Tunahitaji propaganda mpya iliyosimama Kupunguza tatizo la Ajira. Serikali mpoo!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,461
52,106
TUNAHITAJI PROPAGANDA MPYA ILIYOSIMAMA KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Kwa zaidi ya 80% ya maisha ya mwanadamu yanaongozwa na Propaganda. Iwe propaganda nzuri au mbaya. Iwe Kwa wazungu, wachina, waarabu au Waafrika, propaganda Kwa sehemu kubwa ndio hufanya watu wawe na mtazamo Fulani kuhusu mambo/Jambo Fulani.

Kujiona Bora au Duni ni matokeo chanya au Hasi ya Propaganda.

Propaganda inalenga zaidi kugusa sehemu nyeti ya akili na hisia za watu. Ikiwa akili na hisia zitaguswa na kuathirika basi moja Kwa moja maisha ya mtu huathirika.

Taifa lolote au serikali yoyote yenye uwezo wa kucheza na Propaganda ni lazima iwe na nguvu Hasi au chanya kulingana na Aina ya Propaganda.

Wenye macho matatu Kama sio manne tunafahamu, Propaganda ni biashara, hakuna biashara pasipo Propaganda, hakuna media pasipo propaganda, hakuna mahusiano Mema au mabaya pasipo propaganda, hakuna Siasa pasipo propaganda. Propaganda ndio maisha halisi. Hata kwenye ndoa, ili familia ianguke na kuzorota basi mwanaume anapaswa awe madhaifu kwenye kufanya propaganda.

Propaganda Hufanya Jambo lipendwe Sana au lichukiwe kupitiliza. Huwezi kufanya mtu akupende au akuchukie sana pasipo propaganda. Propaganda ni Kama urembo unaoongeza naksi katika Jambo Fulani, pia ni Kama kichocheo cha kuleta chuki iliyozidi.

Kimsingi kwenye hii dunia hakuna tatizo la Ajira. Ila propaganda ndizo zinafanya watu wawe na mtazamo na waone hakuna Ajira.
Kimsingi hakuna tatizo la ukosefu wakazi, Ila propaganda ndio inafanya watu waone hakuna kazi.

Kabla ya ujio wa Elimu ya kizungu ingekuwa ni maajabu ya Dunia kusikia mtu akisema Hana KAZI au AJIRA.

Lakini baada ya ujio WA elimu ya kizungu ambayo ilitiwa nakshi(propaganda) kuwa ndio ufunguo wa maisha, kwamba ukipata elimu utapata maisha mazuri, ika-promotiwa na kufanyiwa propaganda na kila namna.

Huku Wale walioikosa wakizomewa na kutungiwa nyimbo nyingi za kebehi na vijembe. Nani asiyejua wimbo wa "Asiyejua kusoma ni mjinga kabisa?" Nani huyo asiyejua.

Kimsingi Kauli ya kusema elimu ni ufunguo wa maisha ilikuwa propaganda yenye uongo mtamu uliokubalika.
Kusema kupata elimu ni kuwa na maisha mazuri wakati wapo ambao hawajasoma na wanamaisha mazuri kwenye Logic tunasema ni uongo.

Elimu ndio imeleta tatizo la Ajira, na hapa nazungumzia elimu ya kizungu. Najua wengi watanibishia na hii ni kutokana na matokeo ya athari ya propaganda zilizochongwa na watu wajanja Kwa ajili ya biashara.

Elimu ni biashara nzuri Sana. Ili kuifanya biashara hii ni lazima iwepo propaganda Kali itakayoteka visima vya fikra na Hisia za watu.

Kwa Sisi ambao tumeenda shule kidogo tutajua Ile hali ipo Chuo unasoma na jinsi unavyofanya imagination utakavyomaliza shule na kuwa na maisha mazuri. Muono huo tuliokuwa tunauona ni matokeo ya akili na hisia zetu kuchotwa na Propaganda.

Propaganda mara nyingi huleta hofu na utisho katika fikra za watu. Mtu anaathirika kisaikolojia kuwa nisipo pata elimu nimekwisha, sitafanikiwa, Jambo ambalo kimsingi sio kweli.

Kama utaona Vijana waliosoma wanahofu kubwa kuliko ambao hawajasoma. Kijana awapo Chuoni au shuleni ni rahisi kuvunjiwa haki zake Kisa Elimu Kwa maana propaganda umemuambia kuwa elimu ndio kila kitu Jambo ambalo ni uongo wa mchana.

Maprofesa, wakufunzi na waalimu hutisha wanafunzi wanaowafundisha Kwa hadithi za uongo na Kweli ili kuzidi kuwafanya wanafunzi MATEKA wao.

Lengo kubwa la Propaganda za kukosa Ajira ni kupata Watumwa wapya katika Zama mpya katika ulimwengu Mpya.
Watumwa hawa Zama hizi huitwa watumishi au Wafanyakazi..

Propaganda ya tatizo la Ajira ni biashara tamu Sana yenye uchungu Kwa Vijana wa kizazi hiki watokao familia Masikini.

Propaganda ya tatizo la Ajira ni biashara inayowaneemesha zaidi matajiri kuwafanya wazidi kuwa na Utajiri WA kutisha huku Wale waliodanganywa kusoma ni maisha mazuri wakigeuka Watumwa.

Pengine unafikiri nazungumzia Jambo gani, au pengine hunielewi bado, ikiwa ni hivyo nisome polepole Kwa umakini utanielewa.

Propaganda ya tatizo la Ajira ndio inayopelekea Wafanyakazi kuajiriwa Kwa Mshahara mdogo kabisa huku wakizalisha Faida maelfu elfu Kwa matajiri au serikali au mashirika.

Nilitangulia hapo kusema habari za propaganda za elimu ya kizungu kuwa ni ufunguo wa maisha, Kwa mnaokumbuka miisho ya miaka ya tisini na mianzo ya miaka ya elfu mbili jinsi propaganda za kutoa elimu kwenye jamii zilivyopamba Moto.

Lengo la propaganda zile ilipaswa ijitokeze miaka ishirini mpaka hamsini ijayo, na hivi sasa huu ni mwaka wa ishirini kwenda thelasini tangu propaganda hizo kuratibiwa.

Propaganda zile zililenga biashara nzuri Kwa mataifa makubwa na viongozi watakaotawala Ka kila Zama hapa Afrika.

Tayari zimeathiri akili na hisia za vijana waliowengi. Mtu asome mpaka Degree moja au mbili au Stashahada akiwa ameambiwa miaka yote atapata maisha mazuri ambayo Kwa tafsiri rahisi ni kufanya kazi ukiwa kwenye kiyoyozi, Mshahara mzuri, n.k

Alafu Leo hii umuambia mtu huyu akalime, au akauze Dagaa au maembe mtaani😃😃 Thubutu.

Lengo la propaganda Ile ya elimu inakupa maisha mazuri nani ufunguo pekee WA maisha mazuri ni kufanya wasomi kudharau kazi zingine, na hili likishatokea automatically Tatizo la Ajira litajitokeza na halitazuilika.

Nilishasema propaganda ni biashara.
Aidha kudunishwa au kutukuzwa.

Propaganda ya Rangi nyeupe ni Bora na nzuri ni biashara njema inayowatesa Waafrika hasa wanawake zetu.
Kupitia propaganda hii, biashara ya vipodozi imepamba Moto, makampuni yanavuna mapesa kutoka Afrika kila iitwapo leo.

Zipo Propaganda za maumbile Kama uume MREFU, au mwanamke kuwa na matako makubwa.
Hizi zote ni biashara ambazo kimsingi ni ulaghai wa watu Fulani wanaotafuta mapesa Kwa mapesa.

Sitaki kusahau propaganda za Kidini na Imani ambazo zimefanya watu waliopo katika taasisi za Dini kuvuna mamilioni ya Fedha kutoka Kwa waumini wao.

Nikirejea kwenye hoja yangu, dunia haina tatizo la Ajira, na haitakuja kutokea dunia ikawa na tatizo la Ajira. Yaani watu kukosa kazi hiyo haitakuja kutokea KAMWE.

Ila kilichopo ni watu Fulani kutengeneza dunia iwe na ionekane Kama inatatizo la AJIRA. Ili watu wafanyishwe kazi za UTUMWA, na wapatikane Cheap Labour.

NINI KIFANYIKE?

Nafahamu hata nikishauri hakitaweza kufanyiwa Kwa sababu kitagusa maslahi ya Wakubwa wanaopenda kuwa na Mali mara elfu kuliko wenzao.

Labda nishauri Kwa ambao wapo Lower Class;

1. Usichague kazi.

2. Usione aibu kufanya kazi yoyote halali inayokuingizia kipato.

3. Fanya kazi iliyombele yako ilimradi ni halali usisubiri kazi ambayo hujui utaipata lini.

4. Tumia akili zaidi ufanyapo kazi kuliko hisia.

5. Usitafute mwanamke ambaye haithamini kazi yako.

6. Kama wazazi wako wameathiriwa na propaganda za Magharibi au serikali, sio lazima uwaambie unafanya kazi gani endapo utaona wataku-disapoint.

7. Ishi upendavyo ili upate unavyovipenda.

8. Maisha hayasubiriwi. Fanya maisha usitake maisha yafanye Kwa niaba yako.

9. Usimaluamu yeyote, usilaumu serikali. Hakuna aliyepo Kwa ajili yako isipokuwa wewe mwenyewe na aliyekuumba.

10. Pata elimu ili uwe na maarifa ya kufanya kazi yoyote Ile iliyombele yako. Sio upate elimu ili utafute kazi ambayo haipo mbele yako yaani utafute kazi.

Kufikia hapa sina la ziada, na nipumzike sasa.

Ni Yule Mtibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Mbweni, Dar es salaam
 
Back
Top Bottom