"Tunahitaji viongozi majasiri" - Dr. Salim on KLH News

FMES, aliyoyasema is a classic.. nipo hapa I'm trying to transcribe ili yachapwe nyumbani, ila unaweza kuyasikia tayari yako kwenye KLH News..
 
si unajua tena...nawashukuru kwa kutusikiliza...

Mwanakijiji!
Hongera Sana !Yaani umekomaa sasa,Nimeyasikiliza kwa kweli umeuliza vizuri na umeonyesha ukomavu wa hali ya juu.Naomba siku moja utuweke yale mahojiano yako ya awali wakati unafungua kijiji cha ujamaa!
Mgeni wako naye amejibu vizuri na Hakuna ukada hata kidogo ni ufasaha na umakini!
Ninampongeza na mwenza wako Mr GEEQUE!Hongereni Aluta Continua!
 
Niseme hivi, tulikuwa tumekubaliana tangu Ijumaa, Jumapili ile miye nimeenda kwenye nyumba ya ibada hadi kama saa saba hivi. Nilitakiwa nithibitishe naye saa saba ile na nikakuta bado yuko ofisini na nikamwomba radhi kwa kuchelewa na nilikuwa umbali na kibandani kwangu kwa karibu saa moja, nikamwomba tusogeze mbele kwa saa nzima (badala ya kuanza saa nane tuanze saa tisa - saa nne ya nyumbani) na akakubali.

Na tulipoanza kuzungumza mwanzoni nilidhani atanipa dakika kama kumi hivi za haraka haraka, lakini alinipa almost an hour ya mazungumzo hadi nilipoamua mimi mwenyewe kukatisha maana nilianza kutamanani kwenda kwenye mambo mengine ambayo hakuwa tayari kuyazungumzia siku ile.

Hivyo, binafsi namshukuru sana kwa heshima hiyo, na kwa namna ya pekee bwana Geeque kwani mahojiano haya kwa mara ya kwanza tumeyafanya yeye akiwa nje kabisa ya Chi-Town na akawaweza kuunganisha kutoka hapa Motor City, next time nataka tuone kama tunaweza kupokea phone calls wakati tunazungumza hewani na mgeni ili watu waweze kumuuliza maswali yoyote yale.. (within reason of course)..
 
Mahojiano yangu na Dr. Slaa yanatarajiwa kutolewa katika mojawapo ya magazeti ya Nyumbani hapo kesho... nadhani itakuwa kwenye Kulikoni.
 
Mwanakijiji,
ingekuwa vizuri kama "UWIGO" wa mijadala kuhusu Mwalimu ungeongezwa, na kuchunguza kwa nini aliiacha nchi ikiwa hoi bin taabani.

hili somo la mazuri ya Baba wa Taifa nadhani linaeleweka vizuri tu kwa watanzania wengi. Kisichoeleweka ni nini kilichojiri mpaka Mwalimu akaporomosha Uchumi wakati tulikuwa tukipokea misaada lukuki?

Mwalimu aliwahi kuulizwa swali hilo na watu wa IMF/WB lakini akahamaki na kuwapa majibu yasiyostahili. Majibu ya Mwalimu yalijikita zaidi kuonyesha kwamba IMF/WB wamefeli zaidi kuliko yeye(Mwalimu).

Mimi nafikiri wakati nchi inasonga mbele kuna umuhimu wa ku-revisit our past na kuyabeba yale mazuri huku tukiacha yale mabaya. Naamini ni vizuri tukafanya hivyo ili kuepusha kurudia makosa, na vilevile kuboresha yale mema yaliyokwisha fanyika.
 
JokaKuu, majibu ya kwanini uchumi uliporomoka yapo na yameshatolewa mara nyingi, na mwalimu hakuwahi kuwa na illusion kuwa amefanya vizuri zaidi kama alivyotaka kufanya. Ukitaka kuangalia vizuri pitia maandishi yake ya "Miaka Kumi baada ya Uhuru - Vitu tunavyopasa kurekebisha".

la kwanza, ni kuwa baadhi ya sera alizoziona zinafaa kinadharia hazikuwa zinafaa kihalisia. Na hilo aliisha lijibu vizuri kwenye mahojiano na Charlayne Huntur-Gault na unaweza kusoma HAPA Hivyo, suala la sera kutotekelezeka lilikuwa ni kubwa mno sera kama ya "Ujamaa Vijijini" ingawa kinadharia ilionekana ni jambo zuri lakini kivitendo lilishindikana sana, lakini hata hivyo leo hii bado Vijijini vimekuwa ni msingi wa huduma nyingi sana na ndiyo msingi wa nchi yetu.

Matatizo ya Kiuchumi ya mwaka 1970 na ukame wa mwaka 1974, kwa wale wanaojua historia vizuri wanafahamu ni jinsi gani matatizo ya OPEC wakati ule yalitishia kuporomosha uchumi wa nchi nyingi hata ambazo Mwalimu hakuwa Rais wao! Nchi ambazo zilikuwa na vyama vingi na sera za kibepari kama Zaire na Kenya hazikufanya zaidi ya Tanzania!

Zaidi ya yote kabla hatujamaliza lile, tunaingia kwenye Vita iliyotuchukua karibu miaka mitatu kuhakikisha kuna amani kaskazi mwetu, tukumbuke kuwa vita ile tulipagana kwa nguvu zetu zaidi kuliko misaada ya wakubwa ambayo tungeweza kupatiwa. Lile peke yake lilivunja sana uwezo wetu wa kiuchumi. Tafuta historia ujue vita ile ilitugharimu kiasi gani kushinda! Kupeleka askari karibu 20,000 kwa karibu mwaka mzima na baadaye kuhakikisha amani inatawala si mchezo!!

Na kabla hatujapumua vizuri, ukame wa mwanzoni mwa miaka ya themanini ambapo watu tulishindia Yanga, na mambo ya kadi za Duka kwenda kununua vitu kwa ratio!! Na wakati ule ukatumika kuingiza rushwa kwa nguvu kwa mara ya kwanza nchini.

Ni kutokana na busara zake ndio maana hali ilipotulia kidogo aliamua kung'atuka kwani alijua kama mwanadamu alichoweza kufanya amefanya. Na akaamua kuwaachia wengine.

Sasa kuweka lawama zote juu ya Mwalimu ni kutokuwa wa kweli kwani kuna mambo mengine ambayo hata Malaika angeshindwa kuyatatua kwani yalikuwa ni nje sana ya uwezo wake! Ni kweli lawama zinazomwangukia Mwalimu ni zile za Kiongozi kwamba kama kiongozi alifeli mahali fulani na yeye mwenyewe alilijua hilo na alilikiri hadharani.

Lakini kuna jambo jingine la ziada. Mwalimua lipochukua nchi mwaka 1961 alikuwa na mfano gani wa nchi ya kiafrika ambayo imefanya vizuri chini ya uongozi wa Waafrika wenyewe? None. George Washington baba wa Taifa la Wamarekani hakuwaiinua Marekani kuwa nchi kama Uingereza au Ufaransa wa wakati ule, aliweka misingi! The same thing applied to other presidents followed after him. Na kwa miaka mingi wakipozekana Urais vitu kama Utumwa na Ubaguzi wa Rangi vilikuwa vinaendelea kama kawaida wakati Azimio lao la Uhuru linasema watu wote wako sawa!

Hivyo, unapomuangalia Mwalimu usimwangalia kwa kutumia kioo cha "mbona hali ilikuwa mbaya sana wakati wa Mwalimu" na badala yake tumia kioo cha "kwenye hali mbaya wakati wa Mwalimu alifanya kila alichoweza?". Ujiulize wakati wa Kupanda kwa Bei ya Mafuta mwaka 1970 (miaka tisa tu baada ya Uhuru) Mwalimu alikuwa na uwezo wa kupunguza bei hiyo?; Je, Wakati wa ukame wa 1974 Mwalimu alifanya kila alichoweza kuhakikisha Watanzania kwa mamilioni hawafi kwa njaa (japo wengine waliishia kula nzige?); Je alitumia uwezo wake wote kuhakikisha kuwa vita dhidi ya Nduli inapiganwa kwa haraka, kwa nguzu zote na kuhakikisha ushindi?; Na ukame wa mwanzoni mwa miaka ya themanini, Mwalimu alihakikisha hatufi na njaa?

Ukipata majibu ya maswali hayo utaona kuwa tulifanya vizuri sana chini ya Mwalimu kuliko Wakongo waliokuwa chini ya Mabotu! And I'm still glad and proud that at those crucial times of our history Mwalimu was THE PRESIDENT. Do you agree?
 
Mahojiano ya Dr Salim yametoka katika gazeti la Kulikoni la leo, ukurasa wa kwanza na kurasa tatu za ndani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom