Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,702
- 36,143
Ndoa msingi wake ni upendo bila kujali nani ana ajira, ana biashara, ana cheo au hana kitu.
Na jukumu kubwa la mwanaume ni kumpenda mke wake(upendo ndani yake kuna wajibu wa kucare umpendaye). Mwanaume ndiye anapaswa kuleta mahitaji yote muhimu kwenye familia yake kwa kadri ya nguvu na akili zake.
Wajibu wa mke ni kumtii mume wake. Mume akisema kaa nyumbani kwa maslahi ya familia wewe utapaswa kubaki nyumbani, mume akifungua biashara usimamie unapaswa ufanye kama ulivyoamriwa
Mume ni commander in chief wa familia.
Muhubiri wa leo anasema kuwa mume humuheshimu mke mwenye kipato chake ilhali nyie wote ni mashahidi hali ilivyo kwenye hizi ndoa zenye wenza wote wenye vipato vyao. Ndoa zao hazidumu, na zingine zinadumu lakini migogoro haiishi. Wanaume wengi waliooa wanawake wenye vipato vyao tendo la ndoa hupewa kwa kipimo, vyakula hutengewa na house maids n k
Sasa hawa wahubiri wanaoibuka kama uyoga baada ya kukosa Neno litokalo kwa Mungu wameamua kufundisha falsafa za ulimwengu ambazo unaweza kuzipata popote. Kuwasikiliza wahubiri wanahubiri falsafa za ulimwengu ni heri ununue bando ujifundishe jambo lolote upendalo maana hutatoa sadaka, hutalipia Daladala kuwafuata, hutatumia muda mwingi. Maana ukisema uwafuate walipo utatumia siku mzima while ukiwa chumbani kwako lisaa limoja linatosha kujifunza chochote mtandaoni.