"Tunahitaji viongozi majasiri" - Dr. Salim on KLH News

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,694
40,720
Siku ya Jumapili tutakuwa na onesho maalum la kumkumbuka na kumuenzi Baba Taifa. Natarajia kuanza kwenye saa saba za mchana hivi na nimewapangia ugeni mkubwa ambao nina uhakika mngependa kusikia kutoka kwake. Itakuwa ni sawa na saa mbili na saa tatu za EAT, na kwa wale wengine ni -5 GMT
 
my dear Mwafrika.. nitajaribu ila huyo ndugu nikianza kutaja vyeo vyake vyote.. tunaweza tukajikuta tumeishiwa muda.. !
 
Mwafrika wa kike,

Ulifunga wewe? Maana unatuchokoza watu ili mpaka tuseme.

Sawa, weekend njema, ila isiwe mwisho wa mfungo ndio mwanzo wa vurugu kuanzia ulevi wa aina zote mpaka kuendesha hovyo magari.

Mtanzania,

Kusema ukweli sikufunga....... ingawa nilialikwa futari multiple times na wafanyakazi wenzangu hapa toka India..... ambao kwao pia Eid ni leo kwa hiyo kuna very long weekend ya kusherehekea.

Weekend njema nawe pia.....
 
Siku ya Jumapili tutakuwa na onesho maalum la kumkumbuka na kumuenzi Baba Taifa. Natarajia kuanza kwenye saa saba za mchana hivi na nimewapangia ugeni mkubwa ambao nina uhakika mngependa kusikia kutoka kwake. Itakuwa ni sawa na saa mbili na saa tatu za EAT, na kwa wale wengine ni -5 GMT

Mwakjj.

Ushauri tu, mara nyingi wageni wako hawa wanakuwa ni viongozi wakubwa serikali kutoka vyama vya upinzani. Tunafurahia kuwa na watu wa aina hii ktk mahojiano nao ktk kujua mustakbal wa nchi yetu.

Kumezuka mtindo wa baadhi ya wachangiaji kufurumusha kashfa kwa viongozi hawa na kuwaita majinaya kebehi, dharau, na kejeri. Nadhani hii sio nzuri na sio utamaduni wetu na nadhani pia itawafanya wengine waone kama kuja kwao hapa ndio kumefungulia milango ya matusi kwao.

Naomba nieleweka sisemi na wala sishauri kuwa wasibanwe kwa matendo yao na kama ni criticism basi ziwe ni constructive crticism sio mambo majina kama Kara-mavi, Kara-bangi, selfish katibu etc nadhani huk ni kupotoka.

Yawezekana kabisa wakawa sio wasafi lakini kitendo cha kubadili jina la kiongozi lisomeke ndivyo sivyo sidhani kama kunatusaidia sana hapa bali kama sio kutoshusha hadhi yetu na kuonekana ni genge la wahuni.

Ombi langu kwako ni jaribu kuwaomba wasikiliza wako wajiheshimu kwa hilo.

Naomba kuwasilisha
 
Masatu, tabia hiyo hata mimi sipendi lakini kupachika viongozi majina ya utani au kebehi as long as siyo ya matusi ni sehemu moja ya gharama ya kuwa kiongozi. Mwalimu alijua hilo.. na kuna wakati alikiri kwa kusema "Mara ya Kwanza waliniita Musa, Halafu wakaniita Mchonga, siku hizi wananiita Haambiliki"... Hivyo majina kama "Muungwana" au "Msanii" n.k ni sehemu ya gharama ambayo viongozi wanalipa.

That said, binafsi situmii majina yoyote zaidi ya majina yao na siungi mkono kuwatungia majina ya matusi kwani that is counterproductive na kama tunataka kuwa mahali pa kuchukuliwa kwa umakini basi kuna vitu kila mmoja kwa makusudi kuviachialia. Uzuri mmoja wa JF ni kuwa standard yetu ya ushiriki siyo sawa na TV au magazeti.

Kwa upande wangu kwenye eneo langu la "Comments" kule KLH News.. naruhusu ukosoaji wa aina yoyote wa viongozi bila kutumia matusi na hata kama mtu ana point nzuri kiasi gani akianza kutumia matusi ninafuta posting hizo!
 
Mwkjj

Nakubaliana na wewe kuwa viongozi kupewa majina ya bandia ni gharama ya ushiriki wao kisiasa na mfano ulio utoa wa Mwalimu Nyerere unajitosheleza kabisa.

Kimsingi majina ninayozungumzia mimi ni yenye kashfa ndani sidhani kumwita mtu Kara-mavi inaweza kuwa justified kwa namna yeyote ile.

Lakini kubwa zaidi wasiwasi wangu ni kuwa kwa namna fulani hawa watu tunawataka waje kwa wingi kushiriki ktk vipindi vyetu sasa mambo ya kashfa yanaweza kuwa put off au scare them off kuja ambapo kwa maoni yangu loosers tunakuwa ni sisi.
 
Kama ni watu makini hawataogopa majina wanayoitwa na wachangiaji wa pembeni tu... wao wanaitwa na mkjj na as long as mkjj hana hayo majina... wao wanaweza kuja tu na wasitoe visingizio kuwa membaz wa JF wanawaita majina...

Kwani huyo Karamavi mbona hajasema hivyo? yeye mwenyewe kwanza anapenda jina la Karamavi
 
Masatu katika hili nakubaliana na wewe! Hoja haiwi na nguvu zaidi kwa sababu mtu anatumia matusi! na wakati mwingine hoja yenye nguzu inapunguzwa nguvu hiyo mtu akiona matusi!! Ni sawa na mtu anayetaka kukusahihisha lakini kwanza anaanza kukuporomoshea matusi ya nguoni.. hata kama anachosema ni cha kweli hautamsikiliza!
 
Kama ni watu makini hawataogopa majina wanayoitwa na wachangiaji wa pembeni tu... wao wanaitwa na mkjj na as long as mkjj hana hayo majina... wao wanaweza kuja tu na wasitoe visingizio kuwa membaz wa JF wanawaita majina...

Kwani huyo Karamavi mbona hajasema hivyo? yeye mwenyewe kwanza anapenda jina la Karamavi

Uzuri ni kuwa niliemkusudia kumfikishia ujumbe amenielewa, wewe unaweza kuendelea na ya kwako....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom