Tunaposhangilia sheria ya kumrejesha binti aliyezaa shuleni, tusisahau kuuliza haki ya yule mtoto mchanga aliyezaliwa anayebaki nyumbani

Najaribu kuwaangalia watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu zaidi ambapo hata wao binafsi kupata mahitaji yao ni shughuli! Sasa hivyo vichanga itakuaje
Who are you by the way. Mazingira magumu kiaje labda? Si watu wanazaliqa na wanakuwa ,masikini ama namna anavyokuwa nayeye. So hao wa kupata mimba ni wanatokea hayo mazingira magumu tu so wanaotokea mazingira malaini hawapo ama ngono inabagua hadhi ya mtu.

Yaani bana mpaka umri haujui kuwa maisha sio level Kama una maisha malaini shukuru na usilazimishe kila mtu maisha yake yalainike yawe Kama yako. Wao waache waishi kwa namna Yao wanayoishi.
 
Ni jambo jema tunapofanya kampeni ya kwamba watoto wetu waliopata mimba wakiwa mashuleni wakakatisha masomo warudi mashuleni kuendelea na masomo

Lakini ni muhimu zaidi kujiuliza vichanga vilivyozaliwa vitabaki wapi? Na nani atakua akiwalea?

Tukiachilia mbali zile familia chanche zenye uwezo wa kubeba jukumu la kulea vichanga yaani kumlea mama ambaye ni mtoto na mtoto; familia nyingi anayezaa ndio mwenye jukumu la kulea kichanga chake, na ukizingatia mazingira ya shule, nyumbani, hali ya maisha ya familia zao hizohizo familia nyingi ndizo ziko mabinti zake wako kwenye hatari zaidi ya kupata mimba za utotoni.

Wizara ya elimu na wizara ya afya mseme neno kuhusu hivi vichanga. Mama zao wakienda shuleni wao wanabaki wapi, wanabaki na nani, katika umri gani na utaratibu upi?

Nieleweweke tuu kwamba sijapinga watoto wa kike wanaopata mimba za utotoni kurudi mashuleni ila nawaza wakati wao wakirudi shuleni wale watoto wao wanabaki na nani na kwenye hali gani

View attachment 2021808

Mungu awanze wazazi wote tuweze kuendelea kuwalea watoto wetu.

Hakuna mwenye ufundi wa kulea, hakuna bingwa wa kulea, hakuna awezae kutembea na mwanae kila mahala. Ila tupambane zaidi kuwalinda watoto wetu kwa maombi, ibada na malezi waweze japo kuondokana na majanga ya kuacha shule zaidi ya kupambana

Mungu ibariki Tanzania
Hawajatunga sheria ya kuruhusu mtoto kwenda shuleni ila waziri katoa tamko tu.
 
Ninaamini katika serikali kuwekeza nguvu nyingi kupinga watoto wetu kujihusisha na tendo la ndoa nje ya ndoa - kwa sera na sheria.

Ninaamini katika serikali kuweka jitihada zaidi, hasa za usalama, kuwalinda zaidi watoto walio kwenye hatari ya kubakwa.

Kuruhusu watoto wenye watoto kurudi shule ni kama wanapigia debe na kuwahamasisha watoto kujihusisha na tendo la ndoa nje ya ndoa, hii siyo sahihi.
 
Who are you by the way. Mazingira magumu kiaje labda? Si watu wanazaliqa na wanakuwa ,masikini ama namna anavyokuwa nayeye. So hao wa kupata mimba ni wanatokea hayo mazingira magumu tu so wanaotokea mazingira malaini hawapo ama ngono inabagua hadhi ya mtu.

Yaani bana mpaka umri haujui kuwa maisha sio level Kama una maisha malaini shukuru na usilazimishe kila mtu maisha yake yalainike yawe Kama yako. Wao waache waishi kwa namna Yao wanayoishi.

Rudi kasome uelewe uache majibumhemko
 
Acha kuhaha.Watoto wa kike wakipata mimba wana haki ya kurudi shule.

Hakuna kuhaha! Tumia akili yako na uwe mkweli

Screenshot_20211125-080113.jpg
Screenshot_20211125-080039.jpg
 
Hakuna aliyekataa wasirudi shule. Waliozaliwa nao ni watoto wenye wana haki ya kulelewa. Mpango ukoje?
Kwani ambaye kaajiriwa au kajiajiri akishajifungua si anaandaa mazingira ya kumuacha mtoto ili arudi kazini?

Na huyu binti naye ataandaa mazingira ya yeye kurudi shule.

Au ulikuwa unapendekeza serikali ifanyaje? Iwapatie wadada wa kazi mabinti wote kabla ya kurudi shule?
 
Kama unaweza kumlinganisha aliyeajiriwa na mtoto wa miaka 14 aliyezaa tena ambaye wazazi wake hawana ajira wala biashara wewe sio mzima.

Rudi kwenye post ndio uje na maswali
 
Ewaaaa!!! Umenena The Wolf💥

Kwa maana hiyo tunaweza kufurahia hiyo ruhusa lakini utekelezwaji wake ukawa hafifu au usiotekelezeka......... sababu tuu swala la mtoto wa huyo mtoto anayetakiwa kurudi shuleni halijawekwa sawa
Sasa unataka liwekwe sawa vipi? Kwamba serikali ihusike pia kulea hawa vichanga? Kweli kumridhisha binadamu ni jambo gumu sana! Mlikuwa mnalilia warudi shule. Wameruhusiwa kurudi shule mnaleta chokochoko nyingine.
 
Kama unaweza kumlinganisha aliyeajiriwa na mtoto wa miaka 14 aliyezaa tena ambaye wazazi wake hawana ajira wala biashara wewe sio mzima.

Rudi kwenye post ndio uje na maswali
Sizungumzii suala la umri wa aliyejifungua nimeuliza swali kwako kutokana na mada uliyoileta kuwa wewe unataka hilo jukumu la mazingira ya huyo mtoto kurudi shule akamwacha kichanga liwe la nani?

Aliyejifungua ameshafunguliwa milango ya kurudi shule, suala la anarudije si jukumu lake na familia yake? Au kuna la kufanyika ambalo wewe unaliona?
 
Kama unaweza kumlinganisha aliyeajiriwa na mtoto wa miaka 14 aliyezaa tena ambaye wazazi wake hawana ajira wala biashara wewe sio mzima.
Haya toa sasa mapendekezo yako. Unataka serikali ifanye nini cha ziada? Mlikuwa mnataka wali mmepewa, baada ya kupewa kabla hata ya kushukuru mnadai pilau, baadaye mtadai biriani...... na orodha inaweza kuendelea..... Tujifunze kushukuru na kuridhika hata kwa hatua hii tulioifikia, hasa ukichukulia maanani kuwa mwendazake aliweka msimamo wa wazi tena kwa ukali kuwa hatakuwa tayari kuruhusu watoto waliopata ujauzito kurudi shule.
 
Sasa unataka liwekwe sawa vipi? Kwamba serikali ihusike pia kulea hawa vichanga? Kweli kumridhisha binadamu ni jambo gumu sana! Mlikuwa mnalilia warudi shule. Wameruhusiwa kurudi shule mnaleta chokochoko nyingine.

Kutaka kuboresha hiyo elimu ya mtoto wa kike ni Chokochoko!!!?? Hebu acha unafki buana

Screenshot_20211125-080228.jpg
Screenshot_20211125-080113.jpg

Screenshot_20211125-080039.jpg
 
Hakuna aliyekataa wasirudi shule. Waliozaliwa nao ni watoto wenye wana haki ya kulelewa. Mpango ukoje?
Kama mwanamke nilitegemea ungetoa ushauri wa namna watoto wanaozaliwa waleleweje, ila umeacha swali na huku ukidai haupingi, ili kwamba hilo swali likikosa jibu basi iwe si vyema huo mpango kuanza kufanya kazi.

Mimi ni mwanaune ngoja nikujibu.
1. Kuiga namna watu wanaozaa wakiwa ni wafanyakazi.
2.Kuiga namna wenzetu wakenya wanavyofanya.

Tufikirie namna ya kuwezesha jambo zuri.
 
Kama mwanamke nilitegemea ungetoa ushauri wa namna watoto wanaozaliwa waleleweje, ila umeacha swali na huku ukidai haupingi, ili kwamba hilo swali likikosa jibu basi iwe si vyema huo mpango kuanza kufanya kazi.

Mimi ni mwanaune ngoja nikujibu.
1. Kuiga namna watu wanaozaa wakiwa ni wafanyakazi.
2.Kuiga namna wenzetu wakenya wanavyofanya.
kirie namna ya kuwezesha jambo zuri.

Huu ni mjadala unaolenga kuangalia haki na usalama wa watoto wote wawili bila kuangalia mchangiaji au mtoa maada ni mwanamke au mwanaume!

Wakati tunachangia ni vizuri tujue hatuwezi kulinganisha mazingira ya hawa watoto wanaopata mimba za utotoni na watu wazima wanaozaa wakiwa wafanyakazi. Tuangalie pia watoto wa mazingira gani wanaathirika zaidi, nini kinasababisha kuwa kwenye risk kubwa zaidi ya kupata mimba za utotoni, nini kifanyike kuzuia na nini kifanyike ili watoto wanaochwa majumbani wawe salama

Tuwe wakweli bila mihemko, tumepokea kwa furaha mtoto kurudi shule sasa tuangalie usalama yule mtoto anayeachwa nyumbani kwa faida ya kizazi chetu

Naongea kama mzazi mtu mzima ninayejua malezi na makuzi ya vichanga yanavyoweza kukupeleka kasi. Zile siku 84 hazitoshagi kuwa nyumbani fulltime, zile nusu siku za miezi mitatu kwenda 6 nazo zipo lakini mziki wake tunaujua
 
Wewe unashauri nini kwa huo mpango?
 
Kutaka kuboresha hiyo elimu ya mtoto wa kike ni Chokochoko!!!?? Hebu acha unafki buana

View attachment 2022778View attachment 2022779
View attachment 2022781
Unajua maana ya "unafiki?" Anyways, turudi kwenye mada.

Sasa mbona hutoi mapendekezo unataka serikali ifanye nini zaidi ya hivyo ilivyofanya?

Ushauri wa bure:
Busara ya kukosoa jambo fulani, ni kutoa pia mapendekezo na ushauri ya nini ungependa kifanyike ili kulifanya jambo hilo liwe zuri/bora zaidi. Kukosoa na kulalamika pekee bila kuonyesha njia mbadala haisaidii.
 
Naomba ile sheria ya kwenda jela miaka 30 pia ifutwe ili mama mtoto akiwa shule, baba mtoto abaki na mtoto
 
Unajua maana ya "unafiki?" Anyways, turudi kwenye mada.

Sasa mbona hutoi mapendekezo unataka serikali ifanye nini zaidi ya hivyo ilivyofanya?

Ushauri wa bure:
Busara ya kukosoa jambo fulani, ni kutoa pia mapendekezo na ushauri ya nini ungependa kifanyike ili kulifanya jambo hilo liwe zuri/bora zaidi. Kukosoa na kulalamika pekee bila kuonyesha njia mbadala haisaidii.

Uwe unasoma posts na comments kabla hujarukia kusema hakuna ushauri.

Hili ni swala la uhai, haki na wajibu wa jamii na serikali; ni swala ki-sera sio blahblah.

Rudi kasome huu uzi upya ndio uje kucoment. Na tunapojadili uwe unaiangalia changamoto katika upana wake sio uangalie toka kwenye nyumba yako unayoishi tuu. Sawa eeeh
 
Back
Top Bottom