Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Ukitaka kujua hapa Tanzania kubambikia watu kesi ni tatizo kubwa basi hudhuria mahakamani mara kwa mara.
Unaweza kusikia mtuhumiwa wa miaka 40 hati yake ya mashitaka ikitaja kuwa ana miaka 21. George Banoba akatajwa kuwa anaitwa Mohamed John. Hii yote tu ni waendesha mashitaka kulazimisha watu wafungwe na wao kupata sifa kuwa wanapiga kazi.
Unaweza kushtushwa na binti aliyepigwa mimba anatishwa amsingizie mshitakiwa ili mradi tu waendesha mashitaka wamfunge mtuhumiwa.
Wapo watu wanakamatwa kwa uzururaji lakini wanapewa kesi za ujambazi mpaka ukweli uje kupatikana mtu anakuwa amesota kama mwaka mzima gerezani.
Ni wazi kuwa kubambikia wananchi kesi ni suala ambalo lipo wazi na wengi wanaumia kwa kufungwa au kukaa mahabusu kwa muda mrefu. Ipo haja sasa mtu akipata madhara ya kubambikiwa kesi aweze nae kufungua kesi na kupata fidia.
Bahati mbaya huwezi kusikia mbunge akihoji au kutaka kuwe na sheria kama hii