Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,733
- 5,489
Ujumbe Kutoka Kwa Kolo Anaeajielewa
Toka sakata la kinidhamu na labda la kijinai lifanyike pale uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha, bado hakuna taswira sahihi ya nini hasa kilichosababisha hali ile na ukweli halisi wa maneno yaliyozungumzwa kwenye eneo husika.
Nani alisema nini na chanzo kilikuwa nini, vyote hivyo havisemwi bali tunasikia maneno ya Upande mmoja zaidi, kuwa Haji Manara alisema hivi na vile, wakati video inaonesha majibizano, je, upande wa pili ulikuwa unasema nini ??, Hatuambiwi !!!
Kesi hii itufungue akili juu ya Sheria na kanuni za makosa zinavyotekelezwa na Kamati ya Maadili dhidi ya mtu yeyote na si kuchagua upande kwa sababu za kishabiki au kutafuta afadhali au kuona kwa kuwa fulani limemfika basi wacha limfike kwa kuwa si mimi lililonifika.
Tunaweza kuanza kwa kusema siku zote mlikuwa wapi wakati fulani au fulani anakumbwa na adhabu kupitia sheria hizo hizo na kudhani hatuna sababu ya kuziongelea sasa kwa upofu ule tuliokuwa nao hapo awali, lakini Shaaban Robert katika Kitabu chake cha Kusadikika aliandika.."Shujaa huwa hapatikani mpaka tukio kubwa litokee."
Itoshe kuona kuwa hili ni tukio kubwa kwa kuwa linahusisha mamlaka kuu ya soka na lilifanyika katika moja ya matukio makubwa na hata waliokuwepo kwenye eneo husika wanatosha kuitwa wakubwa, hivyo wanaosema kwa nini iwe sasa, tunawashauri wanyamaze tu kwa kuwa uwezo wao wa kujua sababu za mambo makubwa kutokea na kuleta mabadiliko ni mdogo na hatuwezi kupoteza muda kuupa nafasi.
Hukumu dhidi ya Manara ituamshe kwenye mambo kadhaa ambayo kesho na Keshokutwa utajikuta mtuhumiwa ni wewe na lazima utiwe hatiani kwa kuwa wanaokushtaki tayari walishajiandaa kukuadhibu.
Ni wazi kuwa Manara alishakuwa na ameshakuwa na Maneno makali ambayo wakati mwingine huleta taharuki na kuamsha hisia hasi dhidi yake au dhidi ya eneo analowajibikia, hilo halina ubishi na ndilo linaloweza kumfanya akawa ameshahukumiwa hata kama ataitwa kujitetea.
Maswali ni mengi kuhusu hukumu dhidi yake lakini ambayo pengine yangeweza kuwa majibu ya leo na kesho kwenye eneo hilo hilo la Kamati ya Maadili ni;
Nani alikuwa mshtaki wa Manara ?
Swali hili limekuwa muhimu sana kwani imekuwa kawaida kusikia mtu ameitwa Kamati ya Maadili bila kujua mshtaki wake hasa ni nani?
Kwenye misingi ya haki lazima awepo mshtaki kwani ndiye atakayetakiwa kutoa au kuleta ushahidi ambao utaondoa shaka ya wenye mamlaka za kuhukumu ili watende haki.
Lakini kwa asili ya kinachoonekana kwa wengi ni wazi kuwa mshtaki wa Manara ndio huyo huyo aliyekuwa mtoa hukumu.
Nani aliyepeleka ushahidi dhidi ya Manara??
Kimsingi lazima mshtaki ambaye hapa ni wazi anahesabika kuwa Rais wa TFF ndiye ambaye alipaswa kupeleka kesi na ushahidi au mashahidi dhidi ya kile kilichoonekana kuwa ni utovu wa nidhamu au kosa lililostahili adhabu, lakini hakuna sehemu yoyote tunayoambiwa kuwa mshtaki au shahidi alitoa ushahidi kadha wa kadha unaomtia hatiani mtuhumiwa.
Kosa dhidi ya Manara ni lipi na nani alitoa ushahidi usioacha shaka??
Hapa ndipo palipojaa mkanganyiko kwa kuwa haionekani popote aliyetakiwa kuwa Mshtaki na Shahidi wa muhimu kujitokeza popote au kuitwa kwenye Kamati husika ili kueleza au kuhojiwa na kuthibitisha makosa dhidi ya Manara, tunachoona ni nukuu tu za maneno kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati kuwa Manara alisikika akisema na sio shahidi au mashahidi walimsikia akisema, na pia watuambie aliposema alijibiwa nini ??
Anyway.
Ni wazi hata kwa muonekano wa video ile isiyokuwa na maneno yanayosikika ilikuwa wazi kuwa kulikuwa na tukio lisilo la kawaida na hivyo haikupaswa kwa mtu yeyote na si Manara pekee, kufanya au kuhusika na tukio lolote linaloleta taharuki au kuvunja sheria kwa sababu yoyote ile.
Suala zima kwa jinsi linavyoonekana kuendeshwa ni wazi linaondoa sifa za kuhukumiana na hata linachafua nafasi ya Urais wa TFF kwa kuwa itaonekana na mpaka sasa inaonekana kama ni hukumu inayotokana na maelekezo au iliyokusudia kulinda tu nafasi ya Urais bila watoa hukumu kujali kuwa hata yeye Rais alipaswa kuitwa na kuhojiwa ukweli wa kile kilichotokea hata kama yeye hakupeleka mashtaka moja kwa moja ili kila mmoja ajue alikuwa na maoni gani, vp kama kesho atajitokeza kwenye Press na kusema walikuwa wanataniana ??.
Wakati wa mzozo ule, Rais alikuwa anajibu nini ??
Video inaonesha kuna majibizano, je Rais alikuwa anajibu nini au alikuwa anamnasihi Haji Manara aende Msikitini kuswali ?? Majibu yake hasa dhidi ya maneno yanayosemwa kuwa makali ya Haji yalikuwa yapi??
Najua ipo furaha kumuona Haji Manara amefungiwa lakini waliomfungia wanatuachia ujumbe gani kuhusu misingi ya kesi na haki zake katika uendeshaji, tunacheka leo kwa Manara, kesho nasi tunangojewa kufanywa mfano kwa Wengine..!!!
Kwa msingi wa hoja zote hapo juu, Sisemi kuwa Manara kaonewa au hajaonewa, bali nasema kuwa haki dhidi ya shauri la Manara ni wazi kuwa haikuonekana kutendeka !!!
Imenyesha sana, panapovuja panabomoka !!!