Tunamuonea Rais Kikwete? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunamuonea Rais Kikwete?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 3, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Hotuba zake tatu za hivi karibuni zimejaa manung'uniko na malalamiko ya mtu ambaye haeleweki, hapendwi, hasifiwi au ambaye hashukuriwi. Hotuba yake kwa wazee wa CCM wa Dar-es-Salaam baada ya mgogoro wa madaktari na hotuba yake ya Mei Mosi mbele ya wafanyakazi kule Tanga zinatuonesha hisia za mtu ambaye wananchi wake inaonekana hawamshukuru vya kutosha.

  Katika hotuba zote tatu Rais amejaribu kutuonesha ni jinsi gani amejitahidi kufanya mambo kadha wa kadha ambayo kwa kweli watu wangemshukuru kuwa ameyafanya lakini inaonekana hashukuriwi. Ni hotuba ambazo zimejaa "tenda wema nenda zako" nyingi. Madaktari hawamshukuru, wafanyakazi hawamshukuru, wapinzani hawamshukuru, na hata wana CCM wenzake yawezekana hawamshukuru. Lakini pia kwenye hotuba ile ya mambo ya nishati ambapo alisifia serikali yake kufanya mengi katika kuzalisha umeme nchini kuliko serikali zilizomtangulia nayo pia ilijaa kutokuwa appreciated.

  Ndio sababu najiuliza ni kweli yawezekana Rais Kikwete anaona Watanzania hawamshukuru vya kutosha na kuappreciate vitu alivyovifanya? Ni kweli Kikwete amefanya makubwa sana ambayo anapaswa kushukuriwa kwayo? Ni kweli kwamba Watanzania wanambebesha lawama kwa kumuonea tu japo "amejitahidi" sana kufikia malengo mbalimbali kulinganisha na viongozi wengine waliomtangulia?

  Kama ni kweli amefanya yote ambayo anadai amefanya ni kitu gani basi kinawafanya Watanzania wasiyaona mambo hayo na kumpatia pongezi zaidi kiasi kwamba badala ya kuongeza kura zake mwaka 2010 alizipunguzwa kwa asilimia 20 hivi? Kwamba pamoja na yote mazuri anajikuta anashinikizwa kuvunja baraza, utawala wake ukilaumiwa sana na wananchi wakiwa na kiu zaidi ya mabadiliko na uongozi. Tumeona juzi hata baadhi ya viongozi wa chama chake wakimuambia waziwazi kuwa "awe mkali kidogo".

  Labda tujiulize swali la ugomvi zaidi - ni uongozi gani ambao Kikwete anapatia taifa kiasi kwamba anafanya mambo mengi mazuri lakini analaumiwa zaidi? Yaani, anafanya mambo ambayo anaamini ni makubwa lakini mbele ya wananchi yanaonekana kama 'hakunaga'?

  Yawezekana, we are missing to recognize the genius in our midst? are we that blinded by whatever to the extent that we can not appreciate the work of superb and beloved leader? Ni matatizo ya sisi wananchi kutomtambua yeye au ni tatizo la yeye kutotambulika?
   
 2. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  1. Kwa mtizamo wangu ni mtu aliyelemewa na wasaidizi wazembe na waongo wanaomdanganya na wasiopendana wao kwa wao na ni wanafiki.
  2. Moyo wa kuwatumikia watanzania anao ila vikwazo ktk mfumo inaonekana vimemshinda haswa ukizingatia mavuguvugu mengi (mfano kipindi kile wanataka wamuondoe kwenye uenyekiti wa taifa wa CCM) mpaka sasa anaiogopa sana CCM!
  3. Uongozi wake unatia shaka.
  4. Machoni pa watanzania walio wanyonge anaonekana ni msaliti.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Suppose anastahili shukurani na hashukuriwi.

  Yeye aligombea urais ili ashukuriwe?

  Siye Kikwete huyu huyu anayesema uongozi unataka ngozi nene?
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Kiukweli Kikwete na Watanzania wako 'dunia mbili' tofauti....
  ana haki ya kulalamika sometimes....kwa mfano
  Kikwete yeye siku zote huzungumza kuhusu Ilani ya uchaguzi ya CCM...

  wakati mahitaji ya sasa ya taifa ni zaidi ya Ilani ya uchaguzi wa CCM...
  watu walimchagua wakitaka awe 'transformational President'....yeye alidhani watu wamemchagua
  kwa Ilani ya CCM...

  tazama mfano Ilani ya CCM ya mwaka 2005 ilisema watengeneze ajira milioni moja

  wakati kila mtu anajua mahitaji ya ajira ni mara tano au zaidi ya ajira milioni moja....

  so watu hawatazama kama ajira milioni moja zilikuja or not
  watu wanatazama kuna ajira za kutosha or not... so yeye anashangaa mbona hawashukuru kwa ajira milioni moja
  while watu wanashangaa mbona ajira hakuna.....hapo ndo ilipo tofauti ya Kikwete na Watanzania...
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  He wanted the job. He campaigned for it. And he "got" it.

  Blame and praise come with it.

  He should just suck it up and let history and posterity be his judge.
   
 6. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mwanadamu wa kawaida hawezi kushukuru kama hakuna la kushukuru, ukiona hukushukuriwa ujue hakuna cha kushukuriwa na sio kuwa watu hawana shukurani hapana, ukweli ni kuwa kile wanachopata sio wanacho stahili.

  ...na kubwa zaidi ule wakati wa ndio mzee umepita... Uongozi ni kama mchezo wa soka ukifanya vizuri utapigiwa makofi, utashangiriwa na utashukuriwa na ukifanya vibaya washabiki watakugeukia na kukuzome.
   
 7. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tumshukuri kwa lipi, kwa kutuharibia uchumi, kujenga mtadao wa mafisadi, kulea wezi, kucheka cheka au lipi?
   
 8. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  He has failed to kick the ball to the net...he himself is the 1st problem...he is very unbelievable with what he promises...ataahidije kupunguza mfumuko wa bei wakati ameshindwa kutimiza ahadi zake za uchaguzi? Is that practical? Ameahidi mishahara kupanda wakati serikali yake inaishi kwa vimikopo vya barclays na wengine? Ameshindwa kuchukua wajibu wake kama aliyeteua na kudai anasupport bunge? Is he really serious? Anaogopa kila mtu! Hana priorities! Amekuwa situational leader...kazi kuchekacheka tu na kutafuta misiba iliko. Ameamua kuplay uswahili wakati taifa linaangamia. Kweli watz tulijiwekea mzigo...na haki ya nani hatuna rais...subiri baraza atakaloteua, utachoka na roho yako!
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,386
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  Angeweka takwimu badala kuhitaji kushukuliwa bila data... KWA MFANO.. 1. Aliahidi ajira 1M, angesema ajira zimepatikana ngapi na zimechukuliwa na nani. 2. Wakati wa kampeni alitoa ahadi nyingi, angesema katika hizo ngapi zimetekelezwa na ngapi bado na kwa nini bado.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Hayo yanaweza kusemwa kuhusu maraisi wetu wote waliopita!

  Hatujawahi hata wakati mmoja kuwa na neema.
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji watanzania huwa tunasema chema chajiuza kibaya chajitembeza. Kama unakumbuka mwanzo ilkifika wakati hata kikwete mwenyewe aliona aibu. Kila gazeti lilikuwa linamsifia, wengine wakasema ametumwa na Mungu, wengine wakatoa sifa nyingi sana. Ni yeye aliyekuwa wa kwanza kukataa sifa, na alitoa mfano kutoka jimboni kwake Ukerewe wakati constituent mmoja aliyempa lift alipomwambia kuwa watu wanakupenda sana, akamuuliza wananipenda vipi wakati hawana maji, barabara mbaya etc etc?

  Mwanakijiji angalia mwenyewe yanayotokea katika nchi yetu sasa. Kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiuslama kila kitu ovyo, hakuna kinachokwenda inavyotakiwa. Ni lipi unaweza kumsifu Kikwete and his administration? We are not blinded at all, and we do not need a college diploma to see the mess we are in. Nadhani washauri wake wako smart kutumia weaknesses zake kusmahuri kusafiri na kupata per diem nyingi sana.
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  not even Nyerere?????
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Ni wazi Nyerere huwezi kumlinganisha na Kikwete katika umakini.

  Lakini pia wakati wa Nyerere tulikuwa na neema?
   
 14. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,715
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  Ukweli wa mambo ni kuwa kawaida ya wananchi ni kulaumu pale serikali inapofanya makosa na si kazi yetu kusifia inapofanya vizuri kwa sababu kubwa moja, tulichagua serikali ili ifanye mazuri na si vinginevyo.

  Shida ya Dk Kikwete na viongozi wengi wa ki-afrika(au dunia ya tatu?) ni kupenda kusifiwa kwa 'mazuri' waliyofanya na kukataa lawama kwa mabaya yao kwa kisingizio kuwa 'wameshauriwa vibaya na wasaidizi wao'. Sifa njema wapate wao lakini lawama wapate wasaidizi!!! Dk Kikwete ameangukia katika mtego huo kama wengi wengine kabla yake...Mh Mkapa, Shekhe Ali na Mwalimu Julius.

  Katika mtego huo wamekataa kutambua na kukubali kuwa wao kama kichwa basi vyote lawama na sifa ni stahiki zao lakini wakipaswa kuzingatia kwamba kufanya uzuri ni wajibu usiohitaji sifa(isitoshe ni ahadi za kampeni zao siyo?) na upuuzi wao ni lazima uendane na lawama chungu tele.

  Mfano wa uzembe na upuuzi wa kichwa ni pale kinapohitaji ushauri kutoka kwa kiganja ili kuufanya mwili utekeleze wajibu wake (soma: mkuu wa nchi kusubiri kamati kuu ya chama impe baraka za kuwashughulikia wezi na wabadhirifu wenye kujinasibu kuwa hawawajibiki kwa chama bali mkuu wa nchi kama mmoja wa watuhumiwa alivyonukuliwa na gazeti la mwananchi la jumatatu tarehe 30/04/2011).

  Huo ni uzembe ambao hauwezi kusahaulika wala kusameheka na kwa kweli ni uzembe ambao umeigharimu sana serikali ya Dk Kikwete na hasa umaarufu wake binafsi na chama chake.

  Pengine kama kuna kitu ambacho bwana mkubwa Kikwete tutamkumbuka na kwa kweli kimetufikisha hapa pa kusema pasi na woga ni kukuza uhuru wa kujieleza...pamoja na kejeli zake pale awali kama vile kelele za mbu hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi, kwa kweli nafuu ipo kinyume na ilivyokuwa wakati wa Mr ANBEM co-founder(mh Mkapa ukipenda muite Mr Kiwira), Mzee Ruksa au Mwalimu.

  Walau sasa tunaongea kwa uhuru mkubwa tu...kwa hili pongezi Rais wangu, mheshimiwa, Dk, Luteni Kanali Mstaafu J.M. Kikwete.

  Nawasilisha.
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  JK aliutaka urais kwa udi na uvumba toka 1995, alikuwa na too much expectations lakini hakujua uzito wa kazi yenyewe. Amejikikuta kabakiza muda mchache wakati hajatimiza ndoto zake. Anajitahidi kwa kadri ya uwezo wake akitegemea appreciation lakini instead wenzake wanamvunja moyo hadi kutaka kumvua uenyekiti wa chama na juzi tena wabunge wa chama chake wanataka kumpigia vote of no confidence. Of cource hata ingekuwa wewe lazima ujisikie mnyonge.

  Sioni kama ana enjoy urais wake kama Mkapa kwa sababu ya mashinikizo refer Jairo case, mawaziri nk. Anahofu na chama chake hana imani nacho ndio maana sometimes anatafuta sympathy toka vyama vya upinzani.
   
 16. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  That is a fact, but we have never been in a situation where we see ourselves as hopeless and useless people than never before. Other administrations were a bit more serious, they showed that they were doing something, not now. The current administration is just sitting back a sipping a pint.
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I think "Just Kidding" - JK, is lost... he doesnt know where he is, what is doing and what is expected of him

  Hatumwonei
   
 18. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  TatiZo ni kwamba aliamua taasisi ya urais iwe mikononi mwa Familia yake,pia waliomzunguka hawampi tathmini ya utawala wake,hiyo inamfanya akose kabisa uhakika na akkifanyacho,naendelea tu kumpa moyo angalau ka muda alikobakiza akatumie kuaga kila wilaya japo hata hajashukuru kwa kupewa kipindi cha pili cha uongozi wake
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikwete kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?
   
 20. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,160
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji na Wana JF,
  Tatizo kubwa naona lipo kwa Kikwete mwenyewe na Team yake nzima.
  Hapa kuna mawili, moja unaweza washauri na wasidizi wake wanamshauri vibaya na yeye anasikiliza na kufuata ushauri wao, mfano halisi alishawahi kusema kuhusu katiba "wenzangu wangenielewa vibaya". Na la pili ni anashauriwa vizuri na washauri na wasaidizi wake ila yeye anawapuuza.
  Na siku zote binadamu ushukuru kwa jambo alilotendewa, kwa hali ya sasa ya Nchi utashukuru kwa nini ?? Hali ngumu ya maisha, mfumuko wa bidhaa, umeme, afya, yaani kila mahali ukigusa balaa.
  Ushauri wangu kwake awe mtu wa Vitendo kuliko kulalamika, awape Watanzania Matumaini bado hajachelewa sana kurudisha Imani kwa Wananchi akifanya Maamuzi Magumu kwa Ustawi wa Nchi.
  Nawakilisha


   
Loading...