He has failed to kick the ball to the net...he himself is the 1st problem...he is very unbelievable with what he promises...ataahidije kupunguza mfumuko wa bei wakati ameshindwa kutimiza ahadi zake za uchaguzi? Is that practical? Ameahidi mishahara kupanda wakati serikali yake inaishi kwa vimikopo vya barclays na wengine? Ameshindwa kuchukua wajibu wake kama aliyeteua na kudai anasupport bunge? Is he really serious? Anaogopa kila mtu! Hana priorities! Amekuwa situational leader...kazi kuchekacheka tu na kutafuta misiba iliko. Ameamua kuplay uswahili wakati taifa linaangamia. Kweli watz tulijiwekea mzigo...na haki ya nani hatuna rais...subiri baraza atakaloteua, utachoka na roho yako!
PascoWahenga wanasema "Choose your love and love your choice" JK tulimchagua wenyenye na tutake tusitake ni lazima tumpende no matter what! kama ilivyo boga, penda na maua yake!. Tumpende rais wetu na madhaifu yake!.
Tumshukuru JK yote aliyolitendea taifa hili!. Mnaweza kukuta hata huu utendaji wake ni zawadi kitoka kwa Mungu ili Watanzania tuupate ukombozi wa kweli wa pili baada ya ule wa kutupatia uhuru!.
I Love Tanzania,
Mungu ibariki Tanzania!.
Pasco.
Hakika hapo ndio mimi binafsi nakili kuwa kasababisha watanzania wengi kufunguka na kuweza kutambua matatizo ya mfumo wao wa kitaifa,mkoa,wilaya,kata mpaka kijiji!!!Pengine kama kuna kitu ambacho bwana mkubwa Kikwete tutamkumbuka na kwa kweli kimetufikisha hapa pa kusema pasi na woga ni kukuza uhuru wa kujieleza...pamoja na kejeli zake pale awali kama vile kelele za mbu hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi, kwa kweli nafuu ipo kinyume na ilivyokuwa wakati wa Mr ANBEM co-founder(mh Mkapa ukipenda muite Mr Kiwira), Mzee Ruksa au Mwalimu.
Walau sasa tunaongea kwa uhuru mkubwa tu...kwa hili pongezi Rais wangu, mheshimiwa, Dk, Luteni Kanali Mstaafu J.M. Kikwete.
Nawasilisha.
Inabidi ianze kampeni ya kumpamba Rais wetu kwa maua na sifa; picha zake zibandikwe kila nyumba, magazeti yote yaanze kutangaza habari zake ili asijisikie mnyonge sana na kuwa hapendwi...
Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikwete kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?
Labda tujiulize swali la ugomvi zaidi - ni uongozi gani ambao Kikwete anapatia taifa kiasi kwamba anafanya mambo mengi mazuri lakini analaumiwa zaidi? Yaani, anafanya mambo ambayo anaamini ni makubwa lakini mbele ya wananchi yanaonekana kama 'hakunaga'?
Yawezekana, we are missing to recognize the genius in our midst? are we that blinded by whatever to the extent that we can not appreciate the work of superb and beloved leader? Ni matatizo ya sisi wananchi kutomtambua yeye au ni tatizo la yeye kutotambulika?
Mwanakijiji watanzania huwa tunasema chema chajiuza kibaya chajitembeza. Kama unakumbuka mwanzo ilkifika wakati hata kikwete mwenyewe aliona aibu. Kila gazeti lilikuwa linamsifia, wengine wakasema ametumwa na Mungu, wengine wakatoa sifa nyingi sana. Ni yeye aliyekuwa wa kwanza kukataa sifa, na alitoa mfano kutoka jimboni kwake Ukerewe wakati constituent mmoja aliyempa lift alipomwambia kuwa watu wanakupenda sana, akamuuliza wananipenda vipi wakati hawana maji, barabara mbaya etc etc?
Mwanakijiji angalia mwenyewe yanayotokea katika nchi yetu sasa. Kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiuslama kila kitu ovyo, hakuna kinachokwenda inavyotakiwa. Ni lipi unaweza kumsifu Kikwete and his administration? We are not blinded at all, and we do not need a college diploma to see the mess we are in. Nadhani washauri wake wako smart kutumia weaknesses zake kusmahuri kusafiri na kupata per diem nyingi sana.
Hotuba zake tatu za hivi karibuni zimejaa manung'uniko na malalamiko ya mtu ambaye haeleweki, hapendwi, hasifiwi au ambaye hashukuriwi. Hotuba yake kwa wazee wa CCM wa Dar-es-Salaam baada ya mgogoro wa madaktari na hotuba yake ya Mei Mosi mbele ya wafanyakazi kule Tanga zinatuonesha hisia za mtu ambaye wananchi wake inaonekana hawamshukuru vya kutosha.
Katika hotuba zote tatu Rais amejaribu kutuonesha ni jinsi gani amejitahidi kufanya mambo kadha wa kadha ambayo kwa kweli watu wangemshukuru kuwa ameyafanya lakini inaonekana hashukuriwi. Ni hotuba ambazo zimejaa "tenda wema nenda zako" nyingi. Madaktari hawamshukuru, wafanyakazi hawamshukuru, wapinzani hawamshukuru, na hata wana CCM wenzake yawezekana hawamshukuru. Lakini pia kwenye hotuba ile ya mambo ya nishati ambapo alisifia serikali yake kufanya mengi katika kuzalisha umeme nchini kuliko serikali zilizomtangulia nayo pia ilijaa kutokuwa appreciated.
Ndio sababu najiuliza ni kweli yawezekana Rais Kikwete anaona Watanzania hawamshukuru vya kutosha na kuappreciate vitu alivyovifanya? Ni kweli Kikwete amefanya makubwa sana ambayo anapaswa kushukuriwa kwayo? Ni kweli kwamba Watanzania wanambebesha lawama kwa kumuonea tu japo "amejitahidi" sana kufikia malengo mbalimbali kulinganisha na viongozi wengine waliomtangulia?
Kama ni kweli amefanya yote ambayo anadai amefanya ni kitu gani basi kinawafanya Watanzania wasiyaona mambo hayo na kumpatia pongezi zaidi kiasi kwamba badala ya kuongeza kura zake mwaka 2010 alizipunguzwa kwa asilimia 20 hivi? Kwamba pamoja na yote mazuri anajikuta anashinikizwa kuvunja baraza, utawala wake ukilaumiwa sana na wananchi wakiwa na kiu zaidi ya mabadiliko na uongozi. Tumeona juzi hata baadhi ya viongozi wa chama chake wakimuambia waziwazi kuwa "awe mkali kidogo".
Labda tujiulize swali la ugomvi zaidi - ni uongozi gani ambao Kikwete anapatia taifa kiasi kwamba anafanya mambo mengi mazuri lakini analaumiwa zaidi? Yaani, anafanya mambo ambayo anaamini ni makubwa lakini mbele ya wananchi yanaonekana kama 'hakunaga'?
Yawezekana, we are missing to recognize the genius in our midst? are we that blinded by whatever to the extent that we can not appreciate the work of superb and beloved leader? Ni matatizo ya sisi wananchi kutomtambua yeye au ni tatizo la yeye kutotambulika?
Jk ni mzee wa mipasho or malkia wa mipasho, sio kosa lake ni kosa la eneo analotoka ama kutokea ama kukulia ama hulka ya watu wa pwani kote ndivyo walivyo, mfano watu wa mombasa zanzibar lindi mtwara malindi pemba bagamoyo somalia nk. Wao siku zote wanajifanya wajuwaji kumbe hawajui chochote washabiki wa zuri sana lakini sio wachezaji wa zuqi,yuko uwanjani anacheza mpira timu yake imefungwa nae pia kashindwa kufunga goli la wazi kabisa, anaanza kulalamika ooo nataka mnishukuru nimekoa magoli mengi sana tulikuwa turudi na kikapu cha magoli! Upntezf point 3 za bure na za wazi kabisa uje utuambie umeokoa magoli mengi sana? Tunachotaka ni ushindi sio uokoaji wa magoli. Pwani pwaa!!!! Hakuna kitu humo.tunahitaji ushindi na sio kutaka shukrani zisizostahiki.