General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,055
WIKI iliyopita, mwanahabari nguli nchini na kimataifa, Tido Mhando, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media inayomiliki televisheni ya Azam na Radio Azam, alifanya mahojiano katika Ikulu ya Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa. Mahojiano hayo yaliyokwisharushwa katika kipindi cha FUNGUKA kwenye televisheni ya Azam, tunayarejea kwa kuyachapisha hapa kwa faida ya wasomaji wa gazeti hili la Raia Mwema kwa hisani ya uongozi wa televisheni ya Azam – Mhariri Mkuu
…………………………………
Tido Mhando: Januari 12, 1964 ni siku ambayo wananchi wa Zanzibar kupitia Mapinduzi walijiona wamekuwa huru, na kwa hiyo walikuwa na matarajio ya juu sana kuhusu nchi yao. Matarajio haya yametimia?
Dk. Shein: Matarajio yametimia. Watu wa Zanzibar walikuwa wametawaliwa kwa muda mrefu na katika historia, walitawaliwa na madola mawili. Zanzibar ilitawaliwa kwa mara ya kwanza na Wareno mwaka 1553 wakatawala kwa zaidi ya karne mbili na kidogo, baadaye Wareno wakatolewa na Waarabu wa Oman nao wakatawala na katika utawala huo wa Sultan Said bin Taimur wa Oman ambaye alitawala rasmi Zanzibar, tena akiongoza Oman kutokea Zanzibar. Kwa hiyo, Mwingereza baadaye kama vile alikuwa amempa nguvu ya kutawala, kwa hiyo furaha ya watu wa Zanzibar kufanya Mapinduzi ilikuwa kujikomboa na kuikomboa nchi yao.
Tido: Kweli hali za wananchi zimebadilika kiasi cha kujivunia kuongoza wenyewe nchi yao tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya Mapinduzi?
Dk. Shein: Ni dhahiri wanajivunia kwa sababu watu wa Zanzibar awali walibaguliwa sana na tawala zote mbili, hususan utawala wa mwisho. Wananchi wa Zanzibar hawakuwa wakipewa elimu, haikuwa rahisi kwao kusoma, hawakuwa na haki ya kumiliki ardhi na hawakupata fursa sawa ya kupata huduma za afya.
Tido: Kikubwa ni kwamba hadi leo wanapozungumzia maendeleo bado taswira ya mzee Abeid Aman Karume inaonekana, ndiye kiongozi aliyefanya mambo makubwa. Wewe ni rais wa saba, lakini Karume aliacha alama kubwa ambazo bado zinafunika juhudi zenu ninyi marais mliofuatia. Kasi ile ya Karume katika maendelo kama nyumba za Michenzani bado watu wanaizungumzia.
Dk. Shein: Ndio ni sahihi. Karume alifanya kazi ya kuikomboa Zanzibar pamoja na wenzake. Haikuwa kazi rahisi, unajua upo kwenye nchi ambayo ilikuwa imebanwa sana, Karume na wenzake wakaanzisha Chama cha Africa Association baadaye kikaungana na Shirazi Party, juhudi zote hizo haikuwa kazi rahisi. Kwa hiyo, hakuna aliyevuma zaidi yake.
Tido: Mzee Abeid Karume alifanya Mapinduzi na akaingia madarakani, hotuba zake bado zinasisimua zaidi hadi leo. Huoni bado ana nguvu za kisiasa licha ya awamu zenu za utawala kupita baada yake?
Dk. Shein: Hapana, wa kwanza ni wa kwanza, yeye ndiye mwasisi na baba wa taifa hili. Sasa mtu akiasisi kitu lazima aendelee kukumbukwa na tuna mifano ya nchi kadhaa kama Ghana kuna Kwame Nkrumah, Nigeria na nchi za Afrika na hata Ulaya wale wote waliofanya kazi kubwa ya kukomboa nchi zao hata kama hawapo ile jitihada yao, heshima yao ndio wananchi wanaikumbuka na kuienzi. Hatokei Karume mwingine … kunaweza kuwa na watoto na ndugu wengine, lakini yale aliyofanya ni yake, kama Mwalimu Julius Nyerere, hawezi kutokea Nyerere wa pili, mwasisi ni mwasisi, anayeanzisha jambo huungwa mkono hadi leo, sio kwamba sisi wengine hatujafanya kitu ni kwamba sisi sote tunajivunia misingi aliyotuwekea, tunafuata nyayo zake. Tunafuata ile misingi iliyowekwa, misingi ya nchi haiwekwi na kila mtu bali waasisi.
Tido: Miaka 53 sasa Serikali ya Mapinduzi bado inaendelea kuadhimisha Mapinduzi katika hali ambayo ni kama bado kuna wasiwasi, na hivyo ni lazima kuendelea kuyalinda.
Dk. Shein: Mapinduzi ni alama ya Zanzibar. Ni sifa, ndio uhuru wetu. Unajua hapa Zanzibar baada ya mapambano ya uhuru na demokrasia hatimaye Hizbu walishinda uchaguzi na Uingereza iliwapa serikali, na sisi tunasema ule si uhuru wa Zanzibar, ni hila tu. Uhuru wa 1963 Desemba 10, ni hila. Huwezi ukachukua nchi ukamkabidhi nchi mtu ambaye naye si nchi yake, kwa sababu Waingereza walikabidhi nchi kwa Sultan ambaye hii si nchi yake, kwa hiyo kilichofanywa na Afro Shiraz ni kuikomboa nchi, ni kuirudisha Zanzibar kwa Wazanzibari.
Sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni alama yetu, si ile ya 1963 na bendera yetu si ile ya mwaka huo, kwa hiyo, tafsiri yake ni kwamba Mapinduzi ni ishara yetu ya uhuru, si kwamba Mapinduzi eti tunapindua maisha, hapana, maana yake ni kujitawala wenyewe kwenye nchi yetu tukiwa huru, mabadiliko haya ya hali za maisha yataendelea kuwapo.
Tido: Wewe ni rais wa saba. Tuzungumzie juhudi zako za maendeleo ambazo unadhani zitadumu kama alama yako kwa Wazanzibari.
Dk. Shein: Mimi siye nitakayepima kiwango cha maendeleo ninayofanya, watakaopima kipindi changu cha uongozi ni wananchi. Nimeingia serikalini kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndicho ninachofanya. Kwa hiyo, ninachofanya mimi na walichofanya wenzangu wote hadi awmau ya sita, na hata mzee Abeid Karume aliingia na ilani ya chama kwa hiyo kila kiongozi anaingia na ilani ya uchaguzi ya chama chake, chama ndicho kinachotafuta serikali na kisha kinakabidhi ilani kwa serikali ili itekelezwe, sasa kuna mengi makubwa nimefanya, yapo madogo na kuna mengine hayajakamilika. Sitaki kujisifu, nenda kahoji wananchi utasikia kila mmoja akiwa madarakani kafanya yake. Mimi nimefanya na naendelea kufanya mengi, yapo.
Tido: Tuangalie baadhi ya mambo mawili au matatu ambayo ni alama ya mafanikio yako
Dk. Shein: Sifa kubwa ya utawala wa marehemu mzee Abeid Karume ilikuwa elimu bure, kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu walipata ufadhili bure. Baadaye uwezo wa serikali ulikuwa mdogo, wananchi wakaanza kuchangia si kulipia bali kuchangia kwa sababu ndiyo inalipa gharama kubwa hadi mishahara ya walimu. Kwa hiyo mimi wakati wangu nimerejesha elimu bure kama 1964 wakati wa mzee Karume. Nilitangaza wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi kwamba hakuna kulipa elimu ya msingi, sekondari nikasema serikali itagharimia mitihani, imebaki ada ndogo ambayo nayo haina muda nitaiondoa. Kwa hiyo elimu bure, matibabu bure.
Tido: Kuna elimu bure na elimu bora. Ni kweli watoto wanakwenda shule, shule zinajaa wanafunzi. Lakini matokeo ya mitihani yanaonesha shule za Zanzibar hazifanyi vizuri sana. Hili la elimu bora unalizungumziaje?
Dk. Shein: Nakubaliana nawe kwa njia moja lakini sikubaliani pia kwa njia nyingine. Vyombo vya habari navyo vinatia chumvi katika kufanya tathmini ya elimu. Ni kweli ni kwamba vijana wa kidato cha sita hawakufanya vizuri sana lakini waliopata daraja la kwanza mwaka huu ni kubwa zaidi kuliko mwaka mwingine wowote, wenzetu wa habari hawaoni, lakini division ya kwanza zilikuwa nyingi zaidi ya 50, second division hadi 100 na waliopata division zero ni wachache, sasa ukichambua matokeo si mabaya.
Tunachopigania sasa ni ubora kwa hiyo nakubali juhudi zinahitajika zaidi kuna maeneo kuna upungufu wa walimu, tunaendelea kujitahidi tukielewa kuwa uwezo wa uchumi wa Zanzibar unategemea utalii na karafuu, sasa ili ufanye vizuri lazima uwe na nguvu za uchumi zaidi, lakini hatujafanya vibaya sana, Zanzibar sasa ina vyuo vikuu vitatu, awali hapakuwa na chuo chochote kikuu mimi mwenyewe na wengine tumesoma vyuo nje ya Zanzibar, leo madaktari wanafundishwa hapa, Zanzibar tuna wasomi wengi hadi tuna shahada ya uzamili na wengine hawajapata ajira serikalini.
Sekta ya afya ni kama elimu, nako kuna mafanikio, marehemu mzee Abeid Karume alitangaza huduma za afya zitolewe bure, kwa nini? Kwa sababu wakati wa ukoloni ukienda hospitalini kulikuwa na ubaguzi, tiba ilikuwa inatolewa kwa madaraja A, B na C. Kundi A ni Waingereza wenyewe, B ni wale wa serikalini, kundi C wale wa kawaida. Kundi la chini ndio kina sisi wanyonge. Leo, baada ya mzee Karume kutangaza, watu wote sawa, hakuna malipo bila kujali mkubwa wala mdogo hali ni nzuri. Mapinduzi yalipofanyika Zanzibar kulikuwa na vituo visivyozidi 36 vya afya leo kuna vituo karibu 154, hospitali zilizopo ni mara tatu ya wakati ule.
Tido: Bado panapotokea masuala mazito ya maradhi watu wa Zanzibar hukimbilia Tanzania Bara kuonyesha labda kule wanaweza kupata huduma bora za afya kuliko hapa.
Dk. Shein: Hata Bara wanakwenda nchi nyingine kama Kenya au India. Viongozi wengi wanakwenda nje ya nchi kwa hiyo watu wa Zanzibar kutoka hapa kwenda kwingine si jambo la ajabu, si kwamba hapa hakuna huduma, hapana, dunia nzima iko hivyo, aliyeko London pale Uingereza anataka kwenye Manchester au wa Manchester anakwenda Cadiff, ndiyo dunia ilivyo. Kinachotokea ni mwanadamu kuwa na hali ya kujaribu, hata waganga wa kienyeji utasikia watu wanashauriana hapa hapafai nenda kwa mzee Kombo lakini hicho si kipimo. Ni kweli kuna maeneo bado hayajawa sawa kwa mfano katika upasuaji hatuna madaktari wa kutosha, tunafundisha na hata katika eneo la uchunguzi wa maradhi bado, upande wa maradhi ya kina mama kuna nafuu lakini maeneo mengine ya maalumu (specialization) hatujafikia kiwango cha juu.
Tido: katika suala la utalii, wengi wanahisi bado Zanzibar haipati mapato inayostahili, watalii wamekuwa wakifanya malipo huko huko kupitia kwa mawakala. Unazungumziaje hili?
Dk. Shein: Ni kweli wananchi wanadodosa, matatizo yalikuwa makubwa zaidi ya haya, sasa hivi hayako hivyo. Mwanzo ilikuwa ghamara zote na shughuli nyingine zinaandaliwa kwa mfano Milano – Italia, kila kitu kinabakia (pesa) huko mtalii akiwa hapa hatumii sana anakuwa amelipa gharama za matumizi kwa wakala lakini sasa serikali ina sera mpya ambayo iko wazi sana, kuna utalii wa watu kuja kutumia fedha, watalii wa daraja la juu na hoteli zenye sifa sasa zipo nyingi. Kuna hoteli ya nyota tano, nyota nne, nyota tatu pia nyingi tu, sekta ya utalii imebadilika na sheria ya kuanzisha kamisheni ya utalii imebadilika, lakini bado tunaendelea kushughulikia kasoro nyingine kikamilifu.
Tido: Juzi hapa umeweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa hoteli ya mfanyabiashara mzee Bakhersa. Hali hii ya kuinua wawekezaji wa ndani nchini unaiangalia kwa jicho gani?
Dk. Shein: Wawekezaji wa nchini lazima tuwashirikishe na tunaamini katika serikalini ile dhana ya PPP (Public Private Partneship) yaani umoja wa sekta binafsi na sekta ya jamii, kwa hiyo mtazamo wangu ni kwamba tumepata kasi kubwa sana ya ushirikiano kwa sababu wenzetu sekta binafsi wametuelewa, tumeanza na bwana Bakhresa na wengine, nasema si wawekezaji wa ndani tu hata wa kutoka nje wamekuja.
Tido: Tatizo au wasiwasi mkubwa katika uwekezaji ni ile hali ya urasimu serikalini inayokatisha tamaa.
Dk. Shein: Unayosema ni kweli, kuna urasimu lakini hiyo ni kwa sababu ya mazoea. Unajua moja kati ya maelekezo yangu kwa wafanyakazi serikalini ni kutofanya kazi kwa mazoea, ukifanya kazi kwa mazoea utapata matatizo na huu mtindo wa urasimu … jambo la kukamilika leo linachukua mwezi au mwaka ni tabia ambayo si ya maendeleo na wakati mwingine watendaji walifikia mahala kama wamekata tamaa, lakini tunakabiliana na hali hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Tido: Uchaguzi umepita. Lakini uchaguzi uliopita (mwaka 2015) ulikuwa na mambo mengi hadi kufutwa na kurejewa upya (2016). Je uamuzi wa kurejea uchaguzi yalikuwa ni mashauriano kati ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar na serikali yako au ni uamuzi wa tume pekee?
Dk. Shein: Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri (NEC) ni tume mbili zisizoingiliwa katika kazi zake, kuna sheria ya uchaguzi ya Zanzibar kwa hiyo uamuzi wa tume ya uchaguzi ni wa tume yenyewe, mwenyekiti na makamishna wake, serikali inahusika kugharimia uchaguzi tu.
Tido: Umegusia vizuri kuhusu ZEC na NEC, lakini kinachoshangaza ni kwamba watu wale wale waliopiga kura upande mmoja hazikuharibika ni hao hao katika upande mwingine zimeharibika hadi uchaguzi kufutwa.
Dk. Shein: Kwa sababu ni mambo mawili tofauti, uchaguzi wa Zanzibar unaongozwa na Sheria ya Uchaguzi Zanzibar na inayohusika ni ZEC, ule wa jumla wa Jamhuri inayohusika ni NEC…. ni mambo mawili tofauti.
Tido: Kwa nini kurupushani zilihusu tu uchaguzi wa Zanzibar na si upande mwingine?
Dk. Shein: Hapana, pale kuna wasimamizi wa ZEC na NEC, sasa ZEC hawakuridhika na sababu zao zilikuwa karibu tisa walizozitoa, hawakuridhiha na wakaamua kufuta uchaguzi, na waangalizi wote wa vyama walikuwamo katika mchakato wa uchaguzi pamoja na wasimamizi wa tume. ZEC wakatoa uamuzi, na NEC wakatoa wakiwa uamuzi wao kwamba kwa upande wao wameridhika.
Tido: Lakini ZEC inatumika kama wakala wa NEC wakati mwingine
Dk. Shein: Hapana walikuwapo ZEC na NEC, ule wa uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano unasimamiwa na NEC yenyewe, kama sasa kuna uchaguzi wa Jimbo la Dimani hapa Zanzibar, NEC na ZEC wapo.
Tido: Nini kilikwamisha maridhiano kati yako na Maalim Seif Shariff Hamadi baada ya uchaguzi wa awali kufutwa?
Dk. Shein: Hayo ungemuuliza Seif maana yeye alikuja huko Dar es Salaam akazungumza na waandishi wa habari kuhusu mazungumzo hayo. Ungemuuliza yeye. Lakini ni kweli mazungumzo tulifanya kwa moyo mkunjufu, yeye alikuwa hataki kurudia uchaguzi, mimi nikamwambia turudie kwa kuwa uchaguzi unaongozwa na tume ambayo imefuta matokeo, mimi nikasema tume ikiamua uchaguzi urudiwe tutarudia, hayo ndio yalifanya tukatofautiana.
Tido: Kuna watu mliwaleta kuwapatanisha?
Dk. Shein: Hapakuwa na watu wa kutupatisha, mimi ndiye nilikuwa mwenyekiti wa yale mazungumzo, Seif wa pili, walikuwapo marais wastaafu, Aman Abeid Karume, Dk. Salmin Amour, mzee Ali Hassan Mwinyi na Balozi Seif Iddi, tukazungumza.
Tido: Mbona ulikuwa mkusanyiko wa watu fulani dhidi ya mtu mmoja (Seif)?
Dk. Shein: Hapakuwa na uonevu wala upendeleo. Tulizungumza na sitaki kuyasema tuliyozungumza, ninachosema mimi uamuzi wa msingi wa ZEC ulikuwa ni kurudia uchaguzi jambo ambalo tume ile ina mamlaka nalo.
Tido: Unadhani kutokana na masuala haya kuna dosari ya kidemokrasia hadi uchaguzi wa Zanzibar ukarudiwa? Kulikuwa na hila?
Dk. Shein: Uchaguzi wa Zanzibar tangu ule wa 1957 matokeo yalikuwa katika mvutano hivyo hivyo, mnazozana …. mmoja anakubali mwingine hakubali, lakini kwa mwaka 2015 ZEC iliamua kwa kuweka sababu zake kwamba mambo hayakwenda sawa, uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi.
Tido: Maalim Seif aliondoka nchini na kuanza ziara nje ya nchi kuzungumza na watu wengine kuhusu uchaguzi wa Zanzibar. Kuondoka kwake kuliishitua serikali?
Dk. Shein: Mimi sijashituka kwa sababu uchaguzi ule ulirudiwa kwa mujibu wa sheria na ZEC ambayo haiingiliwi na mamlaka yoyote ilitangaza mshindi na hakuna mamlaka ya kubadilisha. Sasa mimi siwezi kumzuia kutembelea watu … dunia kubwa aende tu atarudi.
Tido: Lakini kuna hili kwamba mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ameteuliwa na rais, ni lazima akutetee. Mfano, makamishna wa upinzani ndani ya ZEC hawakupo wakati anatangaza matokeo, kuashiria hapakuwa na maelewano.
Dk. Shein: Hayo muulizeni yeye, mimi najua mwenyekiti wa ZEC ndiye aliyetangaza. Yupo hai nendeni mkamuulize na hao makamishna wako saba nendeni mkawaulize watathibitisha uchaguzi ulikuwa na kasoro.
Tido: Huu ni muhula wako wa mwisho Ikulu. Unapoangalia unadhani kuna uhalali wa baadhi ya wanasiasa kuanza kupita pita kuchukua nafasi yako?
Dk. Shein: Wakifanya hivyo watakuwa wamekosea kwa sababu urais ni wa Chama cha Mapinduzi, kwa hiyo, hadi hapo CCM kitakapotoa ilani na taarifa wenye kutangaza nia wajitokeze, hapo ni ruksa kujitokeza anayefanya utaratibu wowote sasa anakwenda kinyume cha katiba ya CCM na maadili ya uongozi, na huyo akibainika atachukuliwa hatua. Juzi tulikuwa na mkutano wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM (NEC), mwenyekiti alieleza utaratibu wa chama kuhusu hao, wavute subira. Mimi sikujitangaza nimekuwa makamu wa rais miaka tisa sikuwahi kujitangaza, hata hii mara ya pili sikujitangaza nimeibuka siku ya kuchukua fomu na niliibuka kwa sababu wanaCCM walisema tunataka Dk. Shein uende peke yako ukachukue fomu.
Tido: Lakini kuna ambao unawaona wana dalili nzuri kwa mtazamo wako?
Dk. Shein: Nafasi ya uongozi si hisia na mapenzi ya mtu ni nafasi ya chama. Uamuzi utafanywa na Kamati Kuu na NEC kwa urais wa Zanzibar, kwa hiyo hata kama kuna mtu nampenda sana sina mamlaka na amri ya kumnong’oneza na kwa tabia yangu siko hivyo, chama kikimteua nitamuunga mkono.
Tido: Muungano ni suala linalozungumzwa sana. Zanzibar wapo wanaoamini haifurahii Muungano, kuna kero za Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar.
Dk. Shein: Suala la Muungano ni kubwa na la kihistoria, mahojiano haya hayatoshi kulizungumzia. Hapa tulipo (Ikulu ya Zanizbar) ndipo chumba walipoweka saini tarehe 24 Aprili 1964, mzee Karume na Mwalimu Nyerere, tarehe 26 ndipo Muungamo ulikamilishwa. Kwa nini nchi hizi ziliungana ilikuwa ghafla tu? Hapana, ni historia ya watu wa Zanzibar na Tanganyika. Muungano ni wa kidugu, kwa historia ya ASP na TANU baada ya kudai uhuru waliamua kuunganisha nchi, kwa hiyo anayesema hataki Muungano hajui historia ya nchi yake na hajitambui. Jitihada za Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume ni za kulinda nchi yetu, nchi nyingi walishindwa kuendelea na muungano waliyofanya,kuna Egypt, Syria na hata Libya walishindwa, sisi bado leo hii tunasonga mbele.
Tido: Wakati wa mchakato wa Katiba Mpya kulijitoeza hoja za Muungano wa mkataba, Zanzibar watu wanahisi kuna nguvu nyingi kutoka Bara ambayo inafanya wao wasijisikie kufanya wanayotaka.
Dk. Shein: Si kweli, tangu Muungano umeanzishwa Aprili 24, 1964 hadi kurejeshwa vyama vingi mwaka 1992 ndipo yameibuka haya. Ni wale wale waliokuwa hawataki Muungano … wachache, wale wale waliopinduliwa wakaja kwa mlango mwingine ndio hao wanaopinga Muungano.
Tido: Katika kero za Muungano kuna hili suala la uchimbaji mafuta
Dk. Shein: Ndio mafuta haya, si suala la Muungano, uchumi si suala la Muungano. Jamhuri ya Muungano na Zanzibar kila mmoja ana wizara yake, yapo mambo ya Muungano lakini si la uchumi kwa hiyo ukizungumzia mafuta ni kama imetiwa sumu fulani kwamba imejengwa hoja. Mimi nimekuwa makamu wa rais kwa miaka tisa na nusu, hili suala la mafuta si tatizo ndio maana mimi na rais Jakaya Kikwete tulilimaliza, ilitungwa sheria sasa tutazame uchimbaji utakaokuwapo. Kwa hiyo kama kuna kasoro za Muungano zilizosalia ni chache, mimi na Kikwete tulibakisha ya mafuta na tume ya fedha ya Muungano.
Kwa hiyo zipo kero za Muungano kwa mfano mnapokwenda mikutano ya kimataifa, mimi nimewahi kuwa naibu waziri wa afya na nikawa waziri wa nchi, katiba na utawala bora, kwenye vikao vya kimataifa tunakwenda pande mbili, wakati mwingine watendaji wa upande mmoja wanaghafilika kutotoa taarifa na kisha wanakwenda watu wa upande mmoja, haya ni mambo ya utendaji tu.
Hawa wenzetu wa CUF walikuja sita (kwake Ikulu – Zanzibar) wakaniambia kuhusu Muungano wa mkataba nikawaambia nendeni kwenye Tume ya Warioba mkaeleze. Nikauliza mkataba gani kwani hizi “articles of union” sio mkataba? Hizi zilizoandikwa na Mwalimu Nyerere na mzee Karume. Kwa hiyo tatizo si Muungano, tatizo ni watu wanaoutazama Muungano na hoja zao zipo wamezificha hawataki kuzisema.
Tido: Ulikuwa na rais Jakaya Kikwete sasa uko na Rais Dk. John Magufuli. Kuna tofauti ya uongozi na staili zao, unamudu namna gani, kuna upande mmoja wa Muungano hali ya kutumbuliwa majipu upande mwingine wa nchi hukuna. Hii tumbua majipu inakutikisa?
Dk. Shein: Hata kidogo. Rais Magufuli nimefanya naye kazi. Nimeingia mwaka 2001 nikiwa makamu wa rais, Magufuli akiwa waziri wa ujenzi, ilikuwa baada ya kufariki aliyekuwa makamu wa rais, Dk. Omar Ali Juma, kwa hiyo nimefanya naye kazi miaka minne na nusu akiwa waziri wa ujenzi mimi nikiwa makamu wa rais, namfahamu vizuri.
Alipokuja rais Kikwete pia nimefanya naye kazi, kwa hiyo namjua Magufuli akiwa waziri wa mifugo na uvuvi ni mtu ambaye najua uwezo wake na staili yake ya uongozi, kila kiongozi ana staili yake. Kwa hiyo uongozi unategemea unavyoongoza mwenyewe na wale unaowaongoza, uamuzi anaochukua Magufuli ni ule wa ndani ya wigo wa kisheria na huku (Zanzibar) kama husikii si kama mambo hayo hayafanywi, hapana, yanafanywa. Kuna mambo mengi yanafanywa kama hayo ya kukabiliana na rushwa, kuna kesi kadhaa. Tatizo vyombo vya habari vinakaa Dar es Salaam huku haviji lakini utumbuaji majipu upo, shughuli nyingi mimi nimefanya lakini haziandikwi, vyombo vya habari vya umma na binafsi haviji Zanzibar, vyombo vipo Dar. Tunaibua mambo halafu hamuonekani (waandishi wa habari).
Tido: Suala la Katiba Mpya, tunasubiri mchakato wa kura ya maoni. Rais Magufuli kasema hiyo si ajenda kubwa kwake hadi wakati muafaka, unaliangaliaje suala hili?
Dk. Shein: Liko wazi kabisa, mchakato tulianza mimi na Kikwete, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Katiba ya pande mbili za Tanzania, huwezi kutunga Katiba ya Muungano bila kuihusisha kikamilifu Zanzibar, na wakati wa rais Kikwete iliundwa sheria tukaunda tume yenye makamishna nusu pande zote, Katiba ile tulikabidhiwa Dodoma nakala yeye (Kikwete) akainua juu, nakala nami nikainua tukamaliza kazi, sasa ni kusubiri kura ya maoni. Kwa hiyo tulikubaliana mimi na Kikwete kama walivyokubaliana Karume na Nyerere, marais wawili tulikubaliana kutunga ile katiba, cabinet (Baraza la Mawaziri la Jamhuri) na Zanzibar (Baraza la Mapinduzi), atakayofanya Magufuli hayawezi kuwa maamuzi ya peke yake kwa sababu Katiba ni yetu sote. Hili si suala la Jamhuri ya Muungano ni pande mbili, hayafanywi na upande mmoja peke yake, yakifanywa na upande mmoja peke yake ndipo watu wanapiga kelele, mimi ndiye rais wa Zanzibar na ndiye najua mambo ya Muungano yanakwenda vipi na nashauriana na mwenzangu, sasa hivi Dk. Magufuli tunakwenda vizuri.
Tido: Kuna hili suala kwamba Katiba Inayopendekezwa inahitaji kurekebishwa (viraka), kuna mmbo ya maana yameachwa, kwa hiyo yarekebishwe kwanza. Wewe unaona hili linastahili au tuendelee na kura ya maoni?
Dk. Shein: Nadhani yamekwishafanyika, haturudi nyuma, kama kuna mambo hayamo mimi siyajui. Nimeridhika na mchakato wote na mwenzangu Kikwete, hatua ya pili ni kura ya maoni kama kuna upande mmoja haujaridhika hakuna kulazimisha, Mwalimu Nyerere hakumlazimisha Karume walikaa wakakubaliana, hawezi kutokea mtu kuilazimisha Zanzibar kwamba kama hamtaki itakuwa hivi.
Tido: Magufuli alipokuja kushukuru hapa Zanzibar alikutaka uwe mkali kidogo, umekuwa mkali?
Dk. Shein: Mimi nina aina yangu ya uongozi, niliosoma nao wanajua kule sekondari hadi chuo kikuu hadi nje ya nchi, sipendi kusema sema sana napenda kufanya kazi, waulize mzee Mkapa na Kikwete, upole haina maana kwamba wewe ni mtu dhaifu, utaratibu ni busara na sifa ya uongozi, haina maana kwamba utaratibu unaachia watu waharibu nchi, uongozi ni busara, si kwamba Magufuliu kasema vile basi ni udhaifu, hapana, hajakosea, ni sifa yangu napenda kupima mambo kutumia busara sana, wala sina hasira za haraka, lakini mtu akiharibu kazi simuachi, nitakwenda naye hadi dakika ya mwisho.
Chanzo: Raia Mwema.
Dk. Shein: Magufuli hawezi kuamua ‘kivyake’ kiporo cha Katiba Mpya – Raia Mwema