Tunamuonea Rais Kikwete?

Tunamuonea Rais Kikwete?

Ukitaka kujua kwamba JK ni Rais wa namna gani, angalia alivyoshiriki msiba wa Kanumba.

Kwamba ameahirisha safari ili ashiriki. Pili katoa ubani milioni 10, tatu kawakumbusha wasanii kwamba ahadi yao anaikumbuka na hajaisahau anasubiri uongozi wa wasanii wafanyie kazi mambo fulani then wampelekee "ripoti".

Misiba mingapi inatokea na hatusikii akiahirisha safari ili ashiriki na badala yake anatuma wawakilishi? Je, kulikuwa na haja ya kusema hayo? Kulikuwa na haja ya kutangaza "ubani" ametoa kiasi gani na kukumbushia ahadi zake? Why asubiri kwenye msiba? Was that a right place ya kukumbushia hilo?

Hilo la kutoshukuriwa, anajitakia mwenyewe na mojawapo ya vitu vinavyomponza ni hilo hapo juu.
 
Jk ni mzee wa mipasho or malkia wa mipasho, sio kosa lake ni kosa la eneo analotoka ama kutokea ama kukulia ama hulka ya watu wa pwani kote ndivyo walivyo, mfano watu wa mombasa zanzibar lindi mtwara malindi pemba bagamoyo somalia nk. Wao siku zote wanajifanya wajuwaji kumbe hawajui chochote washabiki wa zuri sana lakini sio wachezaji wa zuqi,yuko uwanjani anacheza mpira timu yake imefungwa nae pia kashindwa kufunga goli la wazi kabisa, anaanza kulalamika ooo nataka mnishukuru nimekoa magoli mengi sana tulikuwa turudi na kikapu cha magoli! Upntezf point 3 za bure na za wazi kabisa uje utuambie umeokoa magoli mengi sana? Tunachotaka ni ushindi sio uokoaji wa magoli. Pwani pwaa!!!! Hakuna kitu humo.tunahitaji ushindi na sio kutaka shukrani zisizostahiki.
 
Ukweli wa mambo ni kuwa kawaida ya wananchi ni kulaumu pale serikali inapofanya makosa na si kazi yetu kusifia inapofanya vizuri kwa sababu kubwa moja, tulichagua serikali ili ifanye mazuri na si vinginevyo.

Shida ya Dk Kikwete na viongozi wengi wa ki-afrika(au dunia ya tatu?) ni kupenda kusifiwa kwa 'mazuri' waliyofanya na kukataa lawama kwa mabaya yao kwa kisingizio kuwa 'wameshauriwa vibaya na wasaidizi wao'. Sifa njema wapate wao lakini lawama wapate wasaidizi!!! Dk Kikwete ameangukia katika mtego huo kama wengi wengine kabla yake...Mh Mkapa, Shekhe Ali na Mwalimu Julius.

Katika mtego huo wamekataa kutambua na kukubali kuwa wao kama kichwa basi vyote lawama na sifa ni stahiki zao lakini wakipaswa kuzingatia kwamba kufanya uzuri ni wajibu usiohitaji sifa(isitoshe ni ahadi za kampeni zao siyo?) na upuuzi wao ni lazima uendane na lawama chungu tele.

Mfano wa uzembe na upuuzi wa kichwa ni pale kinapohitaji ushauri kutoka kwa kiganja ili kuufanya mwili utekeleze wajibu wake (soma: mkuu wa nchi kusubiri kamati kuu ya chama impe baraka za kuwashughulikia wezi na wabadhirifu wenye kujinasibu kuwa hawawajibiki kwa chama bali mkuu wa nchi kama mmoja wa watuhumiwa alivyonukuliwa na gazeti la mwananchi la jumatatu tarehe 30/04/2011).

Huo ni uzembe ambao hauwezi kusahaulika wala kusameheka na kwa kweli ni uzembe ambao umeigharimu sana serikali ya Dk Kikwete na hasa umaarufu wake binafsi na chama chake.

Pengine kama kuna kitu ambacho bwana mkubwa Kikwete tutamkumbuka na kwa kweli kimetufikisha hapa pa kusema pasi na woga ni kukuza uhuru wa kujieleza...pamoja na kejeli zake pale awali kama vile kelele za mbu hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi, kwa kweli nafuu ipo kinyume na ilivyokuwa wakati wa Mr ANBEM co-founder(mh Mkapa ukipenda muite Mr Kiwira), Mzee Ruksa au Mwalimu.

Walau sasa tunaongea kwa uhuru mkubwa tu...kwa hili pongezi Rais wangu, mheshimiwa, Dk, Luteni Kanali Mstaafu J.M. Kikwete.

Nawasilisha.

Uhuru wa vyombo vya habari ni swala ambalo hata mkapa lilishaanza kumshinda. Angejifanya jeuri kama Mkapa angejiharibia utukufu mwiiiingi aliokua nao kipindi kile. Na ukuzingatia uhuru wa kutoa maoni ni haki yetu, tumshukuru kwa kipi? Kama akiona ni zawadi basi azuie aone atakachokumbana nacho!
 
Tatizo moja la Kikwete ni kwamba mara nyingine anasahau kuwa yeye ndiye rais wa maamuzi na kujiona kama observer tu. Nakumbuka kuna wakati alisema asilimia 30% ya bajeti huishia mifukoni mwa watu. What did he do about it? Nothing. Halafu alipokuwa Davos akasema tatizo moja la uwekezaji ni kwamba mfumo wetu bila ya rais kuingilia kati hufiki popote. He is in a position do to something about it, but instead akawakaribisha wale waliokuwa wanamsikiliza pale Davos waje wamuone yeye ili mambo yao yaende sawa. Sasa which is which? Katika hili suala la mawaziri, kama kweli ni yeye alipendekeza ripoti ya CAG ijadiliwe bungeni, mbona hakuwachukulia hatua za mara moja mawaziri wake aliowateua mwenyewe? Kulikuwa na sababu gani za kuliweka taifa in suspense kama ilivyo sasa kuhusiana na kama mawaziri wanajiuzlu au hapana? Angefuta baraza la mawaziri mara moja Watanzania wangemuelewa, lakini hivi sasa inaonekana kuwa ni mchezo wa maigizo tu.
 
...Alidhani kuwa Rais ni lelemama atakenuakenua tu na kufanya uVDG miaka yake 10 ikatike halafu huyo anaenda kujidai na retirement fund yake nono...sasa Urais unamtokea puani....Baraza jipya la Mawaziri atatangaza lini? bado anamsubiri Migiro au wengi aliowagusa hawataki kuwa Mawaziri!?...Wiki inakatika sasa nchi haina baraza la mawaziri...nasema haina baraza la mawaziri kwa sababu hawa waliopo sidhani kama hata kama wanafanya kazi zozote kwa kuwa wako very anxious kujua bado wamo au wametemwa.
 
Humjui Kikwete.

Laiti ungemjuwa usingeleta pumba ulizozileta.

Ni hotuba ipi aliyonung'unika kama utakavyo iwe?

Hotuba za Kikwete zote, ni fundisho kwa watu kama wewe wanaolalamika na kunung'unika kila siku lakini mnachonung'unika hakijulikani.

Hotuba aliyoongea na wazee kuhusu madaktari, licha ya kuwaelewesha kilichojiri, alitamba sana na hata kukejeli. Na mpaka leo tumeona madaktari ni kimya na wala hutowasikia tena wakilalamika. Huyo ndio JMK.

Hotuba ya juzi umeona alivyowanyamazisha kwa kukurupuka na kudakia hoja kwa mafanikio ya jitihada zake.

Kikwete, hakupewa "favor" kuupata Urais kama ilivyokuwa kwa wote wa kabla yake. Kikwete alijuwa kabisa kuwa anataka awe Rais na alijipanga hivyo kwa miaka mingi sana na akaupata licha ya kuletewa mizengwe na Nyerere katika uhai wake.

Nakuona una haha kutafuta la kusema kuhusu Kikwete lakini ukweli ni kwamba hamumuwezi kabisa, kila afanyacho hufanya kwa maslahi ya wananchi na si ya kwake binafsi. Leo hii Kikwete angekuwa na madudu japo asilimia 1 tu ya madudu ya Mkapa sijui kama angebaki kwenye Urais, maana mlivyomsakama si kidogo, lakini hamna zaidi ya kuzuwa tu na kutafuta kisichopo, mtatafuta sana lakini bure tu.

Humjui Kikwete, unamsikia tu na unamkisia, he is way too far ahead from your way of thinking. Wewe bado una fikra za kizamani sana, za wakati wa dhiki za chai kukorogwa kwa lawalawa badala ya sukari.

Mnajionea nafsi zenu wenyewe na ndio mpaka zinawafanya mnakuja kubwabwaja hapa hapa, ati "tunamuonea Kikwete", una ubavu upi wewe wa kumuonea Kikwete?

Humjui Kikwete!
 
Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikwete kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?

wanasema huwezi kuuza samaki ukachukia shombo.... wacha tu anuke shombo
 
Humjui Kikwete.

Laiti ungemjuwa usingeleta pumba ulizozileta.

Ni hotuba ipi aliyonung'umika kama utakavyo iwe?

Hotuba za Kikwete zote, ni fundisho kwa watu kama wewe wanaolalamika na kunung'unika kila siku lakini mnachonung'unika hakijulikani.

Hotuba aliyoongea na wazee kuhusu madaktari, licha ya kuwaelewesha kilichojiri, alitamba sana na hata kukejeli. Na mpaka leo tumeona madaktari ni kimya na wala hutowasikia tena wakilalamika. Huyo ndio JK.

Hotuba ya juzi umeona alivyowanyamazisha kwa kukurupuka na kudakia hoja kwa mafanikio ya jitihada zake.

Kikwete, hakupewa "favor" kuupata Urais kama ilivyokuwa kwa wote wa kabla yake. Kikwete alijuwa kabisa kuwa anataka awe Rais na alijipanga hivyo kwa miaka mingi sana na akaupata licha ya kuletewa mizengwe na Nyerere katika uhai wake.

Nakuona una haha kutafuta la kusema kuhusu Kikwete lakini ukweli ni kwamba hamumuwezi kabisa, kila afanyacho hufanya kwa maslahi ya wananchi na si ya kwake binafsi. Leo hii kikwete angekuwa na madudu japo asilimia 1 tu ya madudu ya Mkapa sijui kama angebaki kwenye Urais, maana mlivyomsakama si kidogo, lakini hamna zaidi ya kuzuwa tu na kutafuta kisichopo, mtatafuta sana lakini bure tu.

Humjui Kikwete, unamsikia tu na unamkisia, he is way too far ahead from your way of thinking. Wewe bado una fikra za kizamani sana, za wakati wa dhiki za chai kukorogwa kwa lawalawa badala ya sukari.

Mnajionea nafsi zenu wenyewe na ndio mpaka zinawafanya mnakuja kubwabwaja hapa hapa, ati "tunamuonea Kikwete", una ubavu upi wewe wa kumuonea Kikwete?

Humjui Kikwete1

Hapo kwenye red hapo....
 
Mzee mwanakijiji naomba unisaidie kumfikishie ujumbe huu hapa chini.

Tutamshukuru kwa lipi wakati mfumko wa bei unazidi kupaa na mwanae ndo mdau wa kuhodhi bei za mafuta?
Tutamshukuru kwa lipi wakati wazi wazi watu wanatafuna nchi mchana peupe na yeye anakenua tu bila kuchukua hatua?
Tutamshukuru kwa lipi ili hali tangu ameingia madarakani sijaona anamwajibisha mtu?
Tutamshukuru vipi ili hali maendeleo na kasi tuliyokuwa nayo 2005 tumejikuta tumepiga hatua kurudi nyuma?
Tutamshukuru kwa lipi ili hali amejaza viongozi wabovu katika maeneo nyeti kwa uswahiba?

Mwisho naomba umuulize anataka tuje tumshukurie wapi Brazil,Marekani,Italy,Namibia,Malawi,Ethiopia,Sudan,Uk,France,Uswis,South Africa, atutajie tu kwamba watanzania tumfuate nchi gani tukampe shukrani zetu na machungu yetu ya moyoni.
 
He has failed to kick the ball to the net...he himself is the 1st problem...he is very unbelievable with what he promises...ataahidije kupunguza mfumuko wa bei wakati ameshindwa kutimiza ahadi zake za uchaguzi? Is that practical? Ameahidi mishahara kupanda wakati serikali yake inaishi kwa vimikopo vya barclays na wengine? Ameshindwa kuchukua wajibu wake kama aliyeteua na kudai anasupport bunge? Is he really serious? Anaogopa kila mtu! Hana priorities! Amekuwa situational leader...kazi kuchekacheka tu na kutafuta misiba iliko. Ameamua kuplay uswahili wakati taifa linaangamia. Kweli watz tulijiwekea mzigo...na haki ya nani hatuna rais...subiri baraza atakaloteua, utachoka na roho yako!

Tungetarajia nini kutoka kwa mpiga tumba kwenye ngoma ya kikwere?!

Napita tu, baadae
 
TatiZo ni kwamba aliamua
taasisi ya urais iwe mikononi mwa Familia yake,pia waliomzunguka
hawampi tathmini ya utawala wake,hiyo inamfanya akose kabisa uhakika na
akkifanyacho,naendelea tu kumpa moyo angalau ka muda alikobakiza
akatumie kuaga kila wilaya japo hata hajashukuru kwa kupewa kipindi cha
pili cha uongozi wake

uteuzi wa wasaidizi wake una mushkeli. anaweka wasaidizi wenye family ties na yeye. jairo anasemwa ni shemeji yake (dada ya mkewe wa kwanza). ndiyo maana inampa shida kuwawajibisha!
 
Wananchi siyo wajinga au wapungufu wa kuona mambo. Kwa bahati nzuri au mbaya Kikwete amechukua uongozi kukiwa na 'reference' hivyo ni rahisi sana kulinganishwa na waliopita.

1. Kikwete amechukua nchi ikiwa na 'template' ya kila jambo. Ameshindwa kujaza nyama katika mifupa 'skeleton'
Hapa ndipo kunakuja swali, hivi JK amefanya kitu gani kipya tofauti na watangulizi wake tukifahamu alilelewa katika mfumo anaouelewa vema.

2. Wananchi wanajiuliza alipochukua nchi 'inflation' ilikuwa 9% sasa ipo 20%! wanaopokea maumivu ni wananchi hao hao kulikoni?

3. Kikwete hajawahi kusimamia jambo lolote kama Rais. Amekuwa anakwenda na upepo ili kutoudhi au kufuhisha watu.
Hapa ndipo wananchi wanajiuliza kigeu geu 'flip flop' inasaidiaje taifa? Mfano, wakati analaani ufisadi, Kikwete hajasimama kwa vitendo kuonyesha anafanyia kazi maneno yake. Amekuwa kichaka cha mafisadi

4. Kikwete anaonekana kama 'msanii' na hajasimamia hoja zake kama mgombea au sera za chama
a: Aliahidi kurudisha nyumba za serikali, tumeona anajenga na hana uthubutu hata wa kuzungumzia hayo
b: Alisema atahakikisha waliohusika na kashfa ya rada wanafika mbele ya sheria. Hakuna lolote linaloendelea
c.Aliahidi kupambana na wauza dawa, majina yapo mezani kwake mwaka wa sita sasa
d. Akaahidi maisha bora, sasa ni bora maisha! umasikini umetamalaki kuliko huko nyuma. Inflation 20%
e: Akaahidi kushughulikia kero za muungano, sasa anazuia usijadiliwe

5: Kitendo chake cha kuruhusu washirika na maswahiba wapore rasilimali za nchi, wakombe kodi kwa wanaoishi kwa dola 1 kwasiku bila kuchukua hatua kinatia maudhi sana

Haya ni kwa uchache na mifano tu. Siyo kwamba wananchi wanamchukia bali hawana matumaini naye na hasira zao si kwa JK kama binadamu ni kwa Rais ambaye wataishi naye miaka 4 ijayo bila matumaini.
 
Hotuba zake tatu za hivi karibuni zimejaa manung'uniko na malalamiko ya mtu ambaye haeleweki, hapendwi, hasifiwi au ambaye hashukuriwi. Hotuba yake kwa wazee wa CCM wa Dar-es-Salaam baada ya mgogoro wa madaktari na hotuba yake ya Mei Mosi mbele ya wafanyakazi kule Tanga zinatuonesha hisia za mtu ambaye wananchi wake inaonekana hawamshukuru vya kutosha.

Katika hotuba zote tatu Rais amejaribu kutuonesha ni jinsi gani amejitahidi kufanya mambo kadha wa kadha ambayo kwa kweli watu wangemshukuru kuwa ameyafanya lakini inaonekana hashukuriwi. Ni hotuba ambazo zimejaa "tenda wema nenda zako" nyingi. Madaktari hawamshukuru, wafanyakazi hawamshukuru, wapinzani hawamshukuru, na hata wana CCM wenzake yawezekana hawamshukuru. Lakini pia kwenye hotuba ile ya mambo ya nishati ambapo alisifia serikali yake kufanya mengi katika kuzalisha umeme nchini kuliko serikali zilizomtangulia nayo pia ilijaa kutokuwa appreciated.

Ndio sababu najiuliza ni kweli yawezekana Rais Kikwete anaona Watanzania hawamshukuru vya kutosha na kuappreciate vitu alivyovifanya? Ni kweli Kikwete amefanya makubwa sana ambayo anapaswa kushukuriwa kwayo? Ni kweli kwamba Watanzania wanambebesha lawama kwa kumuonea tu japo "amejitahidi" sana kufikia malengo mbalimbali kulinganisha na viongozi wengine waliomtangulia?

Kama ni kweli amefanya yote ambayo anadai amefanya ni kitu gani basi kinawafanya Watanzania wasiyaona mambo hayo na kumpatia pongezi zaidi kiasi kwamba badala ya kuongeza kura zake mwaka 2010 alizipunguzwa kwa asilimia 20 hivi? Kwamba pamoja na yote mazuri anajikuta anashinikizwa kuvunja baraza, utawala wake ukilaumiwa sana na wananchi wakiwa na kiu zaidi ya mabadiliko na uongozi. Tumeona juzi hata baadhi ya viongozi wa chama chake wakimuambia waziwazi kuwa "awe mkali kidogo".

Labda tujiulize swali la ugomvi zaidi - ni uongozi gani ambao Kikwete anapatia taifa kiasi kwamba anafanya mambo mengi mazuri lakini analaumiwa zaidi? Yaani, anafanya mambo ambayo anaamini ni makubwa lakini mbele ya wananchi yanaonekana kama 'hakunaga'?

Yawezekana, we are missing to recognize the genius in our midst? are we that blinded by whatever to the extent that we can not appreciate the work of superb and beloved leader? Ni matatizo ya sisi wananchi kutomtambua yeye au ni tatizo la yeye kutotambulika?

Tutashukuru vipi wakati inflation ni double digit almost 20%?!
 
Mzee mwanakijiji naomba unisaidie kumfikishie ujumbe huu hapa chini.

Tutamshukuru kwa lipi wakati mfumko wa bei unazidi kupaa na mwanae ndo mdau wa kuhodhi bei za mafuta?

Uzushi huo, weka ushahidi wa kuwa mwanae ndiye mwenye "kuhodhi" bei za mafuta, na ukishindwa kuweka ushahidi basi jijuwe kuwa wewe ni mnafik.

Tutamshukuru kwa lipi wakati wazi wazi watu wanatafuna nchi mchana peupe na yeye anakenua tu bila kuchukua hatua?

Ingekuwa sio jithada zake binafsi ungeyajuwa hayo? unaonesha ni mwepesi wa kusahau kuwa kwa miaka 44 ya mwanzo toka tupate Uhuru hakuna uwazi kwa mahesabu ya Serikali kama ilivyo sasa. Au hulijui hilo? Fikiri!

Tutamshukuru kwa lipi ili hali tangu ameingia madarakani sijaona anamwajibisha mtu?

Una tatizo la kusahau, kama kuna wakati ambapo kuna kesi na mashtaka mengi zaidi ya rushwa na wizi wa mali za serikali basi ni huu wa Kikwete, tumeona vigogo vya mpingo vikifikishwa mahakamani, tumeona mpaka mawaziri wakisambatishwa, tumeona wabunge ambao ndio wawakilishi wako wakikemea na kuwawajibisha mawaziri, au yote hayo uliwahi kuyaona kabla ya awamu ya Kikwete? Fikiri!


Tutamshukuru vipi ili hali maendeleo na kasi tuliyokuwa nayo 2005 tumejikuta tumepiga hatua kurudi nyuma?

Weka ushahidi, maendelo ya Tanzania katika miaka 6 ya Kikwete ni zaidi ya maendeleo ya Rais wowote wa kabla yake, tena kwa ushahidi kabisa. Na hili utaumbuka vibaya sana, tuwekee maendeleo yako ya kabla ya 2005, kwenye chochote ukipendacho tukuoneshe ya leo yakoje halafu u "compare", Nakuhakikishia huna na huwezi kufanya hilo. Utajisuta, kama upo tayari kujisuta weka hapa!

Tutamshukuru kwa lipi ili hali amejaza viongozi wabovu katika maeneo nyeti kwa uswahiba?

Fikra za kijinga hizo, huoni vyama vinavyoweka viongozi kwa mapenzi na uhawara? mkwe, mchumba na mahawara? nakusikitikia sana kama hayo hujayaona!

Mwisho naomba umuulize anataka tuje tumshukurie wapi Brazil,Marekani,Italy,Namibia,Malawi,Ethiopia,Sudan,Uk,France,Uswis,South Africa, atutajie tu kwamba watanzania tumfuate nchi gani tukampe shukrani zetu na machungu yetu ya moyoni.

Alikwambia anataka shukurani yako? hafanyi kazi zake ili umshukuru, huo ni muono finyu kabisa na wala hayupo pale kwa kushukuriwa, umesahau kuwa yeye ni "chaguo la Mungu"?


Huyo uliemuomba akusaidie anashindwa hata kujisaidia mwenyewe, ataweza kukusaidia wewe? Fikiri!
 
Back
Top Bottom