Ushauri: Rais Mstaafu Kikwete, kwa hili la bandari unajiaibisha na kujivua nguo

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,201
3,322
Umofia kwenu.

Wanajamvi,

Nimesikiliza hotuba ya Rais wa awamu ya 4 Mh. Jakaya kikwete akikemea viongozi wa Dini kujihusisha na siasa.
Hotuba ya kikwete inakuja banda ya baraza la maaskofu katoliki Tanzania TEC kutoa waraka wa kupinga uuzwaji wa bandari.

Ni wazi Kikwete alikuja mbele kujibu ule waraka ili kutetea hii serikali iliyofitinika. Najua kikwete anapita Sana hapa jamvini. Nataka nimpe ushauri mdogo tu kuhusiana na hiki anachojaribu kufanya.

Kikwete lazima ajue kwamba, kwa miaka yake 10 ya uongozi wa Taifa letu ndiye rais aliyeboronga zaidi kuliko wote. Huyu ndiye kiongozi ambaye neno ufisadi lilishamiri zaidi kuliko wakati mwingine. Kinachomfanya kikwete mpaka apate nguvu ya kusimama jukwaani ni kiburi tu. Ukweli kikwete ndiye kiongozi anayechukiwa zaidi hapa nchini.

Namsihi Sana kikwete, akae kimyaa km alivyowahi kushauriwa na uv-ccm wakati wa utawala wa mwendazake. Kikwete asifikiri kwamba watanzania bado ni wajinga. Akumbuke kwamba kikwete ndiye kiongozi ambaye kwenye uchaguzi wa 2005 alibeba matumaini makubwa Sana ya watanzania. Lkn tofauti na matarajio ya wengi kikwete AKATUANGUSHA! mwaka 2010 tukamuonyesha Kama tunamchukia kwenye sanduku la kura. Isingekuwa bao la mkono kikwete angeishia awamu moja.

Kikwete km mstaafu aliyechangia kutuharibia hii nchi. Akae atulie alee wajukuu zake ili angalau ile heshima kidogo iliyobaki aibakize. Watanzania hawataki uuzwaji wa bandari. Kitendo cha kikwete kuja front kinathibitisha kwamba hili si jambo Jema hata kidogo.

Tunajua udhaifu wa awamu ya 6. Atuachie watanzania wenyewe tutapambana nao kwenye la bandari na rasirimali zingine za nchi yetu. Nawasilisha.
 
Kikwete hana moral authority ya kusimama na kuwashambulia maaskofu kufuatana na waraka waliotoa kwasababu Kikwete ndio mshauri mkuu wa Serikali ya Samia!! Unapozungumzia pararel government hapa nchini unamzungumzia Kikwete na genge lake!! Samia asingekuwa na ubavu wa kuingia ule Mkataba na DPWorld bila ushauri wa Kikwete na genge lake!! Kikwete ni genge moja na Kinana ambae ndio DALALI wa UAE hapa Tanzania; pia ndiye swahiba wa karibu wa Kikwete!

Kikwete is not the person to advise on the protection of our resources kwani huyu ndiye aliyeuza mbuga kule Serengeti kwa mmarekani na kuwauzia Wachina gesi yetu ambayo mpaka Sasa hatujaifaidi. Kikwete should shut his mouth na aendelee kula matunda ya ufisadi wake na HOME SHOPPING CENTRE/ GSM!
 
20230821_133253.jpg
 
Huyu mstaafu!
Ndie aliyeanzisha ufisadi mkubwa katika nchi hii enzi za utawala wake.
ESCROW,RICHMOND,MEREMETA,SYMBION,IPTL .hizi
Zote ni kashfa za enzi zake!

Sasa ameshikilia Remote bila aibu na anatupelekesha na DP-WORLD!
Hataki kuachia remote akiamini kuwa anao ubavu wa kutupelekesha kwa ushirika na "RA".
Fisadi kubuhu ambaye amerudi kwa kasi ya 5G kwenye awamu hii ya mteule wao maushungi!

Je!
Watanzania mnakubali hali hii mpaka lini?

Nchi inaelekea kugawanyishwa kwa makundi mawili yenye maslahi tofauti.

1-Wapinga mkataba mbovu wa DP-WORLD!
Ambao wana maslahi mapana ya upendo kwa nchi yetu Tanganyika.

2-Waliouleta mkataba baada ya kutundikwa picha zao ukutani huko Emirati.
Kwa maslahi mapana ya matumbo yao mapana yasiyotosheka.

Kama Rais mstaafu analipwa mshahara 80% ya Mshahara wa Rais aliyeko madarakani currently.
Pia anaruhusiwa kutibiwa katika hospitali za kimataifa huko ughaibuni.

Anao walinzi na madereva wa serikali muda wote wa maisha yake.
Huku pia akipewa mgao wa gari mpya kila baada ya miaka mitano.
Amejengewa nyumba ya kifahari na serikali.
Na bado anazo nyumba lukuki za serikali alizojimilikisha toka zile zilizokuwa za serikali.

Walizojiuzia kinyemela....
Yoote hiyo haridhiki nazo na bado anataka kuliyumbisha taifa kwa kutaka mali zaidi!
Sasa naanza kuwaelewa wale viongozi wa Mapinduzi wa Niger dhidi ya Rais bilionea muuza Nickel ...Boughum!

Mungu Inusuru Tanzania

Moderators....please msifanye yenu kuufuta uzi huu.
Ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu Tanzani.
Nawaomba sana ...sana..sana!
AHSANTENI na asubuhi njema.
Maana kwa sasa JF ndio media platform pekee tunayoitegemea.
Huko kwingine kwishney!
 
Hahaha

Nani tena au Komandoo wa Unguja?
Hapana tuwe wakweli wa nafsi zetu,soma andiko mkuu na utamuelewa kwa urahisi sana....

Rais mstaafu analipwa 80% ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani kwa muda wote.
Amejengewa nyumba ya kifahari na serikali jijini Dar es Salaam.
Amepewa ulinzi na serikali 7×4×12.
Anaruhusiwa kwenda kutibiwa ulaya!
Anapewa usafiri mpya na madereva muda wote wa uhai wake!
Hivi tamaa hizi nyingine zinatoka wapi?

Na kwa maslahi ya nani?
Hii inageuka kuwa tamaa ya laana!
 
Andiko liko wapi?
 
Acha uchochezi na punguza chuki kwa asiyefahamu hata uwepo wako.
 
Huyu mstaafu!
Ndie aliyeanzisha ufisadi mkubwa katika nchi hii enzi za utawala wake.
ESCROW,RICHMOND,MEREMETA,SYMBION,IPTL .hizi
Zote ni kashfa za enzi zake!

Sasa ameshikilia Remote bila aibu na anatupelekesha na DP-WORLD!
Hataki kuachia remote akiamini kuwa anao ubavu wa kutupelekesha kwa ushirika na "RA".
Fisadi kubuhu ambaye amerudi kwa kasi ya 5G kwenye awamu hii ya mteule wao maushungi!

Je!
Watanzania mnakubali hali hii mpaka lini?

Nchi inaelekea kugawanyishwa kwa makundi mawili yenye maslahi tofauti.

1-Wapinga mkataba mbovu wa DP-WORLD!
Ambao wana maslahi mapana ya upendo kwa nchi yetu Tanganyika.

2-Waliouleta mkataba baada ya kutundikwa picha zao ukutani huko Emirati.
Kwa maslahi mapana ya matumbo yao mapana yasiyotosheka.

Kama Rais mstaafu analipwa mshahara 80% ya Mshahara wa Rais aliyeko madarakani currently.
Pia anaruhusiwa kutibiwa katika hospitali za kimataifa huko ughaibuni.

Anao walinzi na madereva wa serikali muda wote wa maisha yake.
Huku pia akipewa mgao wa gari mpya kila baada ya miaka mitano.
Amejengewa nyumba ya kifahari na serikali.
Na bado anazo nyumba lukuki za serikali alizojimilikisha toka zile zilizokuwa za serikali.

Walizojiuzia kinyemela....
Yoote hiyo haridhiki nazo na bado anataka kuliyumbisha taifa kwa kutaka mali zaidi!
Sasa naanza kuwaelewa wale viongozi wa Mapinduzi wa Niger dhidi ya Rais bilionea muuza Nickel ...Boughum!

Mungu Inusuru Tanzania

Moderators....please msifanye yenu kuufuta uzi huu.
Ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu Tanzani.
Nawaomba sana ...sana..sana!
AHSANTENI na asubuhi njema.
Maana kwa sasa JF ndio media platform pekee tunayoitegemea.
Huko kwingine kwishney!
Ndiyo maana wamejiwekea kinga wasishitakiwe kwa maovu yao
 
Bahatati mbaya huyo mstaafu mwenye sifa mbovu hivyo ndio amegeuka mshauri wa taifa, kama sio hasara tumeipata hapo sijui ni kitu gani kingine..
Kikwete,
Ni mfano MBAYA kabla wa kuigwa.

Lakini kwa ujumla wake,
Viongozi wanaliingiza Nchi yetu ambao Ni WAISLAMU WOOTE Ni walafi Sana,Ufisadi wao Ni mkubwa Sana na Ni wao ndio wanauza ardhi yetu na kutoa Bandari bure kwa DP WORLD.

Na bado Baadhi masheikh wanatetei ushetani huu wa kutoa RASILIMALI zetu.
 
Back
Top Bottom