Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,492
- 40,533
Kuna stori moja niliileta hapa, kuhusu dada mmoja alikuwa mpenzi wangu (mchepuko), alifumaniwa na mumewe kwa njia ya simu akiwa faragha na jamaa mwingine. Ambapo, alipokuwa faragha simu yake kutoka kwa mumewe iliita, na katika zile harakati za kushika simu ikawa imejipokea, na mumewe kusikia yote yaliyokuwa yanaendelea.
Kutokana na hilo sakata, mumewe alikasirika sana na kumpa vitisho vikali; ingawa hata mimi iliniuma sana kugundua kuwa kuna mtu mwingine anakula huo mzigo. Kwa upande wangu, nilivunja mawasiliano kwa hasira na kufuta namba yake. Hivi karibuni, nilijikuta naanza kumtafuta kwa kufikiria namba zake kichwani. Na simu ilipoita, aliipokea na tukazungumza ya kwetu na kutakiana heri ya mwaka mpya n.k
Cha kushangaza nikawa namtafuta kwa spidi sana, mara kila baada ya masaa machache nampigia simu ili tuongee. Ndipo leo likaja wazo, la kutaka nimuulize aliporudi kwa mumewe lile sakata walilimalizaje! Ndipo mtoto akafunguka,'Kuna rafiki yangu alinielekeza sehemu, na nilipofika huko nilikutana na mtaalamu, na kuniomba majina ya mume wangu, ndipo akamfanyia ulozi na ndani ya dakika chache mume alinipigia simu huku akilia akiniomba msamaha' na 'nilipofika nyumbani mume alitoka kazini muda wote anataka akae na mimi kutokana na mahaba mazito aliyonayo kwangu'.
Alivyoniambia hivyo, nikajifanya kama simu imeisha dakika na kukata simu...ingawa alipiga tena, na kumdanganya simu imeisha salio. Nikawa najiuliza si ajabu na hii spidi ya kumtafuta hii ameshanifanyia majambozi. Hapa nilipo, najaribu kuisahau namba yake ili nisimtafute tena, na hata kama itatokea anataka mechi nitaweka visingizio vya kujiepusha naye; kwa sababu huu sio uungwana, ni kurudishana nyuma kimaendeleo.
Tuwe makini, wanawake wanatufanyia ulozi sana kwenye mahusiano.