Tunahitaji kuwa na sheria itayowapa haki waliobambikiwa kesi kudai fidia

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,513
2,000
Ukitaka kujua hapa Tanzania kubambikia watu kesi ni tatizo kubwa basi hudhuria mahakamani mara kwa mara.

Unaweza kusikia mtuhumiwa wa miaka 40 hati yake ya mashitaka ikitaja kuwa ana miaka 21. George Banoba akatajwa kuwa anaitwa Mohamed John. Hii yote tu ni waendesha mashitaka kulazimisha watu wafungwe na wao kupata sifa kuwa wanapiga kazi.

Unaweza kushtushwa na binti aliyepigwa mimba anatishwa amsingizie mshitakiwa ili mradi tu waendesha mashitaka wamfunge mtuhumiwa.

Wapo watu wanakamatwa kwa uzururaji lakini wanapewa kesi za ujambazi mpaka ukweli uje kupatikana mtu anakuwa amesota kama mwaka mzima gerezani.

Ni wazi kuwa kubambikia wananchi kesi ni suala ambalo lipo wazi na wengi wanaumia kwa kufungwa au kukaa mahabusu kwa muda mrefu. Ipo haja sasa mtu akipata madhara ya kubambikiwa kesi aweze nae kufungua kesi na kupata fidia.

Bahati mbaya huwezi kusikia mbunge akihoji au kutaka kuwe na sheria kama hii
 
Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,716
2,000
Kinga ndio mpango kwa viongozi.

Wabunge wako fiti kusaini posho tu hakuna wakuhoji nini maana ya kinga kwa vipngozi,halafu eti utawala bora ipate fungu kwa mwaka
 
Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,096
2,000
Hakuna Sheria inakataza kudai fidia,

Mbona yapo makesi kibao tu mahakamani ya Malicious Prosecution??
Kawa hiyo leo unakubali hata wale mnaowaita wapinzani,Mimi nawaita wenye mawazo mbadala,wadai fidia sio.Au unamlenga tu kijana wako pendwa.
 
Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,782
2,000
Kawa hiyo leo unakubali hata wale mnaowaita wapinzani,Mimi nawaita wenye mawazo mbadala,wadai fidia sio.Au unamlenga tu kijana wako pendwa.
Hapa naona ni swala la uelewa tu kwa mleta mada pamoja na wewe Ila Sheria haijawahi kukataza mtu yeyote kudai fidia, pale anapohisi ameshitakiwa kimakosa na kadhalilika.

Hilo mbona ni Jambo ambalo liko wazi Wala halihitaji kikao chochote kulipitisha.

Ni uamuzi tu wa mhanga yeyote.
 
Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,096
2,000
Hapa naona ni swala la uelewa tu kwa mleta mada pamoja na wewe Ila Sheria haijawahi kukataza mtu yeyote kudai fidia, pale anapohisi ameshitakiwa kimakosa na kadhalilika.

Hilo mbona ni Jambo ambalo liko wazi Wala halihitaji kikao chochote kulipitisha.

Ni uamuzi tu wa mhanga yeyote.
Kama hayo yanawezekena kwa wote na haki ilikuwa ikizingatiwa mbona nchi ingefilisika kwa kuwalipa fidia wenye mawazo mbadala.Najua enzi hii siyo iliyopita.
 
Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,513
2,000
Hapa naona ni swala la uelewa tu kwa mleta mada pamoja na wewe Ila Sheria haijawahi kukataza mtu yeyote kudai fidia, pale anapohisi ameshitakiwa kimakosa na kadhalilika.

Hilo mbona ni Jambo ambalo liko wazi Wala halihitaji kikao chochote kulipitisha.

Ni uamuzi tu wa mhanga yeyote.
Hakuna kitu kibaya kama kujifanya unajua wakati hujui. Mfano kuna dogo huko Moshi alisingiziwa kumpa uja uzito denti, akapigwa miaka 30. Baadae yule binti anaona huruma kumsingizia mtu. Unadhani kuna sheria hapa bongo inamruhusu kudai fidia huyu dogo?
 
Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,782
2,000
Hakuna kitu kibaya kama kujifanya unajua wakati hujui. Mfano kuna dogo huko Moshi alisingiziwa kumpa uja uzito denti, akapigwa miaka 30. Baadae yule binti anaona huruma kumsingizia mtu. Unadhani kuna sheria hapa bongo inamruhusu kudai fidia huyu dogo?
Sasa si uombe tu kuelimishwa badala ya kujitutumua wakati una argue pumba??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom