Humjui Kikwete1
Hotuba za Kikwete zote, ni fundisho kwa watu kama wewe wanaolalamika na kunung'unika kila siku lakini mnachonung'unika hakijulikani.
Hotuba aliyoongea na wazee kuhusu madaktari, licha ya kuwaelewesha kilichojiri, alitamba sana na hata kukejeli. Na mpaka leo tumeona madaktari ni kimya na wala hutowasikia tena wakilalamika. Huyo ndio JK.
Hotuba ya juzi umeona alivyowanyamazisha kwa kukurupuka na kudakia hoja kwa mafanikio ya jitihada zake.
Humjui Kikwete1
KIJANI: Pengine hatuna shukurani, lakini baadhi ya tunayoyanung'unikia ni:
1. Maisha bora kwa kila Mtanzania v/s
2. Mfumko wa bei wa kutisha
3. Giza totoro kila uchao
4. Madudu yake na ya watendaji wake (orodha kubwa)
5. Rais mtoro (Jenerali Ulimwengu).
6. Mawaziri na watendaji wa chini yao mapanya wanaokula noti (hili kalikubali hata yeye mwenyewe)...kwa kutaja machache tu.
BLUU:
Hizo ndio za Jamadari, Dk. Mheshimiwa Kikwete, kukejeli na kunyamazisha. La mwisho, "Ni upepo tu utapita".
NYEKUNDU:
Kweli hatumjui Dk. Kikwete. Kikwete huyu tuliyenaye sie yule tuliyemchagua kwa matumaini, aliyeahidi mambo lukuki akijua kuwa hayatekelezeki. Kulikuwa na haja gani ya kuweka ahadi 60 badala ya kushughulikia 4 za msingi:
1. Kuchagua watu watendaji na wajibikaji. 2. Mfumko wa bei 3. Umeme/Maji 4. Kuwawajibisha bila kuwaangalia usoni wa hapo nambari moja.
Lakini pengine Dk. Kikwete hakustahiki lawama zote kwani mambo TZ hayakuanza kuharibika leo, yalianza kuharibika tangu enzi za Nyerere. Kama alikuwa halijui hilo wakati anaingia madarakani, ninammuonea huruma. Na kama aliyajua, na alipaswa kuyajua, alikuwa na chaguzi mbili, ama anaingia madarakani kuyazuwia au asiingie kabisa. Uongozi si taasisi ya "trial and error", wananchi hawalifahamu hilo.
Licha ya kuwa TZ haikuanza kuoza leo, yaye ndiye
aliyekamatwa na ngozi. Kwa kuwa kajikubalisha jukumu awe tayari kupokea lawama zote. Watanzania tuna wajibu wa kumsaidia Dk. Kikwete, wakianza wale aliowachagua. Sasa ikiwa wengi aliowachagua, ambao walipaswa kuwa kigezo cha kumsaidia na sisi kuiga, lakini wamemwangusha na yeye anawachekea, anawalinda, anawaogopa...
- Toka ameingia madarakani, ni madudu mangapi yamefanywa na hatua gani amechukua zaidi ya kubadilisha wabovu na kuweka wabovu zaidi?
- Kongozi anapothubutu kusema "hatuwezi kuwashitaki wabadhirifu kwani uchumi utayumba" unataka tumuelwe vipi?
- Kiongozi baada ya dhoruba ya hivi karibuni, anathubutu kukejeli "Ni upepo tu utapita" tumwelewe vipi?
- Kiongozi "anapofurahishwa tu umakini na uwazi wa wabunge" bila ya kuchukua hatua muafaka tumwelewe vipi zaidi ya kuwa anataka kutupoza ili "upepo upite". Bado tuna wajibu gani wa kumsifu kimtindo wa
Zidumu Fikra za Mwenyekiti?
Nehi, nehi, nehi!!
Narudia kauli yako, ni kweli
Hatumjui Kikwete.