugo kwenye madimbwi!!! Sasa what is the point ya kuwa na mwekezaji anaingiza pato la taifa kisha watu walioeneo alilipo yeye ndio kikwako kwamba hawapati maji wanataabika na kufa na magonjwa?? Hata kama ni mimi ningefanya alichoamua Mh Rais. Si lazima tubembeleze mwekezaji. Tusitafute huruma. Aondoke, kama kuna gharama zilipwe tu kama kuzilipa watu watapata maji. Tumeshalipishwa mambo mangapi kila siku umeme nchi inalipa 452Mil? Aondoke!! Mwalimu alisema madinu hayaozi.
Nimetumia uhuru wangu kujieleza. Tafadhali niambie ikiwa maji hayapatikani mpaka tu tank liwekwe hapo kwa mwekezaji, wewe ungeshauri nini? Don't take lightly watu wanataabika hili suala la maji ndugu!
Kama ni makosa ni process nzima ya mpaka kuruhusu awekeze hapo, jambo la juzi wakati shida ya maji ina miaka na miaka!
PRIORITY.
Hivi kitaalamu kweli lazima tank la maji likae hapo, hakuna alternative nyingine ya kuweka tank mpaka hapo?? tujadili kiupana zaidi, wataalamu mwisho wao ulikuwa hapo lazima tank likae hapo??,, siamini kama hapo mahala au hilo eneo halina mahala pengine pa kuweka tank ila ni hapo tu siamini kabisa...wataalam wafanye kazi yao na mh ashauriwe vizuri..
Unaweza ukala hasara ya kujitakia na hii ni hasara ya kujitakia kwa kutofanya mambo yetu kitaalamu baadala yake tunarahisisha...