Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,949
- 6,874
Mimi hata siwaelewi wakina Zitto. Pamekuwa na chaguzi kiasi toka ile ya 2020 na ACT wameshiriki kikamilifu. Kama sikosei ACT wameshinda moja tu tena kwa mbinde. Kuna chaguzi nyingine huku bara wamelalamika kufanyiwa ubabe ule ule wa 2020. Ya mwisho ndio hawakupata hata kura 200. Sasa ikiwa wanachezewa rafu katika nchi ambayo wao ni washiriki kwenye utawala nini kinawaamisha kuwa 2025 hali itakuwa tofauti? Labda kama wanategemea hisani.Wasi wasi wa ACT ni kuwa kuna uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. ACT wanaamini watashinda chaguzi hizo. Hivi wakipata viti 5000 dhidi ya 40,000 kuna maana gani?
ACT wanaamini kuna uchaguzi 2025 na Tume huruikiwepo watashinda. Hivi wakishinda viti 50 vya ubunge dhidi ya 200 vya CCM wataleta mabadiliko gani? Hapo si ndipo watapiga mhuri kwa CCM kufanya mauza uza yao.
Kosa la ACT ni lile walilofanya Chadema mwaka 2010. JK alitangaza kuanzishwa mchakato wa katiba mpya. CDM wakasema Rais amefanya jambo jema na Wamefarijika. Tuliwaambi kuwa hiyo si njia sahihi, mchakato ulitakiwa uanzie Bungeni ili waweze kuuratibu
Matokeo yake mchakato ukawa mali ya 'Rais' na matokeo yake tunayajua
Hilo ndilo kosa la ACT kutaka Tume huru na Wajumbe wake wapatikane kwa mazingira ya sasa
Haraka ni ya nini ACT?
Fatma Karume alitoa pendekezo zuri sana kuhusiana na cheo cha Spika. Kwa vile inaelekea Spika anajiona kuwa ni Rais mtarajiwa basi anaona ni muhimu ajipendekeze kwa mamlaka yenye nguvu ya kuteua mgombea urais. Fatma alishauri kuwa ili kuepukana na tamaa hizo, Katiba imzuie Spika kugombea nafasi yeyote ya kisiasa muhula wake utakapoisha.
Hii itaondoa uwezekano wa kuwa corrupted kwa ahadi ya cheo cha kisiasa. Mimi nashauri iwe hivi kwa Jaji Mkuu, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na ile ya Vyama vya Siasa. Aidha, wasimamizi wote wa uchaguzi na wakuu wa vyombo vya usalama nao wasiruhusiwe kugombea kwenye chaguzi kuu mbili baada ya kutoka kwenye nafasi yao. Kwenye uspika, iwekwe wazi kuwa sio lazima kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na mara ukichaguliwa hauruhusiwi kushiriki katika shughuli zozote za kisiasa za chama chako ( hamna mambo ya kuwa mjumbe wa NEC n.k.).
Mheshimiwa Rais anyang'anywe pia mamlaka ya kuwaondoa kwenye nafasi zao (kwa kuwapa kazi nyingine, kuwapandisha vyeo n.k) bila kutoa sababu inayoeleweka ambayo itakubaliwa na Tume itakayoundwa (kama Spika, tume iwe na maspika kutoka Jumuia ya Madola). Nadhani tukifanya hivi tutapata watumishi ambao wataweka taifa mbele na sio chama chao cha siasa.
Amandla...