Tunataka wawekezaji, mara wanyang'anyeni leseni!

Ndikwega

R I P
Feb 1, 2012
5,979
5,524
Moja ya vitu vinanishangaza kwenye Utawala huu wa Magufuli, yupo Mbele saana kwamba tunahitaji Wawekezaji wa Ndani na Nje, sasa linapokuja swala la Kuwaambia tena waondoke ndipo nachoka sasa.

Juzi juzi kasema Wawekezaji waliopo huko kanda ya Ziwa (Homeland) wasiwasumbue Wananchi. Leo tena Bariadi kasema muwekezaji eneo ambalo ndipo linatakiwa lijengwe Tank la Maji kuwa kama vipi wamnyang'anye lesseni yake. Maeneo hayo mlipokuwa mnagawa hamkujua kuwa patatakiwa papitishwe nini.

Cha kujiuliza, sasa hawa wawekezaji wana kosa lipi maana wapo eneo husika kihalali. Pia, yeye anahamasisha ama kuwakaribisha wawekezaji halafu baadaye mnawageuka sijui tuwaelewaje sasa. Mwishowe wataona Serikali yako haiamiki na hawatakuja tena kuwekeza

Kumbuka hautaishia hilo, pia mtaingia hata kwenye viwanda unavyovisema nchi ndiko inaelekea. Na haya ni madhara ya kufanya hotuba ambazo zinatoka kichwani moja kwa moja bila kuhaririwa na mtu huna karama hiyo.

Hapo ulipo Mkulu nawewe Utapita tu.
 
Huyo jamaa kalipa fidia ya mabilioni kwa wananchi kuchukua maeneo,kafanya exploration kwa mabilioni ya shilingi,kaweka wafanyakazi,kaagiza mitambo

Tujiandae kulipa fidia ya mabilioni,escrow na IPTL inaikumba nchi,tutalipa fidia GEITA na huko ngasamo na kwingine

Fidia mpaka sasa itafika trilioni kadhaa ikijumuisha loss of profit and business

Pia wakienda mahakamani tutashindwa na kuwafidia na eneo kubaki lao

Hawajapewa hata haki ya kusikilizwa kabla ya kunyanganywa,kesi rahisi sana kuishinda

Unajifanya kuwapenda wananchi halafu unawatwisha zigo la fidia!!!
 
Badala ya Kuhangaika na Kudai Kodi yake yeye anaingilia Upuuzi. Yaani Nchi chini ya Magufuli haiana Utaratibu wa Measure Risk za maamzi pia.
 
Ndo maana sifa kuu ya kiongozi ni busara

sababu wanaweza kuja watu kukulilia na machozi..kumbe watu hao wanaolia ndo wezi wakubwa
na waonevu....

Ndo busara inapohitajika

binafsi kiongozi yeyote anaependa kufanya maamuzi kwenye jukwaa huwa namuona 'hamna kitu'

Uongozi ni details details na more details....
 
Uko sahihi kabisa mkuu! Sasa kwa mfano yule muwekezaji kosa lake silioni kabisa.
 
Kwani lazima tank likae hapo mlimani?,
afterall hilo tank linachukua heka elfu ngapi mpaka wamtoe mwekezaji?,
maana kwa uzoefu hakuna tank la kuzidi robo heka,
hata matank ya nuclear power hayawi makubwa kihivyo
 
Umeenda mbali sana,kama huyo mwekezaji angeenda mbali kama wewe basi lazima angetafuta jinsi ya kusaidia wananchi wapate hilo eneo la kujenga tank ili wapate maji,maana maji ni uhai.
Sidhani kama wameongea naye. Mbona yule Afsia Madini na yule Engineer wa Maji hajaongelea hilo, na maamzi yametolewa kwa maneno yao.
 
Kwani lazima tank likae hapo mlimani?,
afterall hilo tank linachukua heka elfu ngapi mpaka wamtoe mwekezaji?,
maana kwa uzoefu hakuna tank la kuzidi robo heka,
hata matank ya nuclear power hayawi makubwa kihivyo
Afisa Madini kasema likikaa hapo litakuwa Disturbed na Uchimbaji wa Madini.
 
Mbona hata Twiga Cement kalipa watu fidia mara mbili na eneo bado lina watu
na serikali sasa inatetea hao watu..

ndo hasara za viongozi 'populous '
Tuna safari ndefu Nchi za Afrika hizi. Ukipata viongozi ndiyo kama hawa, kila jambo lipo mikononi mwake na anaongoza nchi bila kuzingatia utawala wa sheria.
 
Kwanini zisijengwe concrete towers sehemu nyingine wakaweke matanki ya maji, cha muhimu si mwinuko tu? Ajira ngapi hapo zitapotea kwa kufuta leseni ya mwekezaji?! Eneo lenyewe full ukame, watu watakula maji tu?! Ehe Mungu mbona umetuacha?!
 
Huyu anatutia hasala na ukurupukaji wake. Huyu muwekezaji ana haki zote za kumburuza mahkamani na mwisho wa siku ni kodi zetu zina cover upuuzi wake.

Nimeamini kila binadamu ana aina ya ukichaa wake. Ila ukichaa wa bwana yule ni wa level nyingine.
 
Back
Top Bottom