Tunaposhangilia sheria ya kumrejesha binti aliyezaa shuleni, tusisahau kuuliza haki ya yule mtoto mchanga aliyezaliwa anayebaki nyumbani

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Ni jambo jema tunapofanya kampeni ya kwamba watoto wetu waliopata mimba wakiwa mashuleni wakakatisha masomo warudi mashuleni kuendelea na masomo

Lakini ni muhimu zaidi kujiuliza vichanga vilivyozaliwa vitabaki wapi? Na nani atakua akiwalea?

Tukiachilia mbali zile familia chanche zenye uwezo wa kubeba jukumu la kulea vichanga yaani kumlea mama ambaye ni mtoto na mtoto; familia nyingi anayezaa ndio mwenye jukumu la kulea kichanga chake, na ukizingatia mazingira ya shule, nyumbani, hali ya maisha ya familia zao hizohizo familia nyingi ndizo ziko mabinti zake wako kwenye hatari zaidi ya kupata mimba za utotoni.

Wizara ya elimu na wizara ya afya mseme neno kuhusu hivi vichanga. Mama zao wakienda shuleni wao wanabaki wapi, wanabaki na nani, katika umri gani na utaratibu upi?

Nieleweweke tuu kwamba sijapinga watoto wa kike wanaopata mimba za utotoni kurudi mashuleni ila nawaza wakati wao wakirudi shuleni wale watoto wao wanabaki na nani na kwenye hali gani

Screenshot_20211124-131201.jpg

Mungu awanze wazazi wote tuweze kuendelea kuwalea watoto wetu.

Hakuna mwenye ufundi wa kulea, hakuna bingwa wa kulea, hakuna awezae kutembea na mwanae kila mahala. Ila tupambane zaidi kuwalinda watoto wetu kwa maombi, ibada na malezi waweze japo kuondokana na majanga ya kuacha shule zaidi ya kupambana

Mungu ibariki Tanzania
Screenshot_20211125-080228.jpg

Screenshot_20211125-080113.jpg

Screenshot_20211125-080039.jpg

Ninaamini serikali kuwekeza nguvu nyingi kupinga watoto wetu kujihusisha na tendo la ndoa nje ya ndoa.

Ninaamini katika serikali kuweka jitihada zaidi, hasa za usalama, kuwalinda zaidi watoto walio kwenye hatari ya kubakwa.

Kuruhusu watoto wenye watoto kurudi shule ni kama wanapigia debe na kuwahamasisha watoto kujihusisha na tendo la ndoa nje ya ndoa, hii siyo sahihi.
 
Ni jambo jema tunapofanya kampeni ya kwamba watoto wetu waliopata mimba wakiwa mashuleni wakakatisha masomo warudi mashuleni kuendelea na masomo

Lakini ni muhimu zaidi kujiuliza vichanga vilivyozaliwa vitabaki wapi? Na nani atakua akiwalea?

Tukiachilia mbali zile familia chanche zenye uwezo wa kubeba jukumu la kulea vichanga yaani kumlea mama ambaye ni mtoto na mtoto; familia nyingi anayezaa ndio mwenye jukumu la kulea kichanga chake, na ukizingatia mazingira ya shule, nyumbani, hali ya maisha ya familia zao hizohizo familia nyingi ndizo ziko mabinti zake wako kwenye hatari zaidi ya kupata mimba za utotoni.

Wizara ya elimu na wizara ya afya mseme neno kuhusu hivi vichanga. Mama zao wakienda shuleni wao wanabaki wapi, wanabaki na nani, katika umri gani na utaratibu upi?

Nieleweweke tuu kwamba sijapinga watoto wa kike wanaopata mimba za utotoni kurudi mashuleni ila nawaza wakati wao wakirudi shuleni wale watoto wao wanabaki na nani na kwenye hali gani

View attachment 2021808

Mungu awanze wazazi wote tuweze kuendelea kuwalea watoto wetu

Mungu ibariki Tanzania
kwani wewe ukizaa na unakuwa umeenda kazini asubuhi hadi jioni, nani anakilea kichanga chako? halafu, ukimnyima elimu msichana huoni kama umemnyima pia huyo mtoto maisha yake mazuri ya baadaye kwasababu mamake atashindwa hata kuja kumlea baadaye. wakibaki wote nyumbani iyo cycle ya poverty itaisha? wewe ni mwanamke mwenye uke kabiswa unawaza namna hiyo dhidi ya wanawake wenzio? hayo ilitakiwa tuwaze sisi wanaume lakini sio wewe.
 
Uhuru wa kutoa mawazo .. ndio huu. Watalelewa na walezi wao ( mama, bibi , shangazi n.k ) nyie mnapo zaa huku mmeajiriwa baada ya kujifungua na kumaliza ule mda , manaachawaga watoto na nani ? Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake

Mimi namuongelea yule mtoto aliyezaa mtoto wske. Haki ya kile kichanga anapewa na nani?

Na siwaongelei hawa wenye wazazi walio na uwezo wa kuwalea, naongelea wale watoto wasio hata na wakuwalea. Wala sijasema wasirudi shuleni, nimeuliza hivyo vichanga vyao inakuwaje?
 
Wamama zetu wengine walituzaa wakiwa na miaka 16 , waliendelea na shule wakafanya maisha na sie hadi leo hii tupo... mwanamke akisha zaa sio mtoto huyo. Maana kama utatumia kigezo cha umri number hata wewe leo ni mtoto kwa mtu flani... nyie wanawake hampendanagi tu
 
Lilikuwa kosa kubwa sana SSH kusema viatu vya JPM vilikuwa vikubwa. Kwenye hili amedhihirisha ubabe uliokuwepo wakati ule. Amedhihirisha masononeko aliyokuwa nayo wakati ule.

Hongera sana SSH.

UMEMPA NAFASI MTOTO WALAO AMALIZE MASOMO YAKE. HONGERA SANA.

Sasa tujiandae na upungufu wa wasichana wa kazi na mabaamedi.

Umeonyesha ukomavu na maamuzi magumu kama uamuzi wa kuanzisha shule za kata wakati ule.

Umeonyesha ukomavu wa kuruhusu anayetaka kuchanja achanje dhidi ya CORONA.
 
kwani wewe ukizaa na unakuwa umeenda kazini asubuhi hadi jioni, nani anakilea kichanga chako? halafu, ukimnyima elimu msichana huoni kama umemnyima pia huyo mtoto maisha yake mazuri ya baadaye kwasababu mamake atashindwa hata kuja kumlea baadaye. wakibaki wote nyumbani iyo cycle ya poverty itaisha? wewe ni mwanamke mwenye uke kabiswa unawaza namna hiyo dhidi ya wanawake wenzio? hayo ilitakiwa tuwaze sisi wanaume lakini sio wewe.

Naenda kazini namwacha msaidizi mwenye namwachia maelekezo na mahitaji yote ya mtoto wangu. Namlipa na kuhakikisha mtoto anapata ninachokitaka mimi kimalezi na makuzi

Usisahau mimi ni mwanamke na nna watoto wa kike pia ukafikiri staki mabinti wasome.... utakua unakosea! Maana unakua unamuangalia mtoto mmoja tuu yule aliyezaa huyo mwingine aliyezaliwa humwangalii; au utakua unamwangalia mtoto wa familia bora zaidi wakati wengi wa hao wanatoka mazingira magumu.

Najaribu kuwaangalia watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu zaidi ambapo hata wao binafsi kupata mahitaji yao ni shughuli! Sasa hivyo vichanga itakuaje
 
Inaonekana hili suala hujalipenda mpaka unatafuta sababu petty kabisa...eti mtoto atalelewa na nani, unadha i huyo mama yake mtoto anaweza kwenda shule bila kuwa na uhakika mtoto anabaki vipi?kinachopiganiwa hapa ni mwanafunzi aliyepata mimba apate nafasi na kurudi shule pale atakapohitaji
 
siamini kama hadi leo kuna wanawake wenye fikra kama za kwako. ilitakiwa sisi wanaume tufikiri hivyo lakini sio wewe mwenye sehemu za kike kabisa, au zimechanganya?
 
Lilikuwa kosa kubwa sana SSH kusema viatu vya JPM vilikuwa vikubwa. Kwenye hili amedhihirisha ubabe uliokuwepo wakati ule. Amedhihirisha masononeko aliyokuwa nayo wakati ule.

Hongera sana SSH.

UMEMPA NAFASI MTOTO WALAO AMALIZE MASOMO YAKE. HONGERA SANA.

Sasa tujiandae na upungufu wa wasichana wa kazi na mabaamedi.

Umeonyesha ukomavu na maamuzi magumu kama uamuzi wa kuanzisha shule za kata wakati ule.

Umeonyesha ukomavu wa kuruhusu anayetaka kuchanja achanje dhidi ya CORONA.

Rais wetu SSH amefanya jambo jema wala hakuna lawama kwake.
Ninachouliza vipi kuhusu vile vichanga vunavyobaki mtaani?? Kama huyu wa miaka13, 15 ameweza kuwa kwenye sehemu hatarishi hadi kupata mimba. Vipi kuhusu kile kichanga ambacho tambui kabisa??

Na siongelei hawa waliokua kwenye mazingira bora bali wale wengi walio kwenye mazingira magumu
 
Inaonekana hili suala hujalipenda mpaka unatafuta sababu petty kabisa...eti mtoto atalelewa na nani, unadha i huyo mama yake mtoto anaweza kwenda shule bila kuwa na uhakika mtoto anabaki vipi?kinachopiganiwa hapa ni mwanafunzi aliyepata mimba apate nafasi na kurudi shule pale atakapohitaji

Sio kwamba sijalipenda. Utakua unaongea kama mtu aliyezaliwa mijini na kukulia mjini weweee

Tumepata suluhu kwa yule mtoto aliyedrop shule kurudi kuendelea na masomo yake. Vipi kuhusu yule aliyezaliwa

Badala ya kulaumu njoo na hoja kwa kuzingatia wale wasio na uwezo kabisa wa kutunza hao waliopata mimba kwanza kabla ya vichanga
 
siamini kama hadi leo kuna wanawake wenye fikra kama za kwako. ilitakiwa sisi wanaume tufikiri hivyo lakini sio wewe mwenye sehemu za kike kabisa, au zimechanganya?

Ungekua unajua zamani jamii ilikua inaiishi vipi na malezi yalikua yanafanyikaje; na sasa maisha yamegeukia wapi ungenielewa
 
Sio kwamba sijalipenda. Utakua unaongea kama mtu aliyezaliwa mijini na kukulia mjini weweee

Tumepata suluhu kwa yule mtoto aliyedrop shule kurudi kuendelea na masomo yake. Vipi kuhusu yule aliyezaliwa

Badala ya kulaumu njoo na hoja kwa kuzingatia wale wasio na uwezo kabisa wa kutunza hao waliopata mimba kwanza kabla ya vichanga
Kuhusu mtoto, mama yake ataamua alee ama arudi shule, cha msingi na nafasi ya kurudi shule kujiendeleza iwepo atakapotaka...kwa sababu siyo lazima wala hatashikiwa kiboko kurudi, ila akitaka kurudi aruhusiwe mbona ipo clear
 
Ewaaaa!!! Umenena The Wolf💥

Kwa maana hiyo tunaweza kufurahia hiyo ruhusa lakini utekelezwaji wake ukawa hafifu au usiotekelezeka......... sababu tuu swala la mtoto wa huyo mtoto anayetakiwa kurudi shuleni halijawekwa sawa
 
Back
Top Bottom