Tunafanyiwa ulozi sana kwenye mahusiano

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,189
39,954
Kuna stori moja niliileta hapa, kuhusu dada mmoja alikuwa mpenzi wangu (mchepuko), alifumaniwa na mumewe kwa njia ya simu akiwa faragha na jamaa mwingine. Ambapo, alipokuwa faragha simu yake kutoka kwa mumewe iliita, na katika zile harakati za kushika simu ikawa imejipokea, na mumewe kusikia yote yaliyokuwa yanaendelea.

Kutokana na hilo sakata, mumewe alikasirika sana na kumpa vitisho vikali; ingawa hata mimi iliniuma sana kugundua kuwa kuna mtu mwingine anakula huo mzigo. Kwa upande wangu, nilivunja mawasiliano kwa hasira na kufuta namba yake. Hivi karibuni, nilijikuta naanza kumtafuta kwa kufikiria namba zake kichwani. Na simu ilipoita, aliipokea na tukazungumza ya kwetu na kutakiana heri ya mwaka mpya n.k

Cha kushangaza nikawa namtafuta kwa spidi sana, mara kila baada ya masaa machache nampigia simu ili tuongee. Ndipo leo likaja wazo, la kutaka nimuulize aliporudi kwa mumewe lile sakata walilimalizaje! Ndipo mtoto akafunguka,'Kuna rafiki yangu alinielekeza sehemu, na nilipofika huko nilikutana na mtaalamu, na kuniomba majina ya mume wangu, ndipo akamfanyia ulozi na ndani ya dakika chache mume alinipigia simu huku akilia akiniomba msamaha' na 'nilipofika nyumbani mume alitoka kazini muda wote anataka akae na mimi kutokana na mahaba mazito aliyonayo kwangu'.

Alivyoniambia hivyo, nikajifanya kama simu imeisha dakika na kukata simu...ingawa alipiga tena, na kumdanganya simu imeisha salio. Nikawa najiuliza si ajabu na hii spidi ya kumtafuta hii ameshanifanyia majambozi. Hapa nilipo, najaribu kuisahau namba yake ili nisimtafute tena, na hata kama itatokea anataka mechi nitaweka visingizio vya kujiepusha naye; kwa sababu huu sio uungwana, ni kurudishana nyuma kimaendeleo.

Tuwe makini, wanawake wanatufanyia ulozi sana kwenye mahusiano.
 
Kwa wachungaji matapeli wa Upako,vitambaa,mafuta, na kwa waganga wa kienyeji bila shaka unajionea Mwenyewe wateja wakubwa kina nani??

Akili Ku mkichwa mjini hapa.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Inabidi kwenda kwa mwendo wa pole pole, kuna sehemu unaweza kuingia ukajikuta unatimiza ndoto za mwenzako, za kwako hazitimii.
 
Hii ni kweli kabisa .....

Kuna gruop la watsaap la wamama nillingia kinyamela ili kukamilisha research yangu........Kama CIA m.bobezi

Aiseee Mambo ambayo wamama wanashauriana humo...kuhusu Mambo ya kuwafunga wanaume.....ni hatari tupu......ukiona unaweza ....kimbia jukumu la kuoa

Wanaume ....maombi kwa MUNGU ni muhimu
 
Mimi naoa na wakunifunga hayupo na hatakuwepo.
 
Kuna stori moja niliileta hapa, kuhusu dada mmoja alikuwa mpenzi wangu (mchepuko), alifumaniwa na mumewe kwa njia ya simu akiwa faragha na jamaa mwingine. Ambapo, alipokuwa faragha simu yake kutoka kwa mumewe iliita, na katika zile harakati za kushika simu ikawa imejipokea, na mumewe kusikia yote yaliyokuwa yanaendelea.
Dada na mama zetu tunapaswa kuwaombea Sana maake itafikia kipindi tututamlazimisha mungu alete kiyama hata kama alishatoa free offer ya time maake maajabu ya siku hasa yanayofanywa na Ke ni hatari mara ulozi, Mirinda nyeusi,

Ewe mungu baba naomba utufutie mazambi sisi wakosefu.... Amiin
 
Kuna stori moja niliileta hapa, kuhusu dada mmoja alikuwa mpenzi wangu (mchepuko), alifumaniwa na mumewe kwa njia ya simu akiwa faragha na jamaa mwingine. Ambapo, alipokuwa faragha simu yake kutoka kwa mumewe iliita, na katika zile harakati za kushika simu ikawa imejipokea, na mumewe kusikia yote yaliyokuwa yanaendelea.

Kutokana na hilo sakata, mumewe alikasirika sana na kumpa vitisho vikali; ingawa hata mimi iliniuma sana kugundua kuwa kuna mtu mwingine
Hujafanyiwa ulozi. Ww una addiction. Break hiyo addiction na uta masahau. Lakin kuwa makini maana maamuzi yanatoka moyoni
 
Kuna stori moja niliileta hapa, kuhusu dada mmoja alikuwa mpenzi wangu (mchepuko), alifumaniwa na mumewe kwa njia ya simu akiwa faragha na jamaa mwingine. Ambapo, alipokuwa faragha simu yake kutoka kwa mumewe iliita, na katika zile harakati za kushika simu ikawa imejipokea, na mumewe kusikia yote yaliyokuwa yanaendelea.
Kwa maelezo Yako hapo juu wewe ndiye ulikuwa naye sikuhiyo mumewe anampigia simu
 
Hii ni kweli kabisa .....

Kuna gruop la watsaap la wamama nillingia kinyamela ili kukamilisha research yangu........Kama CIA m.bobezi

Aiseee Mambo ambayo wamama wanashauriana humo...kuhusu Mambo ya kuwafunga wanaume.....ni hatari tupu......ukiona unaweza ....kimbia jukumu la kuoa

Wanaume ....maombi kwa MUNGU ni muhimu
Maombi gani wakati maombi yao wanategemea wake zao wao wapo busy acha warogeke, tu!
 
Back
Top Bottom