Tunaoishi mikoani wengi tunaishi kwenye vijiji maana mtaani unajulikana kila kitu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,652
44,973
Dar ndo mkoa wa kipekee unaishi na mtu nyumba moja ila mnakutana weekend tu maana kila mtu anatoka alfajiri anarudi usiku.

Ila mikoani huku unaishi na watu wanajua kila kitu kukuhusu mtaani kila kukikucha unakutana na maneno mapya mixer kusengenyana.inshort mikoani huku mitaani ni kama tuko vijijini tu maana kama huna moyo hukai kwa jinsi utavyochomwa na maneno ya kupakaziwa.

Maneno yako ya aina mbili yanaumiza kiasi cha kuweza kumuua mtu mfano matusi juu ya mtu fulani na kuna vilevile maneno mengine yanaweza kukuponyesha mfano maneno ya kutiwa moyo.
 
Wale Wenye Maisha Fulani yaliyopinda hawapendi kujulikana...!

Lkn wale Wenye Maisha yamenyooka huwa Hawana wasi wasi,popote ni Sawa wanaishi bila shida...!
 
mtu kujulikana ama kutojulikana ni vile umeamua kujiweka wala sio suala la dar wala mkoani

mimi niko mkoani ila kuna watu wanafahamu tu jina langu na hawanifahamu sura nani majirani zangu mie pia siwafahamu

shughuli kama sherehe, misiba ndio bado inatukutanisha watu wa mikoani maana hapo ukijitenga umekwishaaa watakuombea likufike baya wafurah
 
Inategemeana na ulivyojiweka na mazingira pia. Watu tupo mikoani na tunaishi uswahilini lakini hakuna mtu anafahamu hata jina wala kazi, kila siku wananiona kama ni mpya mtaa ninaoishi.
 
Hata Dar kama unaishi uswahilini mbona kuna umbea sana, In short wabongo wanapenda umbea umbea hadi kwenye mitandao ya kijamii kama Insta ni umbea kwa kwenda mbele
 
Back
Top Bottom