Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikwete kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?
Mzee Mwanakijiji, ni kweli wapo wengi wasio na shukrani kwa JK, watu ambao hawana hata chembe ya appreciation!. Wao wanaweka reference ya mabaya tuu!. This is not fair!.
Ila pia tupo wengi akina sisi wenye shukrani ambao tunashukuru kwa yote mazuri na mabaya!. Pamoja na mabaya yake, pamoja na udhaifu wake as a weak president, pamoja na kuwa kutokuwa na msimamo thabiti na kushindwa kufanya maamuzi magumu, bado tuna appreciate kwa mazuri machache aliyolifanyia taifa hili na ndio maana mpaka tumemuanzishia thread ya "Miongoni mwa Mazuri ya JK..." na mode akaona ni busara kupiga sticky ile thread.
Na nilipopandisha thread ya "Mabaya ya JK..." mode hawakuipiga sticky bali waliiacha ipotelee as result watu wanaendelea kuichafua ile thread ya " Mazuri ya JK kwa kuijaza mabaya!".
Niliwahi sema Watanzania ni watu wa kulalamika sana na jf ni cross section ya Watanzania hawa hawa kazi kulalamika tuu!. Malalamiko yakizidi yanageuka nagging! na kuzaa negativity ambayo ikizidi inaweza hata kugeuka ugonjwa!.
Nilitoa wito tupunguze kulalamika, tupunguze maneno meengi!. Tuondoke kwenye maneno maneno, twende kwenye matendo!. Tufanye maneno yawe mafupi na vitendo viwe virefu. Lets be positive kuhusu huyu mtu!, Hivyo ndivyo alivyo and he can't be the other way round!.
Nilisema huko nyuma na leo nasema tena na kesho na kesho kutwa nitaendelea kusema. Kikwete ndiye rais wetu tuliomchagua wenyewe kwa kura zetu!. Haijalishi ulipiga kura au hukupiga, haijalishi hukumpigia au ulimpigia as long as yeye sasa ni rais, anastahili heshima yake kama rais!.
JK ndiye rais wa Dr. Slaa, JK ndiye rais wa wanachadema wote!. Jk ndiye rais wa Lipumba, yeye ndiye rais wa wana CUF wote!. Infact yeye ndiye rais wa Wanzanzibari na Watanzania wote no matter wako wapi be it Tandahimba au New York!. Kwa hilo tuu, tumkubali tumkatae ndiye tunaye and that is a fact!.
Ingelikuwa tumemchagua bila kumfahamu vyema, kumlalamikia ingekuwa haki yetu and that would have justify kulalamika kwa sababu hatukujua!. Lakini wakati tunamchagua tulimjua fika inside out what he is, his capabilities and weaknesses na bado tulimchagua!. Hivyo kuendelea kumlalamikia sasa sasa sio kumtendea haki!. Wajameni tumtendee haki rais wetu!.
Wahenga wanasema "Choose your love and love your choice" JK tulimchagua wenyenye na tutake tusitake ni lazima tumpende no matter what! kama ilivyo boga, penda na maua yake!. Tumpende rais wetu na madhaifu yake!.
Sisi tusio na upande wowote tunapata wakati mgumu sana kusimama kwenye hard facts kwa sababu wengi wetu humu wameshachagua upande na wanafuata the American style " You are either with us, or against us". No standing on the fence!.
Binafsi naendelea kushikilia msimamo wangu kutofungamana na chama chochote, Chadema niliwaambia "hawajajipanga", "CCM imechokwa mpaka basi!" na "CUF inaelekea mkao wa kifo" Pamoja na misimamo hiyo nilitoa wito kwa Wana JF tuwe na shukrani katika madogo ili tuweze kupatiwa makubwa!.
Tumshukuru JK yote aliyolitendea taifa hili!. Mnaweza kukuta hata huu utendaji wake ni zawadi kitoka kwa Mungu ili Watanzania tuupate ukombozi wa kweli wa pili baada ya ule wa kutupatia uhuru!.
I Love Tanzania,
Mungu ibariki Tanzania!.
Pasco.