Vijana wa mjini wamekuwa washirikina sana, punguzeni ulozi jamani

Mijadala Migumu

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
288
283
Miaka ya zamani watu waliokuwa wakiamini mambo ya shirki na ulozi walikuwa ni watu wazima haswa, hawa ndiyo walikuwa wateja wakubwa kwenye vilinge vya waganga.

Kiukweli mambo yamebadilika sana sasahivi vijana wadogo Miaka 20 mpaka 40 ndiyo wamekuwa wateja wakubwa wa waganga na waganguzi.

Siyo vijana wa kike wala wa kiume, yaani wote wamekuwa walozi, wachawi, washirikina haswa. Ufuatao hapa chini uhalisia wa mambo.

1. Huyu ni rafiki yangu wa siku nyingi tulisoma wote mkoani, badae tukaja onana town. Umri 32 Kidume kina majumba magari na biashara kubwa ila kila mwezi lazima apeleke chochote kwa mganguzi wake na kafara za kitoweo zitolewe ili abust biashara zake. Humwambii chochote kuhusu mganga wake.

2. Binti miaka 29. Huyu ni mfanyakazi mwenzangu na ni swahiba wangu sana uwa tunaongea mengi. Aliniambia mumewe alikuwa mgumu sana mwanzoni kukubali kupeleka mahali kwao na binti. Ila binti alienda kwa mganga jamaa akachotwa akili, mahali ikapelekwa ukweni na ndani mwezi tuu ndoa ikafungwa. Huyu naye mpaka leo hajaacha kwenda kwa mganga wake, uwa anasema jamaa akianza kujitambua tuu, anarudigi kwa mganga wake ku update dawa.

3. Jamaa tulisoma wote chuo X, baada ya ku graduate wengine tukakosa hata pa kujitolea. Ila kwake yeye mambo yalikuwa tofauti. Hakuwa na connection wala hakuwa mzuri class. Ila kila alikopita kuomba kazi walikuwa wanampa mkataba wa kuanza kazi bila interview yoyote, haulizwi cha work experience wala nini. Mshikaji alikuwa akiaacha kazi hapa kesho kaajiriwa pale. Jamaa alikuwa anatembea na kipande cha sanda kwenye wallet kila aendako. Kuna siku alidondosha wallet yake tulipokuwa chuo ila hatutilia maanani. Wakati sasa tunaangaika kutafuta kazi jamaa alikuwa anatucheka sana na kutuambia tumeshindwa ku control nature.

Ngoja narudi.
 
2. Binti miaka 29. Huyu ni mfanyakazi mwenzangu na ni swahiba wangu sana uwa tunaongea mengi. Aliniambia mumewe alikuwa mgumu sana mwanzoni kukubali kupeleka mahali kwao na binti. Ila binti alienda kwa mganga jamaa akachotwa akili, mahali ikapelekwa ukweni na ndani mwezi tuu ndoa ikafungwa. Huyu naye mpaka leo hajaacha kwenda kwa mganga wake, uwa anasema jamaa akianza kujitambua tuu, anarudigi kwa mganga wake ku update dawa.
Kuna mdada alijaribu kuniroga mpaka akaenda na kwa Mwamposa ngoma ikashindikana.

Huwa nawashangaa sana wanaume wanaorogeka
 
Back
Top Bottom