Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Tofauti na propaganda za serikali ya wanaccm za kila mwaka, kuwa uchumi wa watanzania unakuwa kwa asilimia kubwa kila mwaka, benki ya Dunia imewashushua waendesha propaganda hizo kwa kueleza ukweli kuwa hali ya maisha ya watanzania walio wengi, hususani wale wa hali ya chini, inazidi kudorora, jinsi miaka inavyokwenda mbele.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Benki ya Dunia, inaeleza kuwa watanzania waliokuwa wakiishi katika hali ya umasikini sana, chini ya dollar moja ya kimarekani, imeongezeka kutoka watanzania milioni 14 mwaka 2018 hadi kufikia zaidi ya watanzania milioni 17 mwishoni maa mwaka 2023.
Taarifa hiyo inapingana vikali na taarifa za (kupikwa) zinazotolewa kila mwaka na serikali hii ya CCM, kuwa hali ya maisha ya watanzania inazidi kuboreka kila mwaka!
Wakati watanzania kila mwaka wanaendelea kulalamika kuhusu gharama za maisha kupanda, serikali ya CCM, imeendelea kutupiga propaganda kuwa hali za maisha ya watanzania inazidi kuboreka kila mwaka.
Katika hali halisi, ingawa benki ya Dunia, imekiri kuwa kuna ongezeko la ukuaji wa uchumi nchini wa asilimia kama 5 hivi, lakini imetahadharisha kuwa ongezeko hilo linawafaidisha watanzania wachache ambao ni matajiri sana.
Kwa hiyo Benki ya Dunia imetutegulia kitendawili cha muda mrefu kilichokuwa kinawasunbua watanzania walio wengi kuwa maisha ya watanzania yanazidi kudorora jinsi siku zinavyozidi kusonga mbele.