Serikali iangalie uwezekano wa kutoa mikopo kupitia halmashauri kwa mtu hata mmoja mmoja badala ya kulazimishwa kuwa katika kikundi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,293
9,723
Ndugu zangu watanzania,

Mfumo uliopo kwa Sasa juu ya pesa za halmashauri zinazotolewa Kama mkopo kwa vijana kutokana na makusanyo na mapato ya ndani unataka vijana au akina mama au watu wenye ulemavu kuweza kujiunga au kuunda kikundi cha kijasiriamali ili kuweza kupatiwa mkopo, ambapo hapa kuna taratibu za kufuata ili kukidhi vigezo Kama vile kutengeneza katiba, kuwa na akaunti ya kikundi, viongozi wa kikundi, mradi au wazo la mradi au biashara na mengineyo.

Ndugu zangu katika utolewaji wa pesa hizi hazitoi fursa kwa mtu mmoja mmoja kupatiwa mkopo, ukiwa kijana pekee huwezi ukapata mikopo hii hata Kama Ni muaminifu,una wazo zuri la biashara au mradi au una mradi au biashara ambayo ungependa uongeze na kukuza mtaji wako.

Hali hii inawanyima fursa vijana wengine ambao wanaona katika vikundi Kuna kuwa na baadhi ya changamoto Kama vile uaminifu mdogo kwa baadhi ya wanakikundi,kutofautiana kwa malengo, matumizi mabaya ya Fedha, uzembe wa baadhi ya wanakikundi, wengine kuchukua hela na kuishia kugawana pasipo kutumia katika malengo husika.

Kutokuwa na Elimu ya kutosha juu ya mradi au biashara tarajiwa na hivyo kuishia kupoteza mtaji wote kabla hata ya kurejesha, Haraka ya baadhi ya Wana kikundi au vijana kutaka utajiri wa haraka haraka na hivyo kuwekeza katika maeneo hatari wasio na uzoefu nayo au ujuzi nao zaidi ya habari za kusikia tu juu ya faida kubwa watakayoipata.

Hivyo nilikuwa naona Ni wakati wa serikali ya Rais wetu mpendwa mama Samia kuangalia uwezekano wa kutoa fursa ya mkopo kwa mtu hata mmoja mwenye kuhitaji mkopo huu huku wenye kuungana na kuwa kikundi nao waendelee kupewa Kama kawaida,hii itarahisisha na kusaidia vijana wengi Sana kuweza kupata mikopo na kuwasaidia vijana wengine hata kimawazo na kiushauri.

Vigezo vinavyoweza kutumika ni Kama vile uwepo wa Taarifa za kutosha juu ya mwenendo wa kiuadilifu, kiweledi, kimaadili, kiutendaji, kiuaminifu na kitabia kutoka katika uongozi wa serikali za mitaa.

Uwepo wa mdhamini anayeaminika na mwenye makazi ya kudumu katika eneo analotokea na kuishi kijana anayehitaji mkopo, mdhamini akubali kuwajibika endapo mhusika au kijana ataamua kukimbia au kutoroka kabla ya kurejesha pesa halmashauri.

Mdhamini asaiini fomu maalumu mbele ya mwanasheria wa serikali na kula kiapo cha kuwajibika juu ya Deni la anaye mdhamini na kopi ya fomu hiyo ibaki halmashauri ,nyingine kwa mwanasheria,nyingine kwa serikali ya mtaa ,nyingine kwa anayechukua mkopo na nyingine abaki nayo mdhamini.

Mdhamini awe na Mali zisizo hamishika na zenye hati inayotambulika kisheria,mdhamini awe Ni mzazi wa mhusika au mtu mwingine yeyote mwenye Mali zisizo hamishika na makazi ya kudumu eneo husika,Mdhamini akitaka kumdhamini mtu zaidi ya mmoja aruhusiwe mpaka pale tu itakapothibitika kuwa Mali za mdhamini Zina thamani kubwa ukilinganisha na mikopo au fedha inayotaka kuchukuliwa.

Hili Jambo litasaidia halmashauri kupata marejesho ya mikopo yote inayotolewa kwa vijana lakini pia itawasaidia vijana wengi kupata mikopo kwa urahisi bila mlolongo wa kutafutana na hata kuwalazimisha wengine ili wajiunge kwenye vikundi kusudi kutimiza lengo la kupata mkopo ambapo mwisho wa siku Hawa walio lazimishwa au kupachikwa kwenye kikundi kuweza kusaidia kupata mkopo wanakuwa hawana ule moyo au ufanisi mzuri na uwajibikaji mzuri na wanakuwa hawana mchango wowote ule katika kukuza ,kulinda na kuendeleza mtaji.

Naiomba Sana serikali iliangalie hili kwa jicho la kipekee kabisa, maana unakuta mtu unalima lakini unakosa hela ya pembejeo hasa mbolea kwa kuwa unawaza ukitaka mkopo wa kupanua kilimo chako inahitaji uende kwenye kikundi ambacho unajikuta nacho kina malengo mengine kabisa Kama vile ufugaji wa kuku wa mayai au ng'ombe wa maziwa ambapo unaona wewe huwezi ukapata hata nafasi ya kwenda kukatia ng'ombe majani au kuwawekea maji kuku kwa kuwa wewe shughuli zako Ni shambani muda mwingi na ndio Jambo unalolipenda kuliko ufugaji wa kuku wa mayai au nyama au ng'ombe wa maziwa.

Unakuta kikundi kimeundwa na kuomba mkopo wa Jambo fulani lakini Wana kikundi kila mmoja ana malengo yake kichwani juu ya hela ikiwa mkononi mwao, hivyo kupelekea mradi uliolengwa kukosa nguvu ya pamoja ya wanakikundi.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
 
Mjomba kana ulikuwa mawazoni mwangu. Muda si mwingi kuna fursa nimeisomea gepu nikawa nafikiria kianzio vipi ndipo nikawa mikopo ya serikali lo kucheki lazima kikundi afu bado sasa ufuatiliaji wake tatizo tena
 
Naamini serikali yetu itaangalia suala hili na kulifanyia kazi ili vijana wengi wanufaike na utaratibu huu mpya ambao nimeona utakuwa mzuri na kuwanufaisha vijana wengi
 
Wazo zuri sana.

Hivi vikundi hata ule mwanzo tu wa kufatilia huo mkopo huwa ni changamoto. Ni mara chache sana kukuta wotw mna nia na uhitaji sawa.

Inakuja tokea yule/wale wenye uhitaji sana na mkopo huo ndio wanawajibika zaidi huku wengine wao wakipokea taarifa tu ya kinachojiri.
 
Pia ikiwa mmoja katika kundi ana mkopo through kundi lingine na haujaisha, inachelewesha/kukosa mkopo
Serikali ikiruhusu hata mtu mmoja kupatiwa mkopo changamoto Kama hizo zitapungua ,lakini pia urejeshaji wa mikopo itakuwa Rahisi na hata kuwafuatilia wahusika itakuwa nirahisi katika kujuwa maendeleo yao
 
Wazo zuri sana.

Sema wewe hukawii kugeuka siku Samia akinena tofauti na haya.

Uchawa shida sana. Tena utampongeza.

Ukiwa chawa hauko huru na mawazo yako hadi mkurungwa akiongea.
Mimi kazi yangu ni kuusema ukweli kupitia akili yangu na ninavyokuwa naona mambo kwa maslahi mapana ya Taifa letu na ustawi wetu sisi watanzania
 
Juzi nilienda kupata ABCD kama kijana nikaambiwa hayo hayo ya kikundi nilimchallenge yule dada Afisa Maendelo kuhusu kuruhusu mkopo wa mmoja mmoja akasema hilo suala limejadiliwa na sio muda Wizara itatoa tamko lakini hadi sasa kuna matumaini ya kuja kwa mikopo ya mtu mmoja mmoja,
Endelea kua karibu na Halmashauri yako utakuja kupokea habari njema.
 
Juzi nilienda kupata ABCD kama kijana nikaambiwa hayo hayo ya kikundi nilimchallenge yule dada Afisa Maendelo kuhusu kuruhusu mkopo wa mmoja...
Hakika serikali itakuwa imefanya Jambo la maana Sana na itakuwa imewasaidia vijana wengi Sana kuliko huu mfumo wa kulazimika kuwa na kikundi ndio mpatiwe mkopo
 
Mkopo mkopo wa nini we kijana

Pambana,hiyo mikopo haina msaada

Wowote bado

Ova
Ndio naendelea kupambana Sana tu, lakini walioweka mikopo Duniani kwote walikuwa na malengo mazuri tu ,ikiwa Ni pamoja na kuwasaidia watu kukuza mitaji yao au kupata mitaji kwa ajili ya kuanzisha shughuli za kiuchumi itakayo wasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na Hali ya umaskini wa kipato.
 
Ndugu zangu watanzania,

Mfumo uliopo kwa Sasa juu ya pesa za halmashauri zinazotolewa Kama mkopo kwa vijana kutokana na makusanyo na mapato ya ndani unataka vijana au akina mama au watu wenye ulemavu kuweza kujiunga au kuunda kikundi cha kijasiriamali ili kuweza kupatiwa mkopo, ambapo hapa kuna taratibu za kufuata ili kukidhi vigezo Kama vile kutengeneza katiba, kuwa na akaunti ya kikundi, viongozi wa kikundi, mradi au wazo la mradi au biashara na mengineyo.

Ndugu zangu katika utolewaji wa pesa hizi hazitoi fursa kwa mtu mmoja mmoja kupatiwa mkopo, ukiwa kijana pekee huwezi ukapata mikopo hii hata Kama Ni muaminifu,una wazo zuri la biashara au mradi au una mradi au biashara ambayo ungependa uongeze na kukuza mtaji wako.

Hali hii inawanyima fursa vijana wengine ambao wanaona katika vikundi Kuna kuwa na baadhi ya changamoto Kama vile uaminifu mdogo kwa baadhi ya wanakikundi,kutofautiana kwa malengo, matumizi mabaya ya Fedha, uzembe wa baadhi ya wanakikundi, wengine kuchukua hela na kuishia kugawana pasipo kutumia katika malengo husika.

Kutokuwa na Elimu ya kutosha juu ya mradi au biashara tarajiwa na hivyo kuishia kupoteza mtaji wote kabla hata ya kurejesha, Haraka ya baadhi ya Wana kikundi au vijana kutaka utajiri wa haraka haraka na hivyo kuwekeza katika maeneo hatari wasio na uzoefu nayo au ujuzi nao zaidi ya habari za kusikia tu juu ya faida kubwa watakayoipata.

Hivyo nilikuwa naona Ni wakati wa serikali ya Rais wetu mpendwa mama Samia kuangalia uwezekano wa kutoa fursa ya mkopo kwa mtu hata mmoja mwenye kuhitaji mkopo huu huku wenye kuungana na kuwa kikundi nao waendelee kupewa Kama kawaida,hii itarahisisha na kusaidia vijana wengi Sana kuweza kupata mikopo na kuwasaidia vijana wengine hata kimawazo na kiushauri.

Vigezo vinavyoweza kutumika ni Kama vile uwepo wa Taarifa za kutosha juu ya mwenendo wa kiuadilifu, kiweledi, kimaadili, kiutendaji, kiuaminifu na kitabia kutoka katika uongozi wa serikali za mitaa.

Uwepo wa mdhamini anayeaminika na mwenye makazi ya kudumu katika eneo analotokea na kuishi kijana anayehitaji mkopo, mdhamini akubali kuwajibika endapo mhusika au kijana ataamua kukimbia au kutoroka kabla ya kurejesha pesa halmashauri.

Mdhamini asaiini fomu maalumu mbele ya mwanasheria wa serikali na kula kiapo cha kuwajibika juu ya Deni la anaye mdhamini na kopi ya fomu hiyo ibaki halmashauri ,nyingine kwa mwanasheria,nyingine kwa serikali ya mtaa ,nyingine kwa anayechukua mkopo na nyingine abaki nayo mdhamini.

Mdhamini awe na Mali zisizo hamishika na zenye hati inayotambulika kisheria,mdhamini awe Ni mzazi wa mhusika au mtu mwingine yeyote mwenye Mali zisizo hamishika na makazi ya kudumu eneo husika,Mdhamini akitaka kumdhamini mtu zaidi ya mmoja aruhusiwe mpaka pale tu itakapothibitika kuwa Mali za mdhamini Zina thamani kubwa ukilinganisha na mikopo au fedha inayotaka kuchukuliwa.

Hili Jambo litasaidia halmashauri kupata marejesho ya mikopo yote inayotolewa kwa vijana lakini pia itawasaidia vijana wengi kupata mikopo kwa urahisi bila mlolongo wa kutafutana na hata kuwalazimisha wengine ili wajiunge kwenye vikundi kusudi kutimiza lengo la kupata mkopo ambapo mwisho wa siku Hawa walio lazimishwa au kupachikwa kwenye kikundi kuweza kusaidia kupata mkopo wanakuwa hawana ule moyo au ufanisi mzuri na uwajibikaji mzuri na wanakuwa hawana mchango wowote ule katika kukuza ,kulinda na kuendeleza mtaji.

Naiomba Sana serikali iliangalie hili kwa jicho la kipekee kabisa, maana unakuta mtu unalima lakini unakosa hela ya pembejeo hasa mbolea kwa kuwa unawaza ukitaka mkopo wa kupanua kilimo chako inahitaji uende kwenye kikundi ambacho unajikuta nacho kina malengo mengine kabisa Kama vile ufugaji wa kuku wa mayai au ng'ombe wa maziwa ambapo unaona wewe huwezi ukapata hata nafasi ya kwenda kukatia ng'ombe majani au kuwawekea maji kuku kwa kuwa wewe shughuli zako Ni shambani muda mwingi na ndio Jambo unalolipenda kuliko ufugaji wa kuku wa mayai au nyama au ng'ombe wa maziwa.

Unakuta kikundi kimeundwa na kuomba mkopo wa Jambo fulani lakini Wana kikundi kila mmoja ana malengo yake kichwani juu ya hela ikiwa mkononi mwao, hivyo kupelekea mradi uliolengwa kukosa nguvu ya pamoja ya wanakikundi.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627

njia pekee ya serikali kusaidia vijana ni kutunga sheria ambayo italazimisha kila after ten yrs, Rais anaemaliza muda wake anatoka na watu wake wote ambao alihudumu nao

anatoka na wabunge, mawaziri, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, wakurugenzi yan wote ili na vijana wapate hizo nafasi

kijana mwenye mastars ya kilimo au mathematics kumpa mkopo wa milion 2 tena kwenye vikundi na mlolongo mrefu hapana

vijana wanata nafasi hizo hizo zao coz kama elimu viongozi wengi wanazidiwa na hawa vijana wa mtaani
 
Back
Top Bottom