Tunamuonea Rais Kikwete?

Hivi mara ya mwisho inflation kuwa 20% ilikuwa lini? anybody...

Tatizo sio ilikuwa lini, tatizo unachukuwa advantage ipi kwa hiyo inflation kupanda? kama hujui mbinu na kuchukuwa advantage ya hilo, kaa kimya, wacha niuze mikaratusi yangu nje kwa haraka, kabla inflation haijashuka!
 
To some extent naona Kikwete ana suffer consequences za vitendo vyake. Mkapa alikuwa anahubiri ukweli na uwazi lakini hakukuwa na uwazi wowote. Leo Kikwete ameruhusu kila kitu kinarushwa hewani na wananchi ndio wanafungua macho kuona mautumbo ya serikali yao na kuona uongozi wote ni mbovu. Nadhani our next president atakuwa na tough choice ila most likely atakaa between Mkapa na Kikwete where uwazi utakuwepo though limited!
 
JK anajitahidi kuonyesha ni mtedaji kwa kulilia huruma ya wanatanzania , lakinin ana msogno mkubwa wa mawazo .. anaogopa kivuli chake , anahukumiwa na matendo yake na hata utawala wake umemshinda
 
Na tujiulize. Rais anashauri wa mtu kama wasira, kigoma malima, ngeleja au lukuvi, unategemea nini hapo? Akija kwenye chama anashauriwa na nape, mukama au chiligati unategemea nini hapo?
Kwa waTz, ili liwe funzo la milele, kukubali tena kuongozwa na mzalamo.
 
JK anajitahidi kuonyesha ni
mtedaji kwa kulilia huruma ya wanatanzania , lakinin ana msogno mkubwa
wa mawazo .. anaogopa kivuli chake , anahukumiwa na matendo yake na hata
utawala wake umemshinda

kweli. inaelekea anapata faraja akiwa nje ya nchi kuliko hapa. ndiyo maana anachukua kila fursa kwenda nje.
 
kwa mara tatu mfululizo katika hotuba zake huyu jamaa nimemsikia anasema '' uwekezaj unahitajika ili nchi iweze kuendelea maana wawekezaji wakija watu wengi wanapata ajira mfano watu wa kufungua vizibo, kusomba bia kwa mkokoten toka kwa agent hadi baa, wauza chips wanaongezeka,wachomba mbavu za mbuzi wanaongezeka na hta wale wanaookota chupa za majiwanaongezeka pia''.......mei mosi kayasema haya sasa mtu wa cheo cha rais anawaza kukuza uchumi wa nchi kwa watu wake kufanya kazi kama hizi anazozitaja?...ndio maana hakuna anaemshukuru maana work done= 0 kwa kila analofanya...

anadai serikali emeongeza kukusanya mapato wakti huo huo anazungumzia mabilion yalioibiwa na viongozi wake....halafu kitu kingine hiyo juzi kulikuwa na haja gani yeye kuanza kuanza kutoa ufafanuzi wa jinsi alivyoipa nguvu ofisi ya CAG na namna walivyoajili wafanyakazi? la msingi ilikuwa ni kusema hatua alizochukua ili kuwadhibiti wezi hawa na sio kuanza kutoa ufafanuzi...na hili nililiona hata wakati anaongea kuhusu mgomo wa madaktari....anatoa ufafnuzi badala ya kusema nini kifanyike
 
Labda tujiulize swali la ugomvi zaidi - ni uongozi gani ambao Kikwete anapatia taifa kiasi kwamba anafanya mambo mengi mazuri lakini analaumiwa zaidi?
anaruhusu kushangaa kwa wageni na wenyeji.
 
  1. Kwa mtizamo wangu ni mtu aliyelemewa na wasaidizi wazembe na waongo wanaomdanganya na wasiopendana wao kwa wao na ni wanafiki.
  2. Moyo wa kuwatumikia watanzania anao ila vikwazo ktk mfumo inaonekana vimemshinda haswa ukizingatia mavuguvugu mengi (mfano kipindi kile wanataka wamuondoe kwenye uenyekiti wa taifa wa CCM) mpaka sasa anaiogopa sana CCM!
  3. Uongozi wake unatia shaka.
  4. Machoni pa watanzania walio wanyonge anaonekana ni msaliti.
Mheshimiwa huyu alipanga kuingia Ikulu kama sifa, kiuhakika hakuwa na 'vision' au agenda kuwa anataka kulifanyia nini taifa akienda ikulu. Matokeo yake anfanya kazi kwa kufuata mongozo wa wanamtandao waliomwingiza madarakani! Kwakuwa waliomuingiza madarakani lengo lao lilikuwa kujilimbikizia ukwasi kwa njia yoyote, basi wanafanya hivyo bila wasiwasi kwani tayari wanaye mlinzi wa uhakika. Mfumo mbaya wa kuongoza nchi ameutayarisha Kikwete mwenyewe kwa kuwakumbatia wahuni wake! angalia nafasi mbalimbali za uteuzi alizozifanya uone kama kuna anayemudu nafasi hizo.
 
kweli. inaelekea anapata faraja akiwa nje ya nchi kuliko hapa. ndiyo maana anachukua kila fursa kwenda nje.

tatizo anakimbia tatizo kuliko kukabili tatizo mwisho anatengeneza tatizo kuliko utatuzi wa tatizo
 
hata sisi tunanung'ukina rais wetu hajatushukuru wananchi kwa kuendelea kuiacha picha iendelee kutuongoza.
 
Tatizo sio ilikuwa lini, tatizo unachukuwa advantage ipi kwa hiyo inflation kupanda? kama hujui mbinu na kuchukuwa advantage ya hilo, kaa kimya, wacha niuze mikaratusi yangu nje kwa haraka, kabla inflation haijashuka!
no wonder unadiriki kusema kikwete ni rais bora kuliko wote maana matatizo yaliyotokea kwa viongozi wa awamu zilizopita unaona ni matatizo lakini matatizo yanayotokea kwenye awamu ya kikwete unaona ni window of opportunity...!
 
  1. Kwa mtizamo wangu ni mtu aliyelemewa na wasaidizi wazembe na waongo wanaomdanganya na wasiopendana wao kwa wao na ni wanafiki.
  2. Moyo wa kuwatumikia watanzania anao ila vikwazo ktk mfumo inaonekana vimemshinda haswa ukizingatia mavuguvugu mengi (mfano kipindi kile wanataka wamuondoe kwenye uenyekiti wa taifa wa CCM) mpaka sasa anaiogopa sana CCM!
  3. Uongozi wake unatia shaka.
  4. Machoni pa watanzania walio wanyonge anaonekana ni msaliti.

Inawezekana wasaidizi wake ndo wanaomuangusha...sasa kwanini asiwawajibishe hao wasaidizi kwa kuteua watu wanaoweza kwenda sambamba na dhamira yake? Kinachotia shaka ni kuwa wengi wa wasaidizi wake hawana uwezo kiuongozi na wapo kwenye nafasi zao kirafiki zaidi kuliko kikazi. Na pengine wanajua hata wafanye nini hakuna atakayewagusa. Hapo ndipo watu wanapokasirika. Akitaka heshima, achague watu wanaojiheshimu na kuheshima dhana ya cheo ni dhamana.
 
Hivi mara ya mwisho inflation kuwa 20% ilikuwa lini? anybody...

Enzi za awamu ya pili wakati Kighoma Malima alipokuwa waziri wa fedha. Mkapa alijitahidi sana kudhibiti mfumuko wa bei tena kwa vitendo sio kwa hadithi hadithi. Ilikuwa unaweza kukaa hata miezi sita bila kuona mabadiliko makubwa ya bei za bidhaa madukani. Leo hii, kila kukicha afadhali ya jana.
 
He wanted the job. He campaigned for it. And he "got" it.

Blame and praise come with it.

He should just suck it up and let history and posterity be his judge.

Well said NN. Historia itampa nafasi anayostahili mbele ya safari tena bila upendeleo. Kila mtu anavuna anayopanda.
 
Hotuba zake tatu za hivi karibuni zimejaa manung'uniko na malalamiko ya mtu ambaye haeleweki, hapendwi, hasifiwi au ambaye hashukuriwi. Hotuba yake kwa wazee wa CCM wa Dar-es-Salaam baada ya mgogoro wa madaktari na hotuba yake ya Mei Mosi mbele ya wafanyakazi kule Tanga zinatuonesha hisia za mtu ambaye wananchi wake inaonekana hawamshukuru vya kutosha.

Observation yako ni nzuri sana, na inawezekana ikawa ni kweli kuwa JK akajiona kuwa anafanya mazuri mengi bila ya kusifiwa. Hili ni tatizo kubwa sana kwa taifa maana inamaanisha kuwa tunaongozwa na kipofu.

Ni kama vile mtoto wa miaka 5 anapotaka kusifiwa na mama yake kwa vile amemsaidia kusafisha chumba bila kujua kuwa alichofanya ni kusambaza tu uchafu. Very unfortunate that we'll have to keep on with this incompetent president for some years to come.
 
Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikwete kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?
Mkuu, naona umeamua kutukejeli au kumukejeli mhusika! mie nilidhani kwa mazingira ya chenji ya rada serikali ya huyu ustaadhi ilitakiwa iwashughurikie kikamilifu wahusika wa sakata zima na sio vinginevyo!
 
Sidhani kama ni wasaidizi wake ndio wazembe na waongo ila yeye ndio kiongozi wa uzembe na uongo. Kwa nguvu aliyopewa kikatiba hilo lisingekuwa ni kikwazo kwake, kwani angeweza kufanya lolote kwao kwa sababu yeye ndiye aliyewapa hicho kitumbua na angetaka kukichukua angeweza. Nionavyo mimi huyu jamaa tulimbebesha mzigo ambao hana uwezo nao!
 
Back
Top Bottom