Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,507
Post yako ni too emotional hadi umeshindwa kutuambia Kikwete amefanya nini hata kimoja ashukuriwe, zaidi ya kusema alijipanga kuwa rais. Je, alijipanga kuwakejeri madaktari? alijipanga kuwanyamazisha wabunge? hebu tuambie alijipanga nini kuwa rais, kuinua uchumi?, maisha bora? au kupunguza mfumuko wa bei, alijipanga nini.Humjui Kikwete.
Laiti ungemjuwa usingeleta pumba ulizozileta.
Ni hotuba ipi aliyonung'umika kama utakavyo iwe?
Hotuba za Kikwete zote, ni fundisho kwa watu kama wewe wanaolalamika na kunung'unika kila siku lakini mnachonung'unika hakijulikani.
Hotuba aliyoongea na wazee kuhusu madaktari, licha ya kuwaelewesha kilichojiri, alitamba sana na hata kukejeli. Na mpaka leo tumeona madaktari ni kimya na wala hutowasikia tena wakilalamika. Huyo ndio JK.
Hotuba ya juzi umeona alivyowanyamazisha kwa kukurupuka na kudakia hoja kwa mafanikio ya jitihada zake.
Kikwete, hakupewa "favor" kuupata Urais kama ilivyokuwa kwa wote wa kabla yake. Kikwete alijuwa kabisa kuwa anataka awe Rais na alijipanga hivyo kwa miaka mingi sana na akaupata licha ya kuletewa mizengwe na Nyerere katika uhai wake.
Nakuona una haha kutafuta la kusema kuhusu Kikwete lakini ukweli ni kwamba hamumuwezi kabisa, kila afanyacho hufanya kwa maslahi ya wananchi na si ya kwake binafsi. Leo hii kikwete angekuwa na madudu japo asilimia 1 tu ya madudu ya Mkapa sijui kama angebaki kwenye Urais, maana mlivyomsakama si kidogo, lakini hamna zaidi ya kuzuwa tu na kutafuta kisichopo, mtatafuta sana lakini bure tu.
Humjui Kikwete, unamsikia tu na unamkisia, he is way too far ahead from your way of thinking. Wewe bado una fikra za kizamani sana, za wakati wa dhiki za chai kukorogwa kwa lawalawa badala ya sukari.
Mnajionea nafsi zenu wenyewe na ndio mpaka zinawafanya mnakuja kubwabwaja hapa hapa, ati "tunamuonea Kikwete", una ubavu upi wewe wa kumuonea Kikwete?
Humjui Kikwete1